Katika uzi niliowasilisha awali nilizungumzia kuhusu athari ya ilani ya CHADEMA kwa ndoa na ajira; katika uzi wangu wa pili nilizungumzia kasoro za kiuchumi katika ilani za CHADEMA na ACT-Wazalendo. Katika uzi wangu huu wa tatu, nitazungumzia ulaghai kuhusu utekelezaji wa sera ya bima ya afya kwa wote.
Kwanza unapozungumzia bima yeyote ile maana yake kuna malipo ya mwanzo (premium) ambayo mnufaika aidha analipa yeye mwenyewe au analipiwa sehemu na yeye mwenyewe analipa sehemu ya hiyo premium au analipiwa yote hiyo premium. Kwa suala la bima ya afya ambayo CHADEMA wanajinasibu sana kuwa watawapa watanzania na itakuwa ni nafuu sana kuliko ile inayotozwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, CHADEMA wanapotosha sana.
Siku zote kipato binafsi ch mtu ndicho msingi wa wapi mtu huyo atatibiwa, wapi ataishi, wapi watoto wake watasoma. Hata siku moja hakutakuwa usawa wa kila mtu kutibiwa Aga Khan hospital, Hindu mandal hosptital au hospitali ya wilaya ya serikali.
CHADEMA wanakwepa kutaja kuwa chini ya utawala wao mtanzania atalipa premium shilingi ngapi ili aweze kuwa na bima, na pia bima hiyo itamuwezesha kutibiwa hospitali zipi. Je serikali itachangia shilingi ngapi kwa kila bima ya mtu mmoja ili kumuwezesha kutibiwa hospitali zipi. Ni wazi wanaweza wakampa kila mtu bima lakini bima hiyo isimruhusu mtu huyo kutibiwa hospitali yenye hadhi kama Aga Khan au Hindu Mandal.
CHADEMA kwa kulijua hilo ndio maana katika ilani yao wamesema kuwa watakuwa na bima maalum kwa askari wa majeshi yetu. Hii maana yake ni kuwa bima hiyo ya maaskari itakuwa tofauti na ile ya watanzania wengine wasio maaskari na kwa kwa lugha nyepesi itakuwa na package ambazo hazipo katika bima ya kawaida za watanzania wengine. Kama bima za watanzania wengine zitawawezesha kupata kila aina ya matibabu katika hospitali yeyote kwa nini kuwe na bima maalum ya maaskari? {Angalia ilani ya CHADEMA (d) Ukurasa 93}
Pia hoja nyingine ni suala la uwezo wa kiuchumi la kuwalipia sehemu kubwa ya gharama za bima hiyo watanzania wote. Ieleweke kuwa sekta ya afya ina gharama na ili kuwa na huduma bora za afya kwanza serikali lazima iwe na mapato makubwa sana ili iweze kutenga bajeti kubwa kwa ajili ya sekta ya afya.
Bajeti hiyo ndiyo inayotumika kugharamia mafunzo ya madaktari, wauguzi na wataalam wengine wa afya, kujenga majengo ya kutolea huduma za afya, kununulia mashine za kitabibu, vifaa tiba, vitendanishi, madawa na piakutunza miundombinu ya mataibabu pa,oja na mishahara ya watumishi. Lissu anatolea mfano wa gharama ndogo za bima za Ubelgiji lakini haangalii tofauti kubwa ya pato kati ya nchi ya Ubelgiji na Tanzania.
Katika uzi wangu wenye kichwa cha habari “Kasoro za kiuchumi katika ilani za CHADEMA na ACT Wazalendo” nimehoji kuwa waeleze matarajio (projection) ya ukuaji wa uchumi kila mwaka kwa miaka yote mitano, GDP ya kila mwaka kwa figures ili iweze kujulikana kwa uhakika chini ya sera zao pato la nchi litakuwaje. Pato la nchi ndio msingi wa mapato ambayo serikali itakuwa inakusanya kwa njia ya kodi na yasiyo ya kodi. Pia waeleze makusanyo yao ya kodi yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka na pia mapato ya ndani ya serikali kwa ujumla yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka. Wataje pia kwa figures (projections) watakuwa wanakusanya shilingi ngapi kila mwaka
Pia niliwataka CHADEMA na ACT Wazalendo watueleze (projections) watatumia shilingi ngapi kati ya makusanyo hayo ya kila mwaka kulipa mishahara hiyo mikubwa wanayoahidi na pia kulipa madeni ambayo watapaswa kuendelea kulipa. Baada ya hapo tutaweza kujua kiasi cha mapato kinachobakia kwa ajili ya kutekeleza hayo mambo makubwa wanayoahidi na watukukotolee matumizi yote kuanzia afya, elimu bure, mikopo ya elimu ya juu, maji, nyumba, viwanda, masoko nk ambavyo hasa CHADEMA wamekuwa wakidai watafanya.
Kwa kulinganisha Ubelgiji yenye watu milioni 11 GDP yake ni Dola za Marekani Bilioni 529.61 mwaka 2019 wakati Tanzania yenye watu milioni 56, GDP yake ilikuwa shilingi trilioni 139.9 takribani Dola za Marekani Bilioni 60 kwa kipindi hicho. Matumizi ya serikali ya Ubelgiji katika sekta ya afya yalikuwa asilimia 10 ya GDP yake (Dola za Marekani Bilioni 53). Tanzania hata wakitumia asilimia kumi kama Ubelgiji bado matumizi yatakuwa kidogo kwa sababu ya GDP ndogo na idadi kubwa ya watu.
Hivyo CHADEMA wanavyoaminisha watu kwamba watatoa huduma bora za afya wanapaswa watueleze kwanza bajeti yao ya sekta ya afya itakuwa shilingi ngapi na watapata wapi pesa hiyo. Uwepo wa bima sio muarobaini wa kuwa na huduma bora za afya kwa sababu katika nchi yeyote kuna gharama ambazo zinabebwa na serikali moja kwa moja ndio maana huko Ubelgiji gharama za bima anayolipia mtu mmoja ni ndogo lakini hiyo haina maana kuwa ndio gharama halisi ya matibabu pimdi huyo mtu akiugua au kwa kuwa wengine hawataugua basi ndio kusema kuwa hiyp hela yote ya bima iliyokusanywa itatosha kugharamia wote watakaougua, la hasha.
Lissu na CHADEMA wanapswa wajielimishe kuhusu masuala ya uchumi badala ya kuchukulia kuwa kila kitu kinawezekana kufanyika na kama hakikufanywa na serikali iliyopo madarakani basi ni kwa sababu haikutaka. Uchumi hauendi hivyo.