Water bridge ...Pont-Canal du Sart, Belgium

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
11,767
19,301
Nimeona bora ku-share tuone wote.

16174736_1347488625296329_3424983759244856201_n.jpg
 
Sisi tulikunya bustanini na kujitwazia upupu Mkuu ndio maana tupo kama tulivyo
Duh, kwa kweli bado najiuliza kulikoni sisi species ya waafrika. Tuna kila kitu lakini wapi ni shida tu. Juzi nimesoma mahali eti tuna import samaki toka china pamoja na kuzungukwa na maji yenye samaki kibao. I rest my case
 
Unajua inafikia mahali naona Adam na Eva walifanya sawa sawa kula lile tunda la katikati maana si kwa maarifa haya. Ila waafrika sijui tulikula tunda la nje ya bustani!!?
Mtafute Mwalimu Mwakasege akueleweshe tofauti ya akili na maarifa.
 
Duh, kwa kweli bado najiuliza kulikoni sisi species ya waafrika. Tuna kila kitu lakini wapi ni shida tu. Juzi nimesoma mahali eti tuna import samaki toka china pamoja na kuzungukwa na maji yenye samaki kibao. I rest my case
Ni kule Mbeya Mkuu,halafu samaki wenyewe walikuwa feki
 
Sina tatizo na uagizaji wa samaki kwa kuwa pamoja na kuzungukwa na Maziwa Nyasa Tanganyika, Victoria na bahari ya Hindi lakini bei ya samaki ni kubwa sana. Samaki wa dar wanabei kubwa utadhani ndani wana TV. Yaani, pamoja na gharama za kusafirisha kuwa kubwa, bado samaki toka ziwa Victoria ni bei nafuu kuliko wanaovuliwa hapa Hindi. Hii inatokana na kutegemea uvuvi wa mitumbwi ya wakojani/wakwajani. Hakuna anayependa kula samaki aliye na mashaka kutoka China ila unahitajika uwekezaji mkubwa kwenye eneo hili ili kutosheleza soko. Aliyetuloga kafa.
 
Naamini pia hawa waingizaji waliingiza kinyemela. Tfda watakula nao sahani moja. Tra watakula nao sahani moja police watakula nao sahani moja na mahakama nayo itakula nao sahani moja. Ama kweli bongo hawapendagi ujinga.
 
Sina tatizo na uagizaji wa samaki kwa kuwa pamoja na kuzungukwa na Maziwa Nyasa Tanganyika, Victoria na bahari ya Hindi lakini bei ya samaki ni kubwa sana. Samaki wa dar wanabei kubwa utadhani ndani wana TV. Yaani, pamoja na gharama za kusafirisha kuwa kubwa, bado samaki toka ziwa Victoria ni bei nafuu kuliko wanaovuliwa hapa Hindi. Hii inatokana na kutegemea uvuvi wa mitumbwi ya wakojani/wakwajani. Hakuna anayependa kula samaki aliye na mashaka kutoka China ila unahitajika uwekezaji mkubwa kwenye eneo hili ili kutosheleza soko. Aliyetuloga kafa.
Na samaki wa China hasa VIBUA ni rahisi kuliko wa hapa. Na wanapatikana kwa uhakika. Humu tuna shida nyingi sana ni basi tu tumezizoea.

Akija yyt toka nje anashangaa kuitiliza maana fursa njenje ila tuko tunafungana jela na kujenga Chato
 
Back
Top Bottom