Watanzania Wanachangia Milioni 300 za harusi lakini hawawezi kuchangia Milioni 20 za kujenga darasa

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,016
2,000
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
 
Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,630
2,000
Kuna vitu vingine vina shangaza sana mpaka unajiuliza maswali..Unakuta mtaa una lalamika mitaro imeziba wanaiomba serikali wakati jambo lipo ndani ya uwezo wao ndani wana acha mpaka wana pata kipindu pindu vitu vya upuuzi ndio wanajitoa vigodoro na sherehe zingine zisio kuwa na maana..
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,016
2,000
Hii ameandika Prof. Joseph Mbele ...

Warsha Zangu Hazina Posho

Tangu mwaka juzi, nimeendesha warsha Tanzania, kuhusu masuala ya utamaduni, utandawazi, na maendeleo. Nina malengo kadhaa katika kufanya hivyo.

Lengo moja ni kuwapa wa-Tanzania ujuzi ambao ninaendelea kuupata huku ughaibuni, kutokana na kusoma vitabu, kuongea na watu, na kuendesha warsha kuhusu masuala niliyotaja hapo juu. Natambua umuhimu wa kutoa fursa kwa wa-Tanzania kuyaelewa masuala hayo, waweze kujizatiti kwa ushindani wa dunia ya leo. Hakuna msingi bora na imara kuliko elimu.

Lengo la pili la kuendesha warsha hizi Tanzania ni kuleta mwamko mpya katika mfumo na uendeshaji wa warsha. Kwanza, kuna mtindo wa kutegemea wafadhili. Watu wamezoea kuona warsha zikifanyika kwa kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili au taasisi fulani. Wahudhuriaji wa warsha wanategemea kulipiwa gharama za ushiriki, pamoja na posho. Vibahasha vya posho ni sehemu ya utamaduni wa warsha katika Tanzania.

Ninapinga utamaduni huu. Sitafuti wafadhili wa kulipia warsha zangu, na warsha zangu hazina posho. Badala yake, wanaohudhuria wanalipia.

Kwa mtazamo wangu, warsha ni fursa ya kujielimisha. Elimu ni mtaji mkubwa, pengine muhimu kuliko mitaji yote. Kama mtu analipia trekta limzalishie mazao shambani, kwa nini asilipie mtaji huu mkubwa kuliko yote, yaani elimu?

Huku Marekani, ninaona utaratibu huu wa kulipia warsha. Mimi mwenyewe nimeshalipia hela nyingi kuhudhuria warsha hizi. Ninajua umuhimu wake. Niligusia kidogo jambo hili katika blogu hii, nilipoongelea suala la kununua vitabu.

Ninanunua pia vitabu na kuvisoma. Kati ya vitabu nilivyonunua hivi karibuni ni Global Literacies. Kwa kusoma vitabu na kuhudhuria warsha, ninajiongezea mtaji wa elimu. Ufanisi wangu kama mtoa mada na mwendesha warsha unaendelea kuongezeka.

Katika kuendesha warsha zangu Tanzania, nataka kujenga utamaduni wa kuthamini elimu. Msimamo huu unanipa wajibu mkubwa. Nawajibika kujielimisha kwa uwezo wangu wote, ili niweze kuwa mwelimishaji bora. Ndio maana ninafanya bidii kuhudhuria warsha, kununua vitabu na kuvisoma, na pia kuendesha warsha. Ninaelimika hata ninapoendesha warsha.

Nawakaribisheni kwenye warsha zangu za mwaka huu:
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,016
2,000
Kuna vitu vingine vina shangaza sana mpaka unajiuliza maswali..Unakuta mtaa una lalamika mitaro imeziba wanaiomba serikali wakati jambo lipo ndani ya uwezo wao ndani wana acha mpaka wana pata kipindu pindu vitu vya upuuzi ndio wanajitoa vigodoro na sherehe zingine zisio kuwa na maana..
Haya ni maradhi mabaya sana kwa kizazi kilichopita - kilichopo ... na sasa kijacho tujaribu kukipa kinga. Ona hii ... kuna madarasa kama sita hivi Sengerema yamejengwa kwa nguvu ya wananchi wachache - lakini uongozi unashindwa kutoa shinikizo kwa serikali kumalizia kazi iliyobaki ili wanafunzi waondokane na changamoto ya kutembea umbali mrefu.
Ukiongea na baadhi ya viongozi - wanakwambia hii tuiandikie write-up ili tupate ufadhili toka kwa donors ....
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,016
2,000
Tumeishajua wazi kuwa wanasiasa hawana nia ya dhati ya kuinua kiwango cha elimu kwa sababu kwao wajinga ndo mtaji wao. Hivyo kuendelea kuwategemea wanasiasa ni kujirudisha nyuma wenyewe. Angalia watoto wa kuanzi diwani hadi wabunge - ni mtoto yupi anayesoma shule ya kata?
Kama watoto wao hawasomi shule za kata - watapata wapi msukumo wa kuendeleza shule hizo sambamba na kushughulikia kero za elimu? Kwa kipindi hiki elimu isiyo rasmi ina tija zaidi ya elimu rasmi.
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,016
2,000
sina hakika,kama bado wanachanga...

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka ya 1990 - kulikuwa na mwamko mkubwa sana wa kuchangia elimu; sekondari kama Burudea, Kadea, Bwabuki n.k zilichangiwa na wananchi. Baada ya hapo wenye fedha walianza kufungua shule binafsi - neno ubinafsi ni shetani tosha ... kila mzazi akawa na moyo wa ubinafsi kwa watoto wake waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya sekondari.
Kwa kumbu kumbu zangu mwanzo wa kuacha kuchangia elimu ulikuwa ndo huo. Na sasa kampeini rasmi ya kutochangia elimu imeanza kwenye awamu hii. Watoto darasani utafikiri ni mkutano wa hadhara! MAKUBWA!
 
busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,647
2,000
unachosema kina ukweli flani chif

Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,837
2,000
Tumeishajua wazi kuwa wanasiasa hawana nia ya dhati ya kuinua kiwango cha elimu kwa sababu kwao wajinga ndo mtaji wao. Hivyo kuendelea kuwategemea wanasiasa ni kujirudisha nyuma wenyewe. Angalia watoto wa kuanzi diwani hadi wabunge - ni mtoto yupi anayesoma shule ya kata?
Kama watoto wao hawasomi shule za kata - watapata wapi msukumo wa kuendeleza shule hizo sambamba na kushughulikia kero za elimu? Kwa kipindi hiki elimu isiyo rasmi ina tija zaidi ya elimu rasmi.
Lakini hata ukichanga na kuwa na uwezo wa kujenga darasa bado utamtegemea huyo mwanasiasa katika kutoa ruhusa ya sehemu ya kujenga, kuthibitisha ubora wa jengo na hata kukupa wataalamu kwa ajili ya kufundisha!...kujidanganya kwamba umtenge mwanasiasa ni uwendawazimu!

Hata ile namna ya kujikusanya kuna wanasiasa wanaotoa muongozo wa wazo na namna ya utendaji wa jambo lenu labda uniambie unamaana nyingine ya mwanasiasa ni nani!

Swala la ujenzi wa miundombinu uliyotaja kimsingi ni swala la serikali yako ambayo "umechangia mchango wako" kwa kulipa kodi, kutoa ruhusa wao kukopa ili wapate fedha za ujenzi na umewapa ruhusa ya kuwaomba wafadhali wamsaidie huyo serikali (mwanasiasa) kupitia sanduku la kura na kura yako ujenzi wa shule au hospitali hiyo!

Hayo mambo tumekubaliana kwa mkataba wa KATIBA kati yangu mimi raia mlipakodi na sisi raia kwa ujumla wetu na kwa utashi wetu kabisa kwamba hayo ndio mambo ya msingi watu hawa (wanasiasa a.k.a. serikali) kututendea.

Katika maswala mengine yeyote ambayo hayapo katika mkataba huo, serikali wala mwanasiasa hana wajibu au ulazima wa kunitekelezea au mimi kulazimishwa, au kuombwa nifanyiwe kwa sababu ni mambo yangu binafsi.

Maswala haya ni kama kuchangia sherehe za harusi, kipaimara, iddi, au hata unyago.

Isiwe nongwa kwenu na kwa mwanasiasa au serikali kunionea gere kuchangia maswala ambayo "hayapo kwenye makubaliano yangu na serikali/mwanasiasa)!

Ni jukumu la serikali kuniletea shule, kituo cha afya, na watumishi wake kwa sababu nimempa hela yangu na ruhusa kukopa hata nje ili nipate hayo mahitaji!

Wivu wenu unatoka wapi nikiamua kujichangia katika sherehe na sio ujenzi wa madarasa ambao tayari nimechangia kupitia kodi?
 
pilato93

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
4,395
2,000
Sijakusoma mkuu!
Asilimia kubwa chochote kinachowafanya watu wafurahi hua kinachangiwa sana afrika mfano msiba utakuta watu wanatoa buku buku tena kwa mbinde pitisha mchango wa sherehe yeyote ile kuna mwamko mkubwa sana

mpuuzi mpuuzi tu
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
7,377
2,000
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
Tukichangia madarasa watapiga na kuandika kwenye vitabu vyao ambavyo hatuvioni kuwa wamejenga wao, pia siku ya uzinduzi watasema serikali ya CCM imejenga, wakiacha utapeli wa kisiasa tutachangia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom