ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Unakuta bajeti ya harusi ni milioni 19,familia yenyewe ki uwezo ni wa chini, katika familia hiyo masikini ni wengi kuliko wenye kujiweza,tunalazimishana kuchangia harusi ya siku moja mamilioni na tunashindwa kusaidia ada na mahitaji ya shule ya watoto ndani ya familia hiyo waliofaulu kuendelea na masomo zaidi!
Kwa experience yangu harusi hizi kwa hapa Tanzania huwa zina hekaheka nyingi,usumbufu mwingi kwa ndugu jamaa na marafiki kwa takriban miezi mitatu hadi minne ma kadi,ma kamati..kugharimia jambo la siku moja..tena gharama kubwa ikiwa ni wakati wa hafla jioni siku ya ndoa.
Yaani kwa muda wa masaa matano tokea saa moja hadi saa sita usiku milioni kumi na tisa inakua ishateketea na watu wamepanda mabasi na wengine usafiri binafsi na kutawanyika!
Cha kushangaza na ambacho pengine wengi hawajakitambua ni kuwa mara baada ya kuisha sherehe siku tatu au nne kila mtu kesha sahau hata kilichotokea!hakuna atakayebaki anasimulia harusi hiyo tena!
Inasikitisha tunaishi kwa mazoea mabaya mno,kuigana na formality za kizamani sana.
Nakumbuka tangu niifanye harusi yetu miaka zaidi ya kumi sijawahi shika album ya picha za harusi yetu kutazama zaidi ya mara mbili,alkadhalika dvd video,na wala hakuna hata ndugu anayeomba kuangalia picha hizo sababu unakuta labda siku ya tukio nao walikuwepo!ma album na dvd video zile zilishachakaa kwa joto hazifai wala hazi play!
Lakini wakati wa maandalizi ya sherehe kwenye vikao hizi video na picha viliwekewa bajeti hadi ya laki saba au nane!
Hapo nimetaka tu kuwafumbua akili Watanzania walio wengi kuwa tubadilike tufanye harusi ndogo, zenye bajeti ndogo sana na zenye watu wachache sana hii itatusaidia sana kupambana na umasikini.angalizo hapa naongelea kwa sie wenye familia duni za chini na kati..siongelei kwa wale familia waliojaaliwa.
Tofauti na mkimsaidia mtoto kwenda shule/chuo gharama yake pengine haivuki milioni moja Lakini hiyo pesa itakua na thamani katika maisha yote ya mtoto na you never know mtoto huyu anaenda kuwa nani baadae pengine akawa pilot, minister..teacher au doctor mkubwa ambaye ataingiza mamilioni ya pesa katika familia na kusaidia wengine wasio jiweza!
Watanzania tubadilike wenzetu wazungu hutushangaa kwa ukubwa wa ma harusi yetu na wao walishabadilika miaka mingi nyuma na ndio kisa wamepiga hatua kubwa, sie bado tunagalagala kwenye umasikini tunaoutengeneza kila siku.
Hakika tunaangamia kwa kukosa maarifa.
Mungu ibariki Tanzania.
Nawasilisha.