Watanzania wanakula nyani!

Kamura

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
506
52
Nimesikitishwa na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Habari Leo ukurasa wa nne kwamba wakazi wa Ludewa wanakula nyani kutokana na kushindwa kumudu gharama ya kununua nyama ya ng'ombe. Watanzania tumekua mafukara kiasi hiki?
 
Waache uchu nao. Kwani ni lazima wale nyama. Si waende ziwani wakale mbasa?
 
Nimesikitishwa na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Habari Leo ukurasa wa nne kwamba wakazi wa Ludewa wanakula nyani kutokana na kushindwa kumudu gharama ya kununua nyama ya ng'ombe. Watanzania tumekua mafukara kiasi hiki?

Wapangwa na Wamanda wameshindwa hata kufuga mbuzi ili wapate kiotoweo?
Filikunjombe wanamsifia sana, n kitu gani spesho amewafanyia wana Ludewa? Soon tutasikia wanakula kunguru kwa kukosa hela ya kununua kuku
 
Filikunjombe anapenda kuuza sura tu kwenye magazeti na TV aonekane anafanya mambo makubwa wakati hakuna kitu.
 
mbona nyani ni mnyama kama wengine tu mkuu. Hizo zote ni protein tu, sema mazoea tu! Kwa mchina jongoo ni delicacy kama ilivyo kiti moto kwa mkristo au muislam. Unajua ni kwa nini mahenge hakuna nyani, sababu ni hiyo kwamba kwa mpogoro nyani ni kitoweo kizuri tu.
 
Kweli nyani naweza kuwa kitoweo lakini lakini si utamaduni wa Watanzania. Sababu inayotolewa ni ukata si kwamba wanakula kwa kupenda.
 
Nimesikitishwa na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Habari Leo ukurasa wa nne kwamba wakazi wa Ludewa wanakula nyani kutokana na kushindwa kumudu gharama ya kununua nyama ya ng'ombe. Watanzania tumekua mafukara kiasi hiki?
Nyama ya nyani inaliwa! sema tu huyo mwandishi kaamua kutoa sababu alizoambiwa ambazo mimi naona hazina ukweli, kwa tamaduni za kusini nyama ya nyani ni mboga nzuri tu! mimi kwetu mtwara na tunakula vizuri kama mboga ya kawaida pia ukisikia samaki nchanga pia ni chakula kizuri na tunatumia!
 
Kama ni utamaduni wa Ludewa wafugwe ili wazaliane wasijewakatoweka.
 
Kweli nyani naweza kuwa kitoweo lakini lakini si utamaduni wa Watanzania. Sababu inayotolewa ni ukata si kwamba wanakula kwa kupenda.

Ni kweli uyasemayo,huwezi kuacha kula ugali otelini kisa umekosa wali ni ngumu sn so utakula kilekile ulichokikuta kwa wakati huo sbb hamna option nyingine watafune tu
 
Kweli nyani naweza kuwa kitoweo lakini lakini si utamaduni wa Watanzania. Sababu inayotolewa ni ukata si kwamba wanakula kwa kupenda.

Mkuu, mbona WaTz hatuna utamaduni mmoja kwenye chakula?? Kila kabila lina utamaduni wake katika chakula. Kwa mfano, Msukuma anasema wali si chakula, chakula kwa msukuma ni ugali. Wamasai hawali samaki wakati makabila mengi yanachangamkia fish!!! Waache waendelee kula nyani, kwanza siyo sumu. Kwa binadamu kila kitu ni chakula mradi tu siyo sumu!!!
 
Kama ni utamaduni wa Ludewa wafugwe ili wazaliane wasijewakatoweka.
No! nyani wa kufuga hakuna atakayekula! watu wanapenda wale walioko porini bwana! hata samaki nchanga waliopo ndani ya nyumba watu hawahangaiki nao! wanapendelea wale waliopo porini pia!
 
Nyani ni mnyamapori, unaposema waendelee tu kuwala huoni kama ni uvunjaji wa sheria za wanyamapori?
 
Mimi karibu nipigane na jamaa aliponiambia watanzania wanakula mbwa isipokuwa paka hana uhakika ila mbwa anauhakika. Nilikataa mpaka karibu kulia kuwa anatusingizia. Hii ya leo kali kumbe watu wanatusanifu.
 
Wanasema kilo moja inauzwa kati ya Sh 2000 na Sh 3000.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom