Watch TBC Live, TIC na TPSF Wampongeza Magufuli Kwa Hatua Anazochukua, Zitaboresha Zaidi Mazingira ya Uwekezaji Nchini

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,626
Wanabodi,

Naangalia TBC, vipindi maalum kuelekea miaka miwili ya rais Magufuli madarakani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini, TIC. Geofrey Mwambe, na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Gedfrey Simbeye, wamempongeza rais Magufuli kwa hatua mbalimbali anazochukua katika kuelekea kuijenga Tanzania ya viwanda, vita dhidi ya rushwa na ufisadi, na vita vya ulinzi wa rasilimali za taifa, anaboresha zaidi mazingira ya biashara nchini, hivyo Tanzania kuendelea kuwa ni nchi kivutio izaidi kwa wawekezaji.

Mwambe amesema, tangu Magufuli ameingia madarakani, wawekezaji wameongezeka na hukuna hata mwekezaji mmoja aliyekuwepo ameondoka, na kwa hatua hizi anazoendelea kuchukua kulinda rasilimali zetu, wawekezaji serious wataongezeka.

Simbeye amesema kitu cha kwanza rais Magufuli alichofanya baada tuu ya kuingia ikulu ya Magogoni, mkutano wake wa kwanza ni kuzungumza na wafanyabiashara ikulu. Rais amewahakikishia wafanyabiashara wote genuine, mazingira mazuri ya kufanya biashara, na hatua alizochukua kwenye vita dhidi ya rushwa, na ufisadi, hizi hatua anazochukua sasa kulinda rasilimali zetu kwa kubadili sheria na kujadiliana upya na wawekezaji ili Tanzania tufaidike zaidi, kutavutia wawekezaji serious ambao wawekezaji hao watafaidika na Watanzania tutafaidika.

NB. Kuna tatizo nimelinote humu jf kwa baadhi yetu, wanachukia na kukasirika kila rais Magufuli akipongezwa kwa mazuri yoyote. Wao kazi yao ni kupinga tuu kila kitu. Naomba kutoa hoja, kwa vile wanaompongeza rais Magufuli, wanampongeza kwa hoja, hivyo naomba wale wote wanaopinga pongezi hizi kwa rais Magufuli kuhusu uwekezaji, pingeni kwa hoja na sio tuu kupinga kwa chuki!.

Nawaomba sana wana jf, tuwe objective katika kulitendea haki jukwaa hili, kwa kubishana kwa hoja, kwenye mazuri tupongeze kwa hoja na kwenye kukosoa, tukosoe kwa hoja.

Jumapili Njema.

Paskali
 
Paskali, kuna wa uthubutu wa kusema kweli iliyo moyoni mwake? Hao wote ni hypocrites! Angelikuwepo Zitto, Lisu, Kigaila and the like wangesema ukweli toka rohoni mwao bila UNAFIKI na WOGA! (na bila kutukana, dharau , kejeli kwa Rais!).
HAO WANAOGOPA HAWAWEZI SEMA UKWELI WAO
 
Asante kwa taarifa Paskali.
Ukweli ni kuwa hata kwa sasa kuna watu wanaishi peponi na kuna wanaoshi jahanamu ndani ya utawala huu.JPM hawezi kuridhisha kila mtu na mambo hayawezi kwenda wote tutakavyo.All in all wakati anasifiwa kuna watakaokuwa wanakosoa tena kwa ushahidi.Haihitaji hasira!!
 
Hao kila awamu wanapongeza, hàwanaga chuki na rais aliyepo madarakani.
VivaTanzania
 
Mimi huwa siangaliagi TBC, wewe kama unataka kutupa updates tupe kama hutaki acha
 
Haiwezekani wote tukuchukie paskali sababu tumeambiwa na mtu mmoja kwa sababu zake kila mmoja ana uhuru wa kupenda akitakacho,ni haki yao kusifia na akija mwingine ana haki ya kuponda!
 
Propeller mgando (propaganda)
 
Mkuu kwa miongo miwili Tanzania ilikuwa shamba la bibi hakuna uwekezaji wa maana uliowekwa mbali na wawekezaji waliokuwa matapeli kuingia mikataba na viongozi waliokuwa madarakani. Kwa mfano hawa waarabu waliokuwa wamepewa vitalu vya uwindaji Loliondo hakuna uwekezaji wowote walioweka mbali na kuchukua wanyama wetu na kusafirisha kwenda Uarabuni. Sasa hivi taifa litapata wawekezaji waliokuwa serious katika kuwekeza Tanzania. Viongozi waliotangulia walikuwa wakiweka maslahi zao mbele kuliko taifa.
 
Wewe jamaa hukati tamaa kabisa yaani teuzi zote unapigwa kibuti lkn bado umo tu?
 
Nakuunga mkono kwa 100%
 

Badala ya kutangaza vitui vivutio vya uwekezaji kwa wananchi na wageni, wao wanatetea matumbo yao.
 
kwahiyo wewe unakubaki hakuna mwekezaji yeyote aliyeondoka na wamekuja wapya wengi ?

hii wewe unaita ulimi kuteleza na sio uongo ?
 

na wewe unaamini mwarabu ataondoka ?
 
Hivi unategemea hao wateule wa Magufuli watakuja kusema kitu tofauti zaidi ya kumsifia, Kumpamba na kumwabudu?
Wenzao waliotangulia walifanya hivyo hivyo Kipindi cha Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete.

Wanatupotezea muda tu.
 
Mbona sijaona huo ushahidi waliotoa kuthibitisha pongezi zao kwa Ngoswe? Kama walitoa vithibitisho naomba mtu anijuze tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…