Watoto wa 4G wana maswali magumu sana. Wazazi jiandaeni

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
214
250
Kabinti kangu ka miaka mitano (05) kameniuliza maswali yafuatayo:-

* Baba kwanini mapaja yetu ni makubwa kuliko miguu, wakati miguu ndio inayobeba mwili wote?

*Na juzi kati aliniuliza, "kwanini mama au wewe unapokuwa unataka kubadilisha nguo huwa haumfukuzi mama au wewe huwa haumpishi mama?"

Swali la kwanza nilishindwa kujibu kwa kweli;

Swali la pili, nilijibu kuwa mama huwa simfukuzi kwa kuwa yeye ni mkubwa sana. Akaniuliza, mbona dada (msichana wa kazi) huwa haingii na wakati yeye pia ni mkubwa?

*Nahisi hakuridhika na majibu yangu

Mmh.. Hawa watoto hawa! Jipangeni wazazi/wazazi watarajiwa.
 
Khakha

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
2,984
1,500
Mkuu nyumba unayoishi ni self au three roomed? That is huku chumba katikati sebule?
 
Khakha

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
2,984
1,500
Mimi naishi nyumba ya peke yangu. Vyumba vitatu vya kulala. Sitting na dinning na stoo na public toilet. Chumba changu kinajitegemea. Na nyumba yangu ina fence. Ni nyumba nzuri kwa mtu wa kipato cha kati.

Nasubiri mchango wako
Mkuu kwa sasa hivi ninafanya upembuzi yakinifu khs hili swala. Ila "over the counter remedy ya sasa ni, Google- " Developmental milestones of a 5 years old girl" utapewa kila kitu. Km ni tofauti basi kuna kitu. But just go there! Carpe diem!
 
Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
300
250
Kabinti kangu ka miaka mitano (05) kameniuliza maswali yafuatayo:-

* Baba kwa nini mapaja yetu ni makubwa kuliko miguu, wakati miguu ndio inayobeba mwili wote?

*Na juzi kati aliniuliza, "kwa nini mama au wewe unapokuwa unataka kubadilisha nguo huwa haumfukuzi mama au wewe huwa haumpishi mama?"

Swali la kwanza nilishindwa kujibu kwa kweli.

Swali la pili, nilijibu kuwa mama huwa simfukuzi kwa kuwa yeye ni mkubwa sana. Akaniuliza, mbona dada (msichana wa kazi) huwa haingii na wakati yeye pia ni mkubwa?
*Nahisi hakuridhika na majibu yangu

Mmh.. Hawa watoto hawa!! Jipangeni wazazi/wazazi watarajiwa.
Very technical question.

Kwa nini miguu ni myembamba kuliko mapaja, wakati miguu ndio inabeba mwili wote? Majibu ya kisayansi yanahitajika. Sio blah blah
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,784
2,000
Unapokuwa na mtoto anayependa kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali kama hayo jitahidi kumpa majibu fasaha na halisi.
Majibu unayompa wakati huu ataishi nayo kama vile ndo reality.
Sasa kama ukimlisha tango pori ataishi nalo kama vile ndo reality.....Matokeo yake watoto wanalishwa myths mfano watoto huletwa na mabox.

Mwishowe mtoto atakuwa goigoi maana wakati alipotakiwa kuelewa mambo muhimu, wazazi aidha kwa kutokujua ama kwa kuhofia kumwambia ukweli, wao walimlisha myths.

Wazazi wajitahidi kuwafundisha watoto wangali katika umri mdogo.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,826
2,000
kikaniki mkuu nimempenda bure mtoto wako, si mbaya ukianza kumuelezea vitu taratibu, wenzetu wanaamini unavyowekeza kwa mtoto ndiyo matokeo ya maisha yake mbele yatakavyokuwa. Si muda mrefu sana tangia nimefahamu hii na ni rahisi kufahamu kwanini mapaja yetu ni makubwa kuliko miguu.
Weight, mass and gravity
People often confuse mass and weight. Remember that weight is a force, and is measured in newtons. Mass is measured in kilograms (kg).
Mass
The mass of an object is the amount of matter or "stuff" it contains. The more matter an object contains, the greater its mass. An elephant contains more matter than a mouse, so it has a greater mass. Mass is measured in kilograms, kg, or grams, g.
A 100 kg object has a greater mass than a 5 kg object. Remember an object's mass stays the same wherever it is.
Gravity
All objects have a force that attracts them towards each other. This is called gravity. Even you attract other objects to you because of gravity, but you have too little mass for the force to be very strong.

Gravitational force increases when:
  • the masses are bigger

  • the objects are closer
Gravity only becomes noticeable when there is a really massive object like a moon, planet or star. We are pulled down towards the ground because of gravity. The gravitational force pulls in the direction towards the centre of the Earth.
 
goldie ink

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
5,662
2,000
Mwambie mtoto ukweli wala usidanganye na umpe majibu yatakayo mridhisha, kuweni wazi kwa watoto wenu huna haja kuficha kitu chochote.........
 
KISHINDO

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
1,747
2,000
Yapo mengi ya kujiuliza kuhusu huyo mtoto.

Kwanza alijuaje kuwa mama yake huwa anashuhudia babake akivaa nguo?

Pili, kuhusu swali la mapaja: ungemwambia kuwa yako hivyo kwa sababu Mungu alipomwumba mwanadamu aliifanya miguu iwe na nguvu nyingi lakini nyama chache. Unaendelea.......Kama miguu ingekuwa minene na mapaja yakawa membamba basi mwanadamu asingeweza kutembea, pia asingeweza kukimbia au kupiga teke kitu.

Ningemjibu hivyo, angeelewa.
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
9,105
2,000
Unapokuwa na mtoto anayependa kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali kama hayo jitahidi kumpa majibu fasaha na halisi.
Majibu unayompa wakati huu ataishi nayo kama vile ndo reality.
Sasa kama ukimlisha tango pori ataishi nalo kama vile ndo reality.....Matokeo yake watoto wanalishwa myths mfano watoto huletwa na mabox.

Mwishowe mtoto atakuwa goigoi maana wakati alipotakiwa kuelewa mambo muhimu, wazazi aidha kwa kutokujua ama kwa kuhofia kumwambia ukweli, wao walimlisha myths.

Wazazi wajitahidi kuwafundisha watoto wangali katika umri mdogo.
Kwa hiyo mkuu ulitaka pale alipoulizwa kwa nini huwa baba anapovaa nguo hampishi mamiye......angemjibu kuwa wao wanatazamana nyuchi ama ajibu vipi labda maana ni changamoto!
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,784
2,000
Kwa hiyo mkuu ulitaka pale alipoulizwa kwa nini huwa baba anapovaa nguo hampishi mamiye......angemjibu kuwa wao wanatazamana nyuchi ama ajibu vipi labda maana ni changamoto!
Angemwambia Baba na Mama ni watu wazima walio oana.
Wanaruhusiwa kuishi kwa pamoja.

Hapo ndipo amfundishe mtoto maana ya ndoa na familiya.

Bora amjibu walau kwa ufupi ila kwa ukweli kuliko kumdanganya.
 
kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
214
250
kikaniki mkuu nimempenda bure mtoto wako, si mbaya ukianza kumuelezea vitu taratibu, wenzetu wanaamini unavyowekeza kwa mtoto ndiyo matokeo ya maisha yake mbele yatakavyokuwa. Si muda mrefu sana tangia nimefahamu hii na ni rahisi kufahamu kwanini mapaja yetu ni makubwa kuliko miguu.
Weight, mass and gravity
People often confuse mass and weight. Remember that weight is a force, and is measured in newtons. Mass is measured in kilograms (kg).
Mass
The mass of an object is the amount of matter or "stuff" it contains. The more matter an object contains, the greater its mass. An elephant contains more matter than a mouse, so it has a greater mass. Mass is measured in kilograms, kg, or grams, g.
A 100 kg object has a greater mass than a 5 kg object. Remember an object's mass stays the same wherever it is.
Gravity
All objects have a force that attracts them towards each other. This is called gravity. Even you attract other objects to you because of gravity, but you have too little mass for the force to be very strong.

Gravitational force increases when:
  • the masses are bigger

  • the objects are closer
Gravity only becomes noticeable when there is a really massive object like a moon, planet or star. We are pulled down towards the ground because of gravity. The gravitational force pulls in the direction towards the centre of the Earth.
Asante sana kwa majibu yako Sky Eclat
 
nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
3,949
2,000
...kweli watoto hawa wa 4G si mchezo...mimi ka kwangu kabinti ka miaka hiyo hiyo 5 ameniuliza eti dad kwanini mchana tunakua macho na usiku tunalala?...swali hili hata mtu mzima wa chuo kikuu hawezi kulijibu kama hajasoma human physiology...
 
hps300

Senior Member
Feb 20, 2016
170
250
Yapo mengi ya kujiuliza kuhusu huyo mtoto.

Kwanza alijuaje kuwa mama yake huwa anashuhudia babake akivaa nguo?

Pili, kuhusu swali la mapaja: ungemwambia kuwa yako hivyo kwa sababu Mungu alipomwumba mwanadamu aliifanya miguu iwe na nguvu nyingi lakini nyama chache. Unaendelea.......Kama miguu ingekuwa minene na mapaja yakawa membamba basi mwanadamu asingeweza kutembea, pia asingeweza kukimbia au kupiga teke kitu.

Ningemjibu hivyo, angeelewa.
Kwanza nikubaliane na mleta mada kuwa watoto wa sasa wana maswali technical sana, mimi nimekuwa nikikumbana na maswali yanayoendana na hayo kutoka kwa binti yangu (miaka 7) Darasa la pili.

Kwanza alijuaje kuwa mama yake huwa anashuhudia babake akivaa nguo?

Ikiwa unaishi nyumba ambayo ni ya kifamilia zaidi ina maana utaoga na kuvaa ukiwa chumbani, na kwa wakati huo pia mama au mke anaweza kuingia na si mtoto. Hilo linasababisha yeye aweze kujiuliza kwa nini? Pia naamini kuna wakati unapokuwa chumbani ktk hali ya kawaida mtoto ataingia pia, ama akihitaji kitu toka kwa mama ama baba,

Kuhusu mapaja umjibu vizuri asante.
 
hps300

Senior Member
Feb 20, 2016
170
250
Kabinti kangu ka miaka mitano (05) kameniuliza maswali yafuatayo:-

* Baba kwa nini mapaja yetu ni makubwa kuliko miguu, wakati miguu ndio inayobeba mwili wote?

*Na juzi kati aliniuliza, "kwa nini mama au wewe unapokuwa unataka kubadilisha nguo huwa haumfukuzi mama au wewe huwa haumpishi mama?"

Swali la kwanza nilishindwa kujibu kwa kweli.

Swali la pili, nilijibu kuwa mama huwa simfukuzi kwa kuwa yeye ni mkubwa sana. Akaniuliza, mbona dada (msichana wa kazi) huwa haingii na wakati yeye pia ni mkubwa?
*Nahisi hakuridhika na majibu yangu

Mmh.. Hawa watoto hawa!! Jipangeni wazazi/wazazi watarajiwa.
Usijali sana uelewa wa watoto wa sasa ni mkubwa sana kutokana na urahisi wa kupata taarifa ukilinganisha na miaka ya nyuma (80 and beyond), miaka kadhaa iliopita kuanza darasa la kwanza mtoto alitakiwa mkono wake uweze kugusa sikio la upande wa pili, kimsingi kipindi hicho lazima awe na miaka 10 hadi 12. Leo miaka 12 mtoto yuko form one, form two ama ana maliza darasa la saba,

Kikubwa jaribu kuwa unatafuta majibu yanayoendana na umri wake, binti yangu yeye siku moja alimwuliza mamake kuwa nimeona kuku anapotolea yai, je mimi nilipitia wapi kutoka tumboni?

Siku nyingine kanichapa mimi swali baada ya kumwacha nyumbani yeye na msichana wa kazi kwa siku mbili mimi na mke wangu tukiwa safarini. Nilivorudi akaanza kwa kuniuliza hivi ktk watoto wako yupi unampenda sana? nikamwambia wote, hakuridhika akasema nataka kujua yule unayempenda sana sana, nikagundua kitu nikamjibu kuwa mimi nampenda sana sana yule anayefanya vizuri shuleni kwa maana ya kuwa namba 1 hadi 3.

Akaja na swali la pili ambalo nalenyewe lilianza kama mazungumzo ya kawaida, kuwa mliondoka na gari mkatuacha mimi na dada ( msichana wa kazi) akauliza dada anajua kundesha gari nika mwambia hajui, akijua utampa aendeshe nikamwambia hapana, akauliza kwa nini nikamwambia kwa sababu naipenda sana gari yangu. Hapo ndo niliingia kwenye mtego wake pasipo kujua, akanambia kwa hiyo mimi hunipendi? nikamwambia nakupenda, Swali tena mbona mimi mnaniacha na dada?
 
Evolution zamani ilikuwa ni kubadilika kiumbo, binadamu alikuwa sokwe (Homo habilis) hadi binadamu katika umbo la sasa (Homo sapiens).

Kwa sasa binadamu habadiliki umbo, anabadilika akili na uwezo wa kufikiri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom