View attachment 420848
Hii mada haina mahusiano na kile kilichotokea mahakamani leo wala kile kinachosemwa semwa kuhusu yule mhanga wa tukio husika. Hii ni kujaribu kuchambua kwa undani zaidi kile kitendo cha kumng'oa mtu macho na wale watetezi kusema kuwa mtuhumiwa ni mtu mzuri mcheshi na mshika dini sana kiasi kwamba hawezi kufanya hivyo.
Kuna mengi hayakuzingatiwa kwenye huo utetezi, hii ni kawaida kwakuwa nia ilikuwa ni kutetea hasa kutokana na hao watetezi jinsi walivyomfahamu mtuhumiwa na kufanya naye kazi. Mtu mbaya hawezi kuwa mbaya kwa wote na mtu mwema pia hawezi kuwa mwema kwa wote hata kama angekuwa mpole kama hua kuna degree za vichokoo vya kihisia huweza kumfanya abadilike na kuwa mtu mwingine kabisa ndani ya dakika moja.
Moyo wa mtu ni kiza kinene!ni ngumu kujua kilichomo ndani ya giza.
View attachment 420790
Dhana ya kuwa mtu mwema mpole na mcheshi haiondoi ile roho ya kinyama aliyonayo binadamu yoyote yule. Huyu mtuhumiwa kwa jina la utani la scorpion au Nge tayari alikuwa na degree za vichokoo hasi mwilini tangu udogoni alipokuwa anaonewa na wengine! Vichokoo na vichocheo hasi hivyo vilimfanya mpaka akaamua kuingia kwenye kufanya mazoezi makali sana ya mapigano na ulinzi binafsi na kwa maneno yake alishawahi kumshikisha mbaya wake adabu kwa kipigo kitakatifu! Hii ni roho ya kisasi yenye viashiria vya ukatili.
Kigezo cha kushika dini
Kiasili dini ililetwa kuwa daraja kati ya Mungu na wanadamu, ilichukuliwa kama kitu chema sana lakini ni kupitia dini hiyo hiyo imepoteza watu kwa maelfu! Dini imetumika kuua na kufanya mambo mabaya kabisa katika jamii.
Mifano ipo mingi na mfano wa hivi karibuni kabisa ni ule wa Dodoma yule aliyesababisha mauti ya wale watafiti! Washika dini wamegeuka kuwa watu wa kuogopwa siku hizi si kwa imani zao bali matendo yao.
Huyu bwana alikuwa mfanya mazoezi makali ya mapigano hasa karate na boxing! Wacheza karate na boxing ni wakorofi tofauti na wacheza kung fu na tai chi...sababu ni moja kwamba karate na boxing zinatumia nguvu za mwili wakati kung fu na tai chi vinatumia vital power nguvu ya ndani.
Bila kujali unajifunza kipi kati ya hivyo ni lazima upate kujifunza na masomo ya darasani pia kuhusiana na mojawapo ya hilo na somo muhimu ni humanity loving kindness na compassion (ubinadamu upendo na huruma). Usipojifunza ukayaelewa haya vizuri ukakimbilia tu kwenye mazoezi athari zake ni kutaka kuonyesha ubabe wako hata kwa wasiostahili.
Wengi wa wanamichezo wetu kwenye hii field wanakosa elimu hiyo ya darasani ndio maana wanakuwa wakorofi na ubabe mwingi. Kwahiyo huyu mtuhumiwa alikuwa na dalili zote na viashiria vyote vya kufanya kile kinachosemekana amekifanya! Ana mazoezi ya kutosha jinsi ya kukaba jinsi ya kutoboa macho nk nk lakini hana pa kujaribia! Mikono inawasha kikitokea kisababishi chochote lazima vile vichokoo hasi viamrishe mwili ufanye kazi.
Nimeongea kwa muktadha wa ujumla kutokana na kile kilichotokea