Watanzania wanamjua Dr. Munga?

Watanzania wanamjua Dr. Munga?

WATANZANIA MNAMJUA Dr STEPHEN MUNGA?

Sijui kama watanzania wanamjua huyu Dr Stephen Munga vizuri,sina uhakika na swali langu lakini yapo mambo kadhaa ambayo nayajua kuhusiana na watanzania kwa Dr Huyu.

Kwanza najua wapo ambao wamewahi kulisikia hili jina.

Pili najua wapo ambao wanamfahamu kwa kumuona .

Tatu najua wapo ambao wanamfahamu kwa kazi na cheo chake

Nne najua kuna ambao hawajawahi kulisikia hili jina na wala hawamfahamu kwa lolote, hii ni kawaida tu!

Lakini pia wapo ambao wamemjua na wanamjua kwa huduma yake .

Vile vile naelewa kuwa watu wengi wanamjua Dr Munga kwa namna tofauti tofauti lakini hofu yangu iliyonifanya mpaka nikaamua kukaa na kuandika haya ni ile kutokujua kuwa Je?

Watanzania wanamjua huyu mtu vizuri?

Wanamfwatilia?

Wanamtumia?

Wanafikiwa na ujumbe wake?

Wanaijua thamani yake?

Ki ufupi mimi nilianza kumfahamu Dr Munga miaka ya 2004/2005 wakati huo akiwa kwenye harakati za kuhakikisha Chuo Kikuu cha SEKOMU kinajengwa. Nakumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuhangaika huku na kule kutafuta wafadhili, kushawishi watu na kuhamasisha kuwa kwa hali yeyote Chuo kikuu kijengwe. Hapo ndipo nilimjua huyu mtu akiwa anashirikiana na mkewe Dr Aneth Munga.

Tangu hapo nilianza kumfwatilia Dr STEPHEN MUNGA mpaka leo namfwatilia sana.

Kwanza kabisa huyu jamaa ni msomi mzuri tu. Ana PhD (Doctor of Philosophy) katika maswala ya Theolojia na kama sikosei kuna Politics kidogo humo. Alisoma LUND UNIVERSITY nadhani ni Ujerumani. Kwa hiyo huyu jamaa ni msomi kwelikweli.

Pili huyu jamaa ndie Askofu wa moja ya Dayosisi kubwa kabisa Tanzania ambayo ni Dayosisi ya Kaskazini mashariki huyu ni Askofu wa hiyo Dayosisi katika kanisa la KKKT.

Tatu Huyu Dr Stephen Munga ni Chancellor wa SEKOMU (SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY), Hiki ni chuo kikubwa sana katika vyuo vikuu binafsi hapa Tanzania, ni chuo ambacho kiko kule Lushoto eneo la Magamba.
Ni moja ya Vyuo vikuu pekee vyenye mandhari kama ya Nchi za Uholannzi au Uswizi kulingana na mazingira yake ya ubaridi na ukijani uliotawala uoto wa eneo lenyewe. Ni chuo kizuri sana.

Lakini zaidi ya hayo DR Stephen Munga amejipambanua kuwa askofu tofauti na maaskofu wengine kwa kuwa Mkweli, huyu jamaa ni mkweli na ndio maana hata kama siku nasikia uvivu wa kuhudhuria ibada nikisikia Askofu Munga yupo lazima niende kwasababu lazima nitapata vitu adimu kutoka kwake. Nampenda sana.

Huyu jamaa anafwata nyayo za mitume wa zamani, anafwata nyayo za Yesu kristo.

Nasema hivyo kwasababu baadhi ya Viongozi wa dini wa siku hizi ni waoga, hawasemi ukweli wakati mwingine kwa kuogopa mamlaka lakini Dr Munga ni tofauti yeye anasema ukweli.

Mussa alipokuwa anawapeleka watu wa Mungu Canaan walipopata kiu alihangaika kuwapa Maji, walipopata njaa alihangaika kuwapa Chakula, walipoumwa alihangaika kuwatafutia dawa mfano walipoumwa na nyoka jangwani japo lengo la safari ilikuwa sio kula,kunywa wala huduma kama hizo.

Yesu Kristo alipohubiri kwa masaa mengi na kuona watu wana njaa aliagiza iletwe mikate na samaki wachache akavibariki na maelfu kwa maelfu wakala na kushiba japo lengo la mahubiri yake ni kuuendea ufalme.

Viongozi wengine wa dini wanafikiri kuwa wajibu wao ni kuhubiri habari za kwendaa mbinguni pekee, kufungisha ndoa, kuzika waumini wakifariki, kukusanya sadaka…sio kweli. Ingekuwa ni hivi hata Yesu asingekufa, asingeuawa na watawala wa Roma.

Viongozi wa Dini wanatakiwa wawe mstari wa Mbele kukosoa watawala, kuwaelekeza waumini wao ninini wafanye katika ufasaha na hapo wawahubirie habari za kumuona Mungu, wasipofanya hivyo watawahudumu waumini wachovu, waliovunjika mioyo, wajinga, wenye njaa, wenye mateso, wanyonge na wasiojitambua…wakati huo huo mbinguni hakitaingia kilicho kinyonge.

Asante sana DR STEPHEN MUNGA kwakuwa wewe umekuwa tofauti…

Hivi MEDIA zinakuona?
WATANZANIA wanakujua?

JE WATAWALA?

IBADA NJEMA WAKRISTO WOTE,

WASIO NA DINI SIKU NJEMA

WAISLAM WOTE NA WENYE DINI NYINGINE TUOMBEANE!
96d5de7ca84396f8a73e6b28af836c3e.jpg
8d42a1b4aed163009c6adb1f031dac2e.jpg
7fad61911bdc6fb7b7290971b9444714.jpg

Ulijaribu kuuliza kama chadema waliufata ushauri wake, alipotoa ushauri juu yao?
 
Yuko vizuri kuna mashetani yanataka kumchafua
 
Dr. Munga is the man of God... viongozi wengine wameufyata kazi yao kukusanya sadaka tu.

Wakati wa utawala wa Kikwete Baraza la Maaskofu TEC ilikuwa mstari wa mbele kupiga kelele dhidi ya dhulma na haki.

Leo wako wapi akina Tarcisius Ngalalekumtwa Rais wa TEC? Wako wapi akina Askofu Method Kilaini, Rwaichi, Lebulu na wengineo?

Au wakatoliki wamekaa kimya kwakuwa Mkatoliki yupo ikulu?

Viongozi wa dini kemeeni uovu acheni ubaguzi
Uchaguzi wa TEC wa mara ya mwisho ulikuwa influenced na watu wa TISS. Waliweza kumpenyeza na kisha kumchagu-lisha Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo la Mbeya kuwa Mwenyekiti wa TEC kwa miaka 5 kuanzia 2018. Eti ilionekana kuwa kanisa liko mbali na Serikali wakati wa Mwenyekiti Tarcissius Ngalelikumtwa wa Iringa hivyo basi wamchague Gervas Nyaisonga kwa vile ana urafiki binafsi na Jiwe.

Hapo ndipo kanisa Katoliki Tanzania limebakia poyoyo katika mstakabali wa kutetea waumini wao.

KKKT waliruka mtego wa TISS uliotaka kumtoa Dr Shoo.
 
duuhh!!! Ndugu yangu ww humjui huyo mtu vizuri labda unamuona tu ni mafia balaa ukimjua vizuri hata kanisani hutaenda uliza waliosoma nae na kufanya nae kaz kwa karibu Mungu ana siri kubwa ndio maana hatumuoni kama tungekuwa tunauwezo wa kuonana nae Tungemhoji maswali mengi nahisi tungemkera
 
Uchaguzi wa TEC wa mara ya mwisho ulikuwa influenced na watu wa TISS. Waliweza kumoenyeza na kisha kumchagu-lisha Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo la Mbeya kuwa Mwenyekiti wa TEC kwa miaka 5 kuanzia 2018. Eti ilionekana kuwa kanisa liko mbali na Serikali wakati wa Mwenyekiti Tarcissius Ngalelikumtwa wa Iringa hivyo basi wamchague Gervas Nyaisonga kwa vile ana urafiki binafsi na Jiwe.

Hapo ndipo kanisa Katoliki Tanzania limebakia poyoyo katika mstakabali wa kutetea waumini wao.

KKKT waliruka mtego wa TISS uliotaka kumtoa Dr Shoo.
Duh hii hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom