Watapeliwa viwanja Kibaha

David Goliath

JF-Expert Member
May 16, 2018
928
1,799
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ametoa siku 14 wasakwe na kukamatwa viongozi 24 wanaotuhumiwa kujihusisha kuwatapeli watu na kuwauzia eneo la shamba la mitamba mali ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Viongozi wanaotafutwa ni pamoja na mabalozi, wenyeviti wa mitaa, watendaji walioshirikiana na madalali waliohusika kuwauzia wananchi viwanja katika eneo la shamba hilo lililopo Halmashauri ya Mji Kibaha.

Kunenge alitoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Pangani uliowahusisha wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha na mkoa kwa ajili ya kutoa msimamo wa serikali kuhusu maamuzi ya eneo hilo ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya makazi.

Alisema orodha na majina ya viongozi hao na madalali waliohusika kuwauzia kinyemela wananchi viwanja katika eneo hilo ambalo linamilikiwa na serikali anayakabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

"Natoa muda wa siku 60 kwa Halmashauri ya Mji Kibaha kupima eneo la shamba hilo namba 34 la mitamba lenye ukubwa wa hekta 4,000 na kubainisha mipaka yote na matumizi yake ili ijulikane kama vile eneo la ujenzi wa ofisi za umma na huduma za kijamii, makazi kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa wananchi walio ndani ya shamba hilo," alisema Kunenge.

Aliwataka makamanda wa polisi na Takukuru Mkoa wa Pwani kuwahoji viongozi na madalali waliohusika kuwauzia wananchi eneo hilo la shamba namba 34 kinyemela na wachukuliwe hatua za kisheria.

Habari Leo
 
Hapo unakuta matapeli ni STD 7, halafu waliotapeliwa ni watu na degree zao
Hili linatokana na watu wenyewe kufanya vitu bila kujiridhisha,Mfano mtu anakwambia anauza viwanja vimepimwa lakini ukimwambia akupe approved survey plan hana,anakuambia bado haijatoka ,sasa unajiuliza huo upimaji wake ana uhakika gan nao? Coz survey plan kibao huwa zinakataliwa kutokana na kukosa vigezo vilivyo ainishwa

Ukiachana na hili watu wananunua ardhi bila kujiridhisha na umiliki wa anayekuuzia
 
Na hapa ndipo tatizo linapoanzia, watu tunafanya mambo kimazoea
 
Juzi hapo ilibakia kidogo nipigwe kama sio kujiongeza.

Jamaa ananiletea ramani ya 2014 kumbe kuna nyingine mpya .

Aisee nilimstahi tu , utapeli umetamalaki kwenye uuzaji wa ardhi, watu wanapigwa sana.

Hizi projects za kuuza viwanja zimekua nyingi bila control ya wizara husika.
 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ametoa siku 14 wasakwe na kukamatwa viongozi 24 wanaotuhumiwa kujihusisha kuwatapeli watu na kuwauzia eneo la shamba la mitamba mali ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Viongozi wanaotafutwa ni pamoja na mabalozi, wenyeviti wa mitaa, watendaji walioshirikiana na madalali waliohusika kuwauzia wananchi viwanja katika eneo la shamba hilo lililopo Halmashauri ya Mji Kibaha.

Kunenge alitoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Pangani uliowahusisha wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha na mkoa kwa ajili ya kutoa msimamo wa serikali kuhusu maamuzi ya eneo hilo ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya makazi.

Alisema orodha na majina ya viongozi hao na madalali waliohusika kuwauzia kinyemela wananchi viwanja katika eneo hilo ambalo linamilikiwa na serikali anayakabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

"Natoa muda wa siku 60 kwa Halmashauri ya Mji Kibaha kupima eneo la shamba hilo namba 34 la mitamba lenye ukubwa wa hekta 4,000 na kubainisha mipaka yote na matumizi yake ili ijulikane kama vile eneo la ujenzi wa ofisi za umma na huduma za kijamii, makazi kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa wananchi walio ndani ya shamba hilo," alisema Kunenge.

Aliwataka makamanda wa polisi na Takukuru Mkoa wa Pwani kuwahoji viongozi na madalali waliohusika kuwauzia wananchi eneo hilo la shamba namba 34 kinyemela na wachukuliwe hatua za kisheria.

Habari Leo
Wenyeviti hamuwalipi mishahara.
Mnataka wafanyekazi 24/7

Matokeo yake ndo hayo
 
Kamata vituo vya redio vinavyowatangaza kwani wao wanawafahamu vizuri ni akina nani na makazi yao. Ukikamata hawa utawapata kirahisi wahusika.
 
Ili mtu anunue ardhi iwe shamba au kiwanja hasa maeneo yaliyo wazi anatakiwa ajiridhishe sana juu ya uhalali wa eneo husika kabla ya kufanya manunuzi.
 
Juzi hapo ilibakia kidogo nipigwe kama sio kujiongeza.

Jamaa ananiletea ramani ya 2014 kumbe kuna nyingine mpya .

Aisee nilimstahi tu , utapeli umetamalaki kwenye uuzaji wa ardhi, watu wanapigwa sana.

Hizi projects za kuuza viwanja zimekua nyingi bila control ya wizara husika.
Sure mamlaka husika ziingilie kati coz ukitapeliwa kiwanja mpaka kuja kupata haki yako ushahangaika sana
 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ametoa siku 14 wasakwe na kukamatwa viongozi 24 wanaotuhumiwa kujihusisha kuwatapeli watu na kuwauzia eneo la shamba la mitamba mali ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Viongozi wanaotafutwa ni pamoja na mabalozi, wenyeviti wa mitaa, watendaji walioshirikiana na madalali waliohusika kuwauzia wananchi viwanja katika eneo la shamba hilo lililopo Halmashauri ya Mji Kibaha.

Kunenge alitoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Pangani uliowahusisha wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha na mkoa kwa ajili ya kutoa msimamo wa serikali kuhusu maamuzi ya eneo hilo ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya makazi.

Alisema orodha na majina ya viongozi hao na madalali waliohusika kuwauzia kinyemela wananchi viwanja katika eneo hilo ambalo linamilikiwa na serikali anayakabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

"Natoa muda wa siku 60 kwa Halmashauri ya Mji Kibaha kupima eneo la shamba hilo namba 34 la mitamba lenye ukubwa wa hekta 4,000 na kubainisha mipaka yote na matumizi yake ili ijulikane kama vile eneo la ujenzi wa ofisi za umma na huduma za kijamii, makazi kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa wananchi walio ndani ya shamba hilo," alisema Kunenge.

Aliwataka makamanda wa polisi na Takukuru Mkoa wa Pwani kuwahoji viongozi na madalali waliohusika kuwauzia wananchi eneo hilo la shamba namba 34 kinyemela na wachukuliwe hatua za kisheria.

Habari Leo
Viongozi wanaotafutwa ni pamoja na mabalozi, wenyeviti wa mitaa, watendaji walioshirikiana na madalali waliohusika kuwauzia wananchi viwanja katika eneo la shamba hilo lililopo Halmashauri ya Mji Kibaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom