Upendo iswa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 375
- 620
TAARIFA YA KERO YA WIZI ENEO LA MACHINJIONI – KATA YA TANGINI, MANISPAA YA KIBAHA
Ndugu viongozi na wananchi wenzetu, tunaomba kuwasilisha kero kubwa ya matukio ya wizi yanayoendelea katika eneo la Machinjioni, Kata ya Tangini, Manispaa ya Kibaha.
Katika kipindi cha hivi karibuni, wezi wamekuwa wakivunja mara kwa mara maduka ya wananchi na kuiba mali zao. Tukio la hivi karibuni limetokea alfajiri ambapo wahusika walivunja kufuli, grill na mlango wa duka, kisha kuiba bidhaa pamoja na mitungi ya gesi na fedha.
Hali hii imeanza kuleta hofu na kuhatarisha usalama wa wananchi pamoja na mali zao. Tunaomba viongozi wa serikali za mitaa, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi kwa ujumla kushirikiana ili kudhibiti hali hii, kuongeza ulinzi na kuwabaini wahusika wa vitendo hivi.
Tunaomba suala hili lichukuliwe kwa uzito ili kuzuia matukio zaidi na kuhakikisha wananchi wanaishi na kufanya biashara zao kwa amani na usalama.
Asanteni kwa ushirikiano wenu.