Watanzania Wanachangia Milioni 300 za harusi lakini hawawezi kuchangia Milioni 20 za kujenga darasa

MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
Kama kodi tunazolipa wanashindwa kuzifanyia kazi ili zifanye hizo kazi, sisi tufanyeje? Kodi tulipe wao wazichue kuboresha vituo vya propaganda kama kule channel ten alivyo watwanga milioni 200 . afu sis jasho letu bado tulitumie kujengea vyoo!! Acha ujuha
 
Back
Top Bottom