Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 370,454
- 857,739
Kwenye hili na Mitamba serikali inasehemu kubwa ya lawamaDah! Siku hizi kila mtu anakula lwa urefu wa kamba yake. Ukizubaa tu, umepigwa.
.Eneo liliachwa kuwa pori kwa miaka mingi
.Halmashauri ya Kibaha haikuchukua hatua mapema wavamizi na matapeli walipoanza biashara ya viwanja
. Viongozi na watendaji nao hawakuchukiliwa hatua mapema nao walipojiingiza kwenye hiyo biashara ya kitapeli
. Kwasababu zisizojulikana pori likaachwa bila kufyekwa wala kuhudumiwa na kugeuka pori la maasi, mauaji, vibaka, ujambazi na shughuli za kishirikina
Unamkumbuka yule binti aliyechomwa moto? Alichomewa huko Mitamba...
Bodaboda wengi wameuliwa huko na kuporwa pikipiki zao
Ni kawaida pori la Mitamba kuokota maiti zilizokwisha oza na kuharibika kabisa.. Hapo sijazungumzia makaburi
Baada ya Mabwepande sasa ni Mitamba.. Ukipelekwa huko.. Kutoka salama ni majaliwa ya mbingu
Viwanja vilivyouzwa na kujengwa mijengo ya maana tena kwa nyaraka halali na kupatiwa huduma zote muhimu za kijamii kama umeme na maji ni vingi sana
Serikali ikubali kukosea.. Iwawajibishe waliopiga dili lakini waliokwisha jenga na kufanya maendeleo waachwe tu maana ni wengi mno
Sent using Jamii Forums mobile app