Watanzania wenzangu...

I always wonder,hivi mhando na trupu lake la tanesco wakiamua kugoma na kuzima mitambo mtera itakuwaje? Dawasco nao wakigoma na kuzima mitambo ruvu chini itakuwaje? Na staff wa huduma za anga wakizima mitambo kisa haina quality itakuwaje? Na zima moto waki down tools kisa magari mazee je? For that matter hata wazoa taka darisalama waki down tools je?
This reminds me story ya Anus iliyogoma kupitisha choo eti inadharauliwa matokeo yake ikawa ni head ache na mwili mzima kuwa dysifunctional.
Ndugu zangu hakuna taaluma iliyo bora kuliko nyingine,hata Invisible na taaluma yake ya IT ana mchango mkubwa tu katika jamii.
Nawasilisha,
Bishanga Abashaija.

unajua Bishanga wewe umesema ukweli ambao watu wataukataa tu ila ndivyo ulivyo. Juzi nilikuwa naongea na prof mmoja hapo huo kikuu cha dar es salaam, kiukweli huyu prof alinimbia kitu kimoja kigumu sana juu ya hili sakata la madaktari alisema tatizo ni system yenyewe ya utoaji elimu ndio inayopelekea hapo.

kitendo cha kuwatenga hawa na wanafunzi wengine katika mabweni na lecture rooms ndilo tatizo mtu toka anaanza first yr anaitwa Dr so and so hivyo anafikiri he is somebody very special akasahau kwamba ni mwanafunzi wa kawaida tu. hivi huyu anayesomea udaktari 5 yrs anatofautiana vipi na anayesoma archtech miaka 5? in terms of education duration? na je hiyo miaka 5 inamuongezea ufaulu na uelewa ama bado inambakiza pale alipo kiakili? manake kama makarai wengi tu wana clear kwa makarai lakini sasa inakuja kuleta shida .

hivi wakisema wanalia na kujiona bora je wao ni bora kuliko waalim ambao wamewafundisha? je ni kwanini waifanye field yao kuwa the most expensive field ili hali ita can not survive alone? wanajitetea wao wanawasahau manesi wanaofanya nao kazi tena ambao ndio wanachapa mzigo kuliko wao? ukilazwa hosp utagundua nesi muda mwingine anakuwa ni dr lakin hilo hawalion wanataka tu mifuko yao itune. hebu wareason as prudent and not acting like money mongers.
 
Last edited by a moderator:
kama madaktari wana fight juu ya hali ngumu na mazingira magumu ya kufanyia kazi basi wangeweza kueleweka zaid kama wangewajumuisha na manesi ambao wanafanya nao kazi kwa karibu. tena wangelifanya hivi wangepata mass sapoti kubwa sana ila jinsi ilivyo its like wao hawajui wanataka nini na watawin vip majority ya watu. japo dr anampasua mtu na kumuandikia dawa ila anayesafisha na kufunga vidonda ni nesi anayempa dawa ni nesi yeye anaandika tu sasa huwa najiuliza hivi manesi wakisema hawazitoi hizi dawa kwa wagonjwa hata kama dr kaandika ingekuwaje? mbona kama madaktari wanasahau uhalisia wanabebwa na hisia za kuwa watu bora kuliko wengine?

kibaya zaid ni pale unapokwenda hosp ukataka kuongea na dr juu ya ugonjwa wako omba Mungu usiwe na knowledge ya kile kitu ila kama wengine ambao ni multi professional huwa tunakoma manake ukimwmbia unachokijua jamani anaona kama unaundermine ujuzi wake wakati nafikiri ndio njia nzuri ya kufikia maamuzi juu ya swala lako. to me sipend jinsi wanavyo act.
 
Muhimbili is the crime scene

What of other government hospitals? Hakuna dawa hakuna vifaa, maabara vipimo hakuna. Na kwa sasa hospitali ya mkoa Kilimanjaro hakuna chumba cha upasuaji zaidi ya mwaka, wananchi wanateseka sana, is the government serious? Hakuna maintenance services ya mashine zetu kila ikisema inahitaji maintenance jibu ni pesa hakuna, kiufupi serikali bado haijali afya za wananchi wake, huku hospitali za wilaya hata x ray machine hakuna, madaktari watende miujiza kutibu?
 
Kuna mchezo mchafu hapo hao watu wanauwa makusudi hizo mashine ili wafanye biashara kwenye hospital binafsi
 
Kuwa makini na toa taarifa sahihi ct scan mnh ni lak 1.7 na ni mbovu mda mrefu , mashine moja inahudumia nchi nzima haifanyiwi service itadumu vipi???

Mkuu sikusoma vizuri ebu fafanua.
 
kama madaktari wana fight juu ya hali ngumu na mazingira magumu ya kufanyia kazi basi wangeweza kueleweka zaid kama wangewajumuisha na manesi ambao wanafanya nao kazi kwa karibu. tena wangelifanya hivi wangepata mass sapoti kubwa sana ila jinsi ilivyo its like wao hawajui wanataka nini na watawin vip majority ya watu. japo dr anampasua mtu na kumuandikia dawa ila anayesafisha na kufunga vidonda ni nesi anayempa dawa ni nesi yeye anaandika tu sasa huwa najiuliza hivi manesi wakisema hawazitoi hizi dawa kwa wagonjwa hata kama dr kaandika ingekuwaje? mbona kama madaktari wanasahau uhalisia wanabebwa na hisia za kuwa watu bora kuliko wengine?

kibaya zaid ni pale unapokwenda hosp ukataka kuongea na dr juu ya ugonjwa wako omba Mungu usiwe na knowledge ya kile kitu ila kama wengine ambao ni multi professional huwa tunakoma manake ukimwmbia unachokijua jamani anaona kama unaundermine ujuzi wake wakati nafikiri ndio njia nzuri ya kufikia maamuzi juu ya swala lako. to me sipend jinsi wanavyo act.

kila profession ina chama chake cha kitaaluma na kuhitaji kutetea mahitaji na mapenndekzo ya taaluma hiyo..mfano Madaktari, Wafamasia, Wauguzi, Watu wa maabara n.k.

-si kila madai huusisha taaluma zote wakati wote
- kuna dai katika madai pendekezwa inayojumuisha taaluma zote

kuhusu kuwa na uelewa..ni vizuri, mara nyingi nafurahi napokutana na wagonjwa wenye uelewa na kusoma angalau ugonjwa kupitia na aina za matibabu. Kwa mfn nilikutana na mgonjwa wa saratani ya ngozi(Malignant melanoma) iliyokuwa katika mguu mmoja, tuliposhauriana kufanya vipimo kuhusu kuona ni jinsi gani imesambaa mwilini(kwa kutumia Ct- scan, Ultrasound sonography, na X-ray) kwa mgonjwa huyu ilikuwa ni shida madai yake ni kuwa tatizo liko ktk mguu, kwa nini tusikate mguu na kuhangaika na mengine..lakini kwa kulazimisha ilibidi nilazimishe vipimo! saratani ya ngozi kwa mfano haikuchukui hata miaka miwili) sasa kama kwa mfano ningelazimisha kufata tu maelezo ya mgonjwa aliyoyasoma ktk mtandao(ambao kila mtu anaweza kuandika kwa maoni yake) mgonjwa huyu alikuwa anapotea.
Ushauri wangu ni vema kusoma katika mitandao ya kidaktari au ule wa Shirika la afya duniani(WHO) kuona ni njia gani za vipimo,matibabu mgonjwa anaweza kupata, lakini zaidi ya yote kujua ni njia zipi zilizo hapa nchini.
 
Wakati mwingine unashangaa kwa kweli kwa nini huko Hindu Mandal, Aga Khan, Regency, TMJ, vifaa vipo salama muda wote...

Habari kutoka hospitali ya Ocean Road, serikali kwa kutumia fedha nyingi za umma ilinunua kompyuta tatu maalumu kwa ajili ya kupimia magonjwa ya saratani, lakini kompyuta moja kati ya hizo imetoweka hospitalini hapo imeibiwa.

Kuna mashine ingine ya magonjwa ya saratani imeibiwa ambayo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wake.
 
kila profession ina chama chake cha kitaaluma na kuhitaji kutetea mahitaji na mapenndekzo ya taaluma hiyo..mfano Madaktari, Wafamasia, Wauguzi, Watu wa maabara n.k.

-si kila madai huusisha taaluma zote wakati wote
- kuna dai katika madai pendekezwa inayojumuisha taaluma zote

kuhusu kuwa na uelewa..ni vizuri, mara nyingi nafurahi napokutana na wagonjwa wenye uelewa na kusoma angalau ugonjwa kupitia na aina za matibabu. Kwa mfn nilikutana na mgonjwa wa saratani ya ngozi(Malignant melanoma) iliyokuwa katika mguu mmoja, tuliposhauriana kufanya vipimo kuhusu kuona ni jinsi gani imesambaa mwilini(kwa kutumia Ct- scan, Ultrasound sonography, na X-ray) kwa mgonjwa huyu ilikuwa ni shida madai yake ni kuwa tatizo liko ktk mguu, kwa nini tusikate mguu na kuhangaika na mengine..lakini kwa kulazimisha ilibidi nilazimishe vipimo! saratani ya ngozi kwa mfano haikuchukui hata miaka miwili) sasa kama kwa mfano ningelazimisha kufata tu maelezo ya mgonjwa aliyoyasoma ktk mtandao(ambao kila mtu anaweza kuandika kwa maoni yake) mgonjwa huyu alikuwa anapotea.
Ushauri wangu ni vema kusoma katika mitandao ya kidaktari au ule wa Shirika la afya duniani(WHO) kuona ni njia gani za vipimo,matibabu mgonjwa anaweza kupata, lakini zaidi ya yote kujua ni njia zipi zilizo hapa nchini.

sasa ndugu yanu Dr umenijibu vyema sana, ila huoni kwamba kama kweli nia yenu ilikuwa ni kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwanini msingejumisha watumish wote wa mahspitalini? hili lingewezekana kabisa na nina uhakika nalo kabisa.

juu ya mgonjwa kuwa na ujuzi wa anaumwa nini hili kwa hapa kwetu Tz ni tatizo manake wengi wetu hatupendi kusoma. wachache sana waliobahatika kupenda kusoma. wengi wa wanaoelewa matatizo ya magonja hadi wakawa na confidence ya kuongea na dr ni wale ambao ama waliwah kupitia elimu ya biolojia kwa undani zaid najua layman hawez wala hana hiyo confo. ishu inakuja pale ambapo kwa mfano mimi ni mtaalam wa physiology and anatomy ingawa siyo medical practitioner unakwenda hosp unamgonjwa ana osteomilitis dr ambayo ni recurrent anakwambia piga x-ray unapiga inaonyesha tu kuna non union fructure unamwambia kwakua hii tayari ni re occured kwanini tusifikiri kufanya MRI ili kuona extent ya infection anakwambia hapana aende tu theater huko tutapata jibu la extent ya infection. wewe unabaki na maswali je kwa jins ilivyona huu mfupa ukiwa umeharibika kabisa atakuja kutusainisha tena consent form ili aukate ama? pili inabidi kama akiingia theatre awe mgonjwa pekee ili pawe sterilized ku avoid contaminat kwa wagonjwa wengine sasa je pakitokea complication ambayo ni kubwa pasi kutuandaa itakuwaje?

kwakweli hapa nilifika mahali uvumilivu ulinishinda na nashukuru senior wao alisema hapana afanyiwe mri ili tujue tunafanya nini manake mtu mzima ni tofauti na mtoto. sasa miye naongelea mazingira kama hayo.
 
Sina tabia ya kufungua nyuzi jukwaa la siasa (JLS), anga zangu ni mmu na chi chat.
Lakini katika hili la hospitali ya muhimbili kwa kuwa naijua vyema naomba niseme haya yafuatayo:
1.MRI ( magetic resonance imaging):
Mashine hii muhimbili ipo,gharama za kipimo ni sh 120,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 540,000.- kwa kipimo.
2.CT scanning:
Muhimbili tsh 80,000.-
Ukienda agha khan,regency na hindu mandal unapigwa sh 360,000.-
3. Kidney dialysis:
Hiyo ndo usiseme.
In short,vipimo hivi day in day out ukienda muhimbili unaambiwa vimekufa, nenda agha khan,hindu mandal na regency,same doctors hao hao wa muhimbili wana handle vifaa hivi private hospitals na kutoa majibu kwa gharama kubwa,mnyonge inabidi augulie tu cant afford.
Kila kukicha technians from Phillips company Uholanzi wanakuja TZ kurekekibisha mashine hizi muhimbili na zinakuwa ok,wakitoka tu zinakufilia mbali, patients wanaendelea wenda private hospitals,doctors wanalalamika vifaa duni.
Tutafika kweli?????

We vipi unashangaa hayo! Mbona hushangai Komba wa ToT kwenda kupima afya India?
 
mkuu manshiroo, ahsante kwa umakini na uchambuzi mzuri..Nakubaliana na wewe kuwa hayo yanatokea, lakini wakati mwingine sababu kama hizi zinaweza kusababisha;

Uchumi:- mgonjwa kushindwa kumudu gharama ya matibabu kwa vipimo vingine mf USS,CT scan au MRI.

Uzoefu:-kwa kutumia uzoefu wa wagonjwa tuyaonayo hospitalini na kupitia takwimu mbalimbali za magonjwa.

Matarajio:-inawezekana kuwa kwa kutumia hata vifaa bora bado hali ya mgonjwa haitakuwa bora kutokana na usambaaji wa ugonjwa mwilini.

lakini wakati mwingine huja kutokana na uzoefu binafsi(personal competency).
 
chit chat na mmu oyeeee

huku sitii neno maana walishaninyoa sasa naoopa kunyolewa ngozi.

Kuna kipimo cha figo pale ocean road kimekufa, mgonjwa anaambiwa aende Bugando, nauli, mahali ya kuishi, gharama ya kipimo chenyewe, wanyonge bora turudi kwenye maombi tu.
 
Nini tena shemeji Bishanga ??? ....nani kakufanya nini nikamchape?

Yangu macho kwenye huu uzi lolest.....ila umejilipua hadi raha.....bado Erickb52 na Asprin nawasubiri na wao niwaone siku moja waje wajilipue jukwaa la siasa lol......shemu leo vinywaji juu yangu!

Kwangu mimi Siasa ni mchezo wa kuigiza. Twenzetu turudi nyumbani. Yani Bishanga leo yuko huku?

_DSC0014.JPG
 
Last edited by a moderator:
Kuna ufisadi sana kwenye hospitali zetu za serikali. Na hayo hayo mafisadi papa sasa yanadai mamishahara makubwa eti wenzao bungeni wanalipwa vizuri.
 
Wasi wasi wangu ni nini hasa kinasababisha mashine za dialysis,ct scanner na MRI kila kukicha muhimbili zimekufa , opearators kwa maana ya technicians , wasoma majibu kwa maana ya doctors ambao wanasimamia mashine hizi za muhimbili ndo more or less unawakuta hao hao regency,agha khan na hindu mandal wanapiga mzigo?
Mkuu unataka tutajane kwa majina hapa? Twajuana ati.

Kiongozi,

Unataka kueleza nini umma wa Wa-Tanzania?

Hivi vifaa ulivyovitaja nani mwendeshaji wake? Ma-daktari?

Ni jinsi gani Daktari anaweza kuhujumu hivi vifaa?

Anyway - Kwa kuwa Watanzania tunaishi kwa mazoea ndiyo maana unaweza kuona suala hili linachukuliwa ki-MAZOEA - shame..!

Kwakuwa DAWASCO, TANESCO, E.t.c wana vifaa duni, basi tukubali kuendelea kutokuwa na vifaa kwenye Ma-Hospitali?

"Ni dhambi kubwa kuruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa..."
 
chit chat na mmu oyeeee

huku sitii neno maana walishaninyoa sasa naoopa kunyolewa ngozi.

Kuna kipimo cha figo pale ocean road kimekufa, mgonjwa anaambiwa aende Bugando, nauli, mahali ya kuishi, gharama ya kipimo chenyewe, wanyonge bora turudi kwenye maombi tu.

Kile kipimo Kongosho, kinaitwa bone scanner, ni kwa ajili ya kuweza kugundua saratani imesambaa kiasi gani kwenye mifupa
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli hakuna taaluma ya maana zaidi ya nyingine. Ni imani yangu Drs wamefikisha ujumbe kwa watawala kwa niaba ya taaluma nyingine. Watz hebu tuamke, hivi mnajua kuwa mgodi wa geita peke yake unaweza kuexempt PAYE za wafanyakazi kwa miaka kama mitano bila kuathiri bajeti kama ukisimamiwa vizuri. Hebu tuacheni jamani msitutie hasira bure...
 
Back
Top Bottom