Watanzania wanamjua Dr. Munga?

Watanzania wanamjua Dr. Munga?

Dr. Munga is the man of God... viongozi wengine wameufyata kazi yao kukusanya sadaka tu.

Wakati wa utawala wa Kikwete Baraza la Maaskofu TEC ilikuwa mstari wa mbele kupiga kelele dhidi ya dhulma na haki.

Leo wako wapi akina Tarcisius Ngalalekumtwa Rais wa TEC? Wako wapi akina Askofu Method Kilaini, Rwaichi, Lebulu na wengineo?

Au wakatoliki wamekaa kimya kwakuwa Mkatoliki yupo ikulu?

Viongozi wa dini kemeeni uovu acheni ubaguzi
Wamemwachia Niwemugizi pekee yake. Wengine wamebaki watazamaji
 
Huyu mzee si ndiye alipata ajali wakati fulani akitokea Dar kwenda Tanga ?
 
Samahani niulize; katika kampeni za uchaguzi 2015 Lowasa alisali kanisa analosalisha ambapo Mhe. Lowasa alitamka kuwa sasa ni zamu ya KKT kumpata rais? Please anayejua anijulishe. Kama ni ndio ama la?
 
Wachache tunaomkubali mtu huyu wa Mungu,yeye na Askofu Severin aliyepewa kesi cha uraia na madikteta uchwara,nawakubali
 
Hivi na watanzania wanamjua mjomba wangu Abdallah Sabuni? Huyo mjomba wangu hajui kupindisha maneno, yeye ni ukweli tu. Lakini yeye amesomea chuo kimoja huko Ontario Canada. Watanzania naomba mumfahamu.
 
Picha za chuo kikuu cha SEKOMU zikionesha mazingira mazuri kama huko Uholanzi na Uswizi please.

Though, Hongera zake
 
Dr. Munga is the man of God... viongozi wengine wameufyata kazi yao kukusanya sadaka tu.

Wakati wa utawala wa Kikwete Baraza la Maaskofu TEC ilikuwa mstari wa mbele kupiga kelele dhidi ya dhulma na haki.

Leo wako wapi akina Tarcisius Ngalalekumtwa Rais wa TEC? Wako wapi akina Askofu Method Kilaini, Rwaichi, Lebulu na wengineo?

Au wakatoliki wamekaa kimya kwakuwa Mkatoliki yupo ikulu?

Viongozi wa dini kemeeni uovu acheni ubaguzi
TEC wehu tu..
 
Samahani niulize; katika kampeni za uchaguzi 2015 Lowasa alisali kanisa analosalisha ambapo Mhe. Lowasa alitamka kuwa sasa ni zamu ya KKT kumpata rais? Please anayejua anijulishe. Kama ni ndio ama la?
Tabora na Lushoto wapi na wapi

Lowasa alitamka maneno hayo akiwa Tabora
 
DR MUNGA SIMJUI. JINA LAKE LIMENIKUMBUSHA MAREHEMU MWANAFALSAFA MUNGA TEHENAN MTANZANIA. NI MTANZANIA ALIYEWAPENDA WATANZANIA WENZAKE NA KUANDIKA SANA KUWASAIDIA KUJITAMBUA. ALISIMAMIA GAZETI LA JITAMBUE AMBALO HALITOKI BAADA YA KIFO CHAKE. HAKIKA WE NEED TO CELEBRATE MUNGA TEHENAN.
Marehemu Munga alikuwa vizuri sana

Angekuwa hai mpaka sasa, tungefaidi sana elimu yake ya jitambue
 
Humjui vizuri huyo mchawi wa kutoka kijiji cha Tewe, aliyevuruga kanisa nakugeuza miradi ya kanisa kama mali binafsi ya familia, inshort humjui Dr. Munga vizuri, askofu aliyenajisi kanisa kwa ubinafsi na uchawi. Zuri unaloliona kwake ni hilo la kukemea serikali lakini anakokuongoza yeye aibu tupu.
 
Sasa ndugu yangu Zumbe wewe kanisa na msikiti wapi na wapi?

Acha hizo
 
WATANZANIA MNAMJUA Dr STEPHEN MUNGA?

Sijui kama watanzania wanamjua huyu Dr Stephen Munga vizuri,sina uhakika na swali langu lakini yapo mambo kadhaa ambayo nayajua kuhusiana na watanzania kwa Dr Huyu.

Kwanza najua wapo ambao wamewahi kulisikia hili jina.

Pili najua wapo ambao wanamfahamu kwa kumuona .

Tatu najua wapo ambao wanamfahamu kwa kazi na cheo chake

Nne najua kuna ambao hawajawahi kulisikia hili jina na wala hawamfahamu kwa lolote, hii ni kawaida tu!

Lakini pia wapo ambao wamemjua na wanamjua kwa huduma yake .

Vile vile naelewa kuwa watu wengi wanamjua Dr Munga kwa namna tofauti tofauti lakini hofu yangu iliyonifanya mpaka nikaamua kukaa na kuandika haya ni ile kutokujua kuwa Je?

Watanzania wanamjua huyu mtu vizuri?

Wanamfwatilia?

Wanamtumia?

Wanafikiwa na ujumbe wake?

Wanaijua thamani yake?

Ki ufupi mimi nilianza kumfahamu Dr Munga miaka ya 2004/2005 wakati huo akiwa kwenye harakati za kuhakikisha Chuo Kikuu cha SEKOMU kinajengwa. Nakumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuhangaika huku na kule kutafuta wafadhili, kushawishi watu na kuhamasisha kuwa kwa hali yeyote Chuo kikuu kijengwe. Hapo ndipo nilimjua huyu mtu akiwa anashirikiana na mkewe Dr Aneth Munga.

Tangu hapo nilianza kumfwatilia Dr STEPHEN MUNGA mpaka leo namfwatilia sana.

Kwanza kabisa huyu jamaa ni msomi mzuri tu. Ana PhD (Doctor of Philosophy) katika maswala ya Theolojia na kama sikosei kuna Politics kidogo humo. Alisoma LUND UNIVERSITY nadhani ni Ujerumani. Kwa hiyo huyu jamaa ni msomi kwelikweli.

Pili huyu jamaa ndie Askofu wa moja ya Dayosisi kubwa kabisa Tanzania ambayo ni Dayosisi ya Kaskazini mashariki huyu ni Askofu wa hiyo Dayosisi katika kanisa la KKKT.

Tatu Huyu Dr Stephen Munga ni Chancellor wa SEKOMU (SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY), Hiki ni chuo kikubwa sana katika vyuo vikuu binafsi hapa Tanzania, ni chuo ambacho kiko kule Lushoto eneo la Magamba.
Ni moja ya Vyuo vikuu pekee vyenye mandhari kama ya Nchi za Uholannzi au Uswizi kulingana na mazingira yake ya ubaridi na ukijani uliotawala uoto wa eneo lenyewe. Ni chuo kizuri sana.

Lakini zaidi ya hayo DR Stephen Munga amejipambanua kuwa askofu tofauti na maaskofu wengine kwa kuwa Mkweli, huyu jamaa ni mkweli na ndio maana hata kama siku nasikia uvivu wa kuhudhuria ibada nikisikia Askofu Munga yupo lazima niende kwasababu lazima nitapata vitu adimu kutoka kwake. Nampenda sana.

Huyu jamaa anafwata nyayo za mitume wa zamani, anafwata nyayo za Yesu kristo.

Nasema hivyo kwasababu baadhi ya Viongozi wa dini wa siku hizi ni waoga, hawasemi ukweli wakati mwingine kwa kuogopa mamlaka lakini Dr Munga ni tofauti yeye anasema ukweli.

Mussa alipokuwa anawapeleka watu wa Mungu Canaan walipopata kiu alihangaika kuwapa Maji, walipopata njaa alihangaika kuwapa Chakula, walipoumwa alihangaika kuwatafutia dawa mfano walipoumwa na nyoka jangwani japo lengo la safari ilikuwa sio kula,kunywa wala huduma kama hizo.

Yesu Kristo alipohubiri kwa masaa mengi na kuona watu wana njaa aliagiza iletwe mikate na samaki wachache akavibariki na maelfu kwa maelfu wakala na kushiba japo lengo la mahubiri yake ni kuuendea ufalme.

Viongozi wengine wa dini wanafikiri kuwa wajibu wao ni kuhubiri habari za kwendaa mbinguni pekee, kufungisha ndoa, kuzika waumini wakifariki, kukusanya sadaka…sio kweli. Ingekuwa ni hivi hata Yesu asingekufa, asingeuawa na watawala wa Roma.

Viongozi wa Dini wanatakiwa wawe mstari wa Mbele kukosoa watawala, kuwaelekeza waumini wao ninini wafanye katika ufasaha na hapo wawahubirie habari za kumuona Mungu, wasipofanya hivyo watawahudumu waumini wachovu, waliovunjika mioyo, wajinga, wenye njaa, wenye mateso, wanyonge na wasiojitambua…wakati huo huo mbinguni hakitaingia kilicho kinyonge.

Asante sana DR STEPHEN MUNGA kwakuwa wewe umekuwa tofauti…

Hivi MEDIA zinakuona?
WATANZANIA wanakujua?

JE WATAWALA?

IBADA NJEMA WAKRISTO WOTE,

WASIO NA DINI SIKU NJEMA

WAISLAM WOTE NA WENYE DINI NYINGINE TUOMBEANE!
96d5de7ca84396f8a73e6b28af836c3e.jpg
8d42a1b4aed163009c6adb1f031dac2e.jpg
7fad61911bdc6fb7b7290971b9444714.jpg
Ujumbe mzuri, lkn LUND university ni Sweden.
Asante.
 
Humjui vizuri huyo mchawi wa kutoka kijiji cha Tewe, aliyevuruga kanisa nakugeuza miradi ya kanisa kama mali binafsi ya familia, inshort humjui Dr. Munga vizuri, askofu aliyenajisi kanisa kwa ubinafsi na uchawi. Zuri unaloliona kwake ni hilo la kukemea serikali lakini anakokuongoza yeye aibu tupu.
Nilikua natafuta hoja kinzani, hebu jitahidi kidogo kunyoosha maelezo labda tutakuelewa.

Toa ushahidi juu ya uchawi wake
Toa ushahd wa miradi binafsi

Mtoa hoja ameeleza mazuri yake

Ujenzi wa SEKOMU
Ujasiri wa kuikosoa serikali
 
Samahani niulize; katika kampeni za uchaguzi 2015 Lowasa alisali kanisa analosalisha ambapo Mhe. Lowasa alitamka kuwa sasa ni zamu ya KKT kumpata rais? Please anayejua anijulishe. Kama ni ndio ama la?
Dr Munga yuko dayosisi ya Kaskazini Mashariki yenye makao makuu yake katika mji uliojaa ustaarabu na mandali nzuri uitwao Lushoto.
Kwa hiyo usichanganye mambo mkuu
 
Dr. Munga is the man of God... viongozi wengine wameufyata kazi yao kukusanya sadaka tu.

Wakati wa utawala wa Kikwete Baraza la Maaskofu TEC ilikuwa mstari wa mbele kupiga kelele dhidi ya dhulma na haki.

Leo wako wapi akina Tarcisius Ngalalekumtwa Rais wa TEC? Wako wapi akina Askofu Method Kilaini, Rwaichi, Lebulu na wengineo?

Au wakatoliki wamekaa kimya kwakuwa Mkatoliki yupo ikulu?

Viongozi wa dini kemeeni uovu acheni ubaguzi
Aisee...|O
 
Kwa hicho kipengele cha kua mkweli,kuna mtu mmoja hata kuambiwa ukweli,mtu anaeweza kuongea ukweli ni yeye tu.
Usije ukamponza kama ndio hivyo.
 
Ingekuwa yaliyosemwa juu yake ni kweli kulikuwa hakuna haja ya uzi fb ili wamfahamu.

Labda katenda kidogo, huduma take haijafikia kiwango cha kusheherekewa tena ukichukulia ni askofu.

Kwa kuwa kila mti hutambulika kwa matunda yake basi atatambulika kwa jinsi alivyo pasipo kumtafutia kiki.

Halafu umesema eti SECUCO ni nini vile? Hiyo sekondari ipo wapi?Tafakari!
 
Back
Top Bottom