Watanzania Wanatazama Mbele kwa Matumaini kuliko wakati Mwingine wowote

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Hatimaye kauli ya kijasiri kutoka kwa kiongozi Jasiri na mwenye maono mh Rais Dr Mama Samia Suluhu Hassan imeshika mizizi na kumea katika mioyo ya watanzania,kauli hii ilitamkwa kwa ujasiri mkubwa Sana na mh Rais wetu Jasiri muongoza njia Mara baada ya kuondokewa na Rais wetu wa awamu ya Tano Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli Akiwa madarakani.

Kwa Sasa kila mtu, kila Mtanzania, kila mwananchi na kila mzalendo wa Taifa letu anatazama mbele kwa matumaini na siyo hofu, kila mtanzania anaona Nuru mbele yake, kila mwananchi anaiona njia katika maisha yake na uchumi wake, kila mmoja wetu Anayo matumaini ya kutimiza Ndoto zake, kila anayefanya kazi kwa juhudi, maarifa, kujituma, kujitoa na kujitolea anaona akifikia malengo yake.

Iwe Ni wakulima, wafanyabiashara, wajasiriamali,wavuvi,wanasiasa,wazee, vijana,akina mama na watu wenye ulemavu Wanatazama Mbele kwa Matumaini makubwa sana. Juhudi,mipango, mikakati, sera, ajenda, maono, vipaombele na kazi za Mh Rais zimefanya kila kundi na kila Rika kuona mwanga wa mafanikio ukiangaza mbele yake, serikali ya Rais Samia imeleta matumaini makubwa Sana kwa watanzania kuliko wakati Mwingine wowote ule.ni matumaini kila sehemu, ni faraja kila mahali, ni hatua kwenda mbele kila mahali,hakuna tulipo Rudi nyuma Kama Taifa Bali tumesonga mbele kila mahali Kama Taifa.

Ndio sababu serikali ya Rais Samia inapongezwa na kila mtu,ndio sababu uchumi wetu unaendelea kufanya vizuri kwa kuwa kila mmoja wetu anawajibika katika eneo lake katika ujenzi wa Taifa letu,Ndio sababu Taasisi za kimataifa zinamimina sifa kwa Tanzania kutokana na kufanya vizuri katika kila eneo,ndio sababu Tanzania imechomoza Kama chaguo namba moja la wawekezaji, wafanyabiashara wakubwa na watalii kutoka Mataifa mbalimbali.

Kwa hakika Mwenyezi MUNGU yupo pamoja na Taifa letu, yupo pamoja na Rais wetu, Yupo pamoja na watanzania,Ndio maana Rais wetu kapewa njia na maarifa ya kuliongoza Taifa letu, ndio maana anaongoza Taifa kwa hofu ya Mwenyezi MUNGU, ndio maana kila kitu kinafanikiwa, ndio maana Mwenyezi MUNGU anatuepusha na kutukinga na majanga, ndio maana Mwenyezi MUNGU anaendelea kulibalika Taifa letu katika kila nyanja kwa kuwa linaoongozwa kwa mkono wa haki wa Rais samia,Ndio maana ya kutamalaki kwa amani, utulivu na upendo mkubwa miongoni mwa Watanzania.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Nakiri, sijasoma maudhui ya mada. Mada Imetosha kusema yafuatayo.

Ukiniuliza mimi, sioni tofauti yeyote ya manung'uniko na maneno yanayojirudia rudia ya kuanzia kati ya 2008 na 2014! Nipo tayari kusahihishwa, ila.
Ninachokitambua, "Matumaini" huwa hayapimwi nje ndani. Roho za Mtanzania haziwezi kuwa zinachezewa na sarakasi za kumpendezesha na kumfurahisha Alwatan.

Nikiri pia,Nina bubujikwa kusema haya. Tarehe hii ya Leo.

Amani itutawale Watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika na Viongozi wake.
 
Nakiri, sijasoma maudhui ya mada. Mada Imetosha kusema yafuatayo.

Ukiniuliza mimi, sioni tofauti yeyote ya manung'uniko na maneno yanayojirudia rudia ya kuanzia kati ya 2008 na 2014! Nipo tayari kusahihishwa, ila.
Ninachokitambua, "Matumaini" huwa hayapimwi nje ndani. Roho za Mtanzania haziwezi kuwa zinachezewa na sarakasi za kumpendezesha na kumfurahisha Alwatan.

Nikiri pia,Nina bubujikwa kusema haya. Tarehe hii ya Leo.

Amani itutawale Watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika na Viongozi wake.
Rudia kusoma ulichoandika
 
Kuna "Manung'uniko" mengi sana.
Kuna Njaa sana leo hii -sawa na Kipindi cha J.M. Kikwete

Rudia kusoma nilichoandika.
 
Kuna "Manung'uniko" mengi sana.
Kuna Njaa sana leo hii -sawa na Kipindi cha J.M. Kikwete

Rudia kusoma nilichoandika.
Mimi Naye ishi mitaani naona namna watanzania walivyo na matumaini katika mioyo Yao, Wana Imani kubwa Sana na uongozi wa Rais Samia kutokana na usikivu wake pamoja na kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mbele yetu Kama Taifa. Wananchi wanaona Nuri mbele Yao, wakulima wanaona Neema usoni Pao,njaa walishaifukuza umbali mrefu kutokana na kulima kwa nguvu hasa baada ya kuwezeshwa na serikali yao kwa kupewa mbolea za Ruzuku.
 
Mimi Naye ishi mitaani naona namna watanzania walivyo na matumaini katika mioyo Yao,
You meant the Streets. As in British Streets?. Well, in swahili there is a different intralingual definition....You know why I say this...well, its because Mitaani hakuna mashamba ya kulima...Njaa also, is intralingual.;-Kuna njaa mtaani ndugu na hakuna shamba au ruzuku inayoweza kuondoa "Njaa" hiyo.

Tunapishana Lugha.

Na itoshe kusema, sikuwa nasema na wala sikumaanisha kuwa sina Imani na Raisi Samia. Nilichokisema ni kuwa kuna "manung'uniko" kana yale ya miaka ya 2008-2014....haina maana sikuwa na imani na Raisi wakati huo pia.



Wana Imani kubwa Sana na uongozi wa Rais Samia kutokana na usikivu wake pamoja na kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mbele yetu Kama Taifa. Wananchi wanaona Nuri mbele Yao,wakulima wanaona Neema usoni Pao

,njaa walishaifukuza umbali mrefu kutokana na kulima kwa nguvu hasa baada ya kuwezeshwa na serikali yao kwa kupewa mbolea za Ruzuku
CCM Oyeee
 
Back
Top Bottom