Watoto kukosa vyumba vya madarasa alaumiwe Nani?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Ilijulikana mapema kuwa elimu bila malipo ingesababisha watoto wengi kwenda shule na hatimae kufaulu wengi kuliko kawaida. Nani hakuwa na uelewa wa aina hii?

Watendaji wanamuangusha mhe. Rais Kwa jitihada zake mbalimbali. Tulitarajia watendaji wakuu wangemshauri Rais kuhusu projections mbalimbali baada ya interventions zake mbalimbali. Sasa hivi tunaonekana kama vile tunafanya mambo bila kuwa na mipango. Eti idadi kubwa ya watoto wamefaulu lakini hawana vyumba vya madarasa, hawa watendaji wanastahili kumbua Tu. Hawa wanafunzi walikuwa na kila aina ya dalili kuwa wataenda kufaulu wengi mwaka huu kutoka na yale yote yanafanywa na serikali kwenye elimu. Kwanini watendaji wasilione hili mapema?

Rais wetu anakazania uchumi wa viwanda, viwanda vingi vinajengwa na kuzalisha bidhaa nyingi za viwandani. Lakini watendaji wake hawafanyi lolote sasa katika kuwaandaa wananchi ili wawe na uwezo wa kuzikununua bidhaa hizo za viwandani. Soko la bidhaa hizo litakuwa wapi kama wakulima walio wengi hawana vyanzo thabiti vya kupata hela?, wafanyakazi wana mishahara midogo sana isiyomuwezesha mfanyakazi kununua mifuko 20 ya cement Kwa mwezi na bado akaendelea na maisha yake ya kupata mahitaji yake Kwa mwezi huo. Mabenki yetu yanatoza riba kubwa sana na wananchi wengi hawakopesheki.
Ukienda nchi za viwanda utakuta watu wake wengi wananunua vitu vyao Kwa njia ya mikopo nafuu sana, na mishahara ya watumishi iko juu ili kumudu kuvinunua na hata kulipa kodi. Haya yote watendaji wetu wanayafahamu lakini wako kimya hari hapo viwanda vyetu vitakapofungwa Kwa bidhaa zao kukosa wanunuzi. Hili ni balaa la watanzania

Tunasubiri yatokee ndiyo tuchukue hatua. Hebu tumsaidie Rais wetu.
 
Back
Top Bottom