Nimesikitishwa na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Habari Leo ukurasa wa nne kwamba wakazi wa Ludewa wanakula nyani kutokana na kushindwa kumudu gharama ya kununua nyama ya ng'ombe. Watanzania tumekua mafukara kiasi hiki?
Usipo guswa na masahibu yanayomgusa jirani yako ujue upo karibu kutojali hata masuala muhimu yanayokuhusu.ya habari keo muachie habari leo
Filikunjombe anapenda kuuza sura tu kwenye magazeti na TV aonekane anafanya mambo makubwa wakati hakuna kitu.Wapangwa na Wamanda wameshindwa hata kufuga mbuzi ili wapate kiotoweo?
Filikunjombe wanamsifia sana, n kitu gani spesho amewafanyia wana Ludewa? Soon tutasikia wanakula kunguru kwa kukosa hela ya kununua kuku
mbona nyani ni mnyama kama wengine tu mkuu. Hizo zote ni protein tu, sema mazoea tu! Kwa mchina jongoo ni delicacy kama ilivyo kiti moto kwa mkristo au muislam. Unajua ni kwa nini mahenge hakuna nyani, sababu ni hiyo kwamba kwa mpogoro nyani ni kitoweo kizuri tu.
Nyama ya nyani inaliwa! sema tu huyo mwandishi kaamua kutoa sababu alizoambiwa ambazo mimi naona hazina ukweli, kwa tamaduni za kusini nyama ya nyani ni mboga nzuri tu! mimi kwetu mtwara na tunakula vizuri kama mboga ya kawaida pia ukisikia samaki nchanga pia ni chakula kizuri na tunatumia!Nimesikitishwa na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Habari Leo ukurasa wa nne kwamba wakazi wa Ludewa wanakula nyani kutokana na kushindwa kumudu gharama ya kununua nyama ya ng'ombe. Watanzania tumekua mafukara kiasi hiki?
Kama ni utamaduni wa Ludewa wafugwe ili wazaliane wasijewakatoweka.Nyama ya nyani inaliwa! sema tu huyo mwandishi kaamua kutoa sababu alizoambiwa ambazo mimi naona hazina ukweli, kwa tamaduni za kusini nyama ya nyani ni mboga nzuri tu! mimi kwetu mtwara na tunakula vizuri kama mboga ya kawaida pia ukisikia samaki nchanga pia ni chakula kizuri na tunatumia!
Kweli nyani naweza kuwa kitoweo lakini lakini si utamaduni wa Watanzania. Sababu inayotolewa ni ukata si kwamba wanakula kwa kupenda.
Kweli nyani naweza kuwa kitoweo lakini lakini si utamaduni wa Watanzania. Sababu inayotolewa ni ukata si kwamba wanakula kwa kupenda.
No! nyani wa kufuga hakuna atakayekula! watu wanapenda wale walioko porini bwana! hata samaki nchanga waliopo ndani ya nyumba watu hawahangaiki nao! wanapendelea wale waliopo porini pia!Kama ni utamaduni wa Ludewa wafugwe ili wazaliane wasijewakatoweka.
Nyani ni mnyamapori, unaposema waendelee tu kuwala huoni kama ni uvunjaji wa sheria za wanyamapori?No! nyani wa kufuga hakuna atakayekula! watu wanapenda wale walioko porini bwana! hata samaki nchanga waliopo ndani ya nyumba watu hawahangaiki nao! wanapendelea wale waliopo porini pia!
Mimi karibu nipigane na jamaa aliponiambia watanzania wanakula mbwa isipokuwa paka hana uhakika ila mbwa anauhakika. Nilikataa mpaka karibu kulia kuwa anatusingizia. Hii ya leo kali kumbe watu wanatusanifu.