Waziri Dkt. Kijaji Awaasa Vijana Kufanya Kazi kwa Uadilifu na Kujituma Wanapopata Ajira Viwandani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Waziri Dkt. Kijaji Awaasa Vijana Kufanya Kazi kwa Uadilifu na Kujituma Wanapopata Ajira Viwandani

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ametoa rai kwa vijana wa kitanzania kuwa na uadilifu na kujituma wanapopata ajira viwandani ili waendelee kunufaika kwa pamoja na kuimarisha uchumi wa mmoja mmoja na Taifa lkwa ujumla.

Dkt. Kijaji amebainisha hayo Desemba 21, 2023 jijini Dar es Salaam alipotembelea Kiwanda cha Chemicotex kilichopo Mbezi Beach Jogoo jijini Dar es Salaam lenye eneo la hekari 17 na viwanda mbalimbali kuona bidhaa wanazozalisha pamoja na kuikiliza na kutatua changamoto zilizopo kiwandani hapo.

"Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji pamoja na wafanyabiashara waliokuja kuwekeza katika viwanda na wazalisha bidhaa kwa amani na utulivu "Amesema Dkt.Kijaji.

Ameeleza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoenda kuhitimishwa 2025 na Dira inayoandaliwa sasa inatoa mwanga mkubwa kwa wenye viwanda kuendelea kuja Tanzania na kuwekeza kwa kuwa viwanda ni sehemu inayoajiri watanzania wengi.

Naye Mwenyekiti wa Kiwanda cha Chemicotex, Yogesh Manek amesema katika kiwanda hicho wanazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo dawa za meno whitedent vipodozi na vinginevyo.

"Asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia bidhaa ya Kiwanda hiki tumeajiri jumla ya watu 1000 kati ya hao 550 wanawake na 450 wanaume na walemavu 6 hii ni fursa kwa mtu yeyote anataka kufanya kazi,"amesema Manek.

Aidha, amesema hali ya biashara kwa sasa ni nzuri kwa sababu wanafursa ya kufanya kazi na wanapeleka bidhaa zao nchi sita ikiwemo Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi, Congo pamoja na soko la Tanzania.
 

Attachments

  • GB4jhQCWAAA4USn.jpg
    GB4jhQCWAAA4USn.jpg
    267.2 KB · Views: 3
  • GB4jhQAWoAAR-Vm.jpg
    GB4jhQAWoAAR-Vm.jpg
    196 KB · Views: 3
  • GB4jhQEWUAMIWfy.jpg
    GB4jhQEWUAMIWfy.jpg
    237.7 KB · Views: 3
  • GB4jhQFX0AIboQp.jpg
    GB4jhQFX0AIboQp.jpg
    418.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom