Watanzania Wanachangia Milioni 300 za harusi lakini hawawezi kuchangia Milioni 20 za kujenga darasa

Kuna vitu vingine vina shangaza sana mpaka unajiuliza maswali..Unakuta mtaa una lalamika mitaro imeziba wanaiomba serikali wakati jambo lipo ndani ya uwezo wao ndani wana acha mpaka wana pata kipindu pindu vitu vya upuuzi ndio wanajitoa vigodoro na sherehe zingine zisio kuwa na maana..

Haya ni mawazo ya kike, kwani kodi tunalipa kwenye michango ya harusi au kwa serikali? Ulishawahi omba kinywaji kwa serikali au kuomba barabara kwa kamati ya harusi? Kaa kwa jinsia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumehakikishiwa kuwa Elimu ni bure tangu darasa la 1 hadi kidato cha 4. Tena ikaambiwa ni marufuku michango ya aina yeyote. Imekuwaje weye watuletea za kuleta humu jf kuwa tuchangie madarasa??
Kila kitu ni bure hadi chakula cha mchana kwa watoto wetu. Tena tumeambiwa tufyatue watoto katika kipindi hiki cha 10 yrs zake. Nadhani unastahili kuchunguzwa. Huenda weye ni mwalimu mkuu unataka kula ile hela inayotolewa na serekali.
 
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.

Kinachoniudhi zaidi, ni pale wanaposhindwa kutoa laki kadhaa ili mgonjwa atibiwe ila akifariki ndo utaona mashauzi. Milioni kibao zitatumika kwa ajili ya kumsafirisha na kumzika. Hivi inakuwa kama vile wamefurah kwa kufariki kwake au vipi?
Ndio hivyo pia ktkshughuli za maendeleo. Gharama kubwa inatumika kwa harusi na shughuli ikiisha tu maharusi hawana hata hela ya mboga. Si bora kwenye hizo milion milion wangezipiga basu na maharusi wakapata kianzio cha maisha.
 
Haya Mambo NI ya kushanyaza Sana. Mtu Ana shida Hadi anafikia hatua ya kuuza nyumba yake hakuna wa kumsaidia mawazo lakini kwenye sherehe Kila kikao wanatoka amelewa. Akili au matope?
MAMBO YA KUSHANGAZA
 
Mchango wa darasa ni hizo kodi tunazokamuliwa daily, au unafikiri kodi ni kwa ajili ya kununulia bombadia na kujengea flyover tu?
Sasa madarasa hakuna lakini ukihoji unaambiwa we mpinzani. Kwani taifa halikuwa na vipaumbele Hadi kutegemea mawazo ya kundi dogo tu kununua mandege yenye sifa umazoziona mwenyewe.l?
 
Tukichangia madarasa watapiga na kuandika kwenye vitabu vyao ambavyo hatuvioni kuwa wamejenga wao, pia siku ya uzinduzi watasema serikali ya CCM imejenga, wakiacha utapeli wa kisiasa tutachangia.
Kwa hiyo ni mgomo baridi? Kina kitu nimepata hapo.
 
Lakini hata ukichanga na kuwa na uwezo wa kujenga darasa bado utamtegemea huyo mwanasiasa katika kutoa ruhusa ya sehemu ya kujenga, kuthibitisha ubora wa jengo na hata kukupa wataalamu kwa ajili ya kufundisha!...kujidanganya kwamba umtenge mwanasiasa ni uwendawazimu!

Hata ile namna ya kujikusanya kuna wanasiasa wanaotoa muongozo wa wazo na namna ya utendaji wa jambo lenu labda uniambie unamaana nyingine ya mwanasiasa ni nani!

Swala la ujenzi wa miundombinu uliyotaja kimsingi ni swala la serikali yako ambayo "umechangia mchango wako" kwa kulipa kodi, kutoa ruhusa wao kukopa ili wapate fedha za ujenzi na umewapa ruhusa ya kuwaomba wafadhali wamsaidie huyo serikali (mwanasiasa) kupitia sanduku la kura na kura yako ujenzi wa shule au hospitali hiyo!

Hayo mambo tumekubaliana kwa mkataba wa KATIBA kati yangu mimi raia mlipakodi na sisi raia kwa ujumla wetu na kwa utashi wetu kabisa kwamba hayo ndio mambo ya msingi watu hawa (wanasiasa a.k.a. serikali) kututendea.

Katika maswala mengine yeyote ambayo hayapo katika mkataba huo, serikali wala mwanasiasa hana wajibu au ulazima wa kunitekelezea au mimi kulazimishwa, au kuombwa nifanyiwe kwa sababu ni mambo yangu binafsi.

Maswala haya ni kama kuchangia sherehe za harusi, kipaimara, iddi, au hata unyago.

Isiwe nongwa kwenu na kwa mwanasiasa au serikali kunionea gere kuchangia maswala ambayo "hayapo kwenye makubaliano yangu na serikali/mwanasiasa)!

Ni jukumu la serikali kuniletea shule, kituo cha afya, na watumishi wake kwa sababu nimempa hela yangu na ruhusa kukopa hata nje ili nipate hayo mahitaji!

Wivu wenu unatoka wapi nikiamua kujichangia katika sherehe na sio ujenzi wa madarasa ambao tayari nimechangia kupitia kodi?
Hakuna mwenyewe wivu na vihela vyako Bali binafsi nashangaa akili za wabongo zilivyo za hovyo. Hivi unataka hata semina / warsha za kunoa bongo zilipiwe na serikali?
 
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
Hebu tusichoshane. Kila hela na kazi yake.
 
Watu wanataka misifa tu sasa ukijenga darasa nani anakusifia mtu anataka watu wale,wanywe baadaye wakamuadisie huko.

Serikali haina aibu kabisa inakusanya tril 1.3 kwa mwezi halafu inataka tuchangie elimu? Kwa nn? Hizo hela wanazipeleka wapi na wakati wenyewe wanasema eameziba mianya yote ya wizi na sasa wanamudu kutoa elimu bure?

Serikali iache ubabaishaji iendelee kutoa elimu bure kikamilifu kama ilivyoahidi. Hela wanazokusanya kwa mwezi zinatosha sana kutoa elimu bure. Sisi watuache tuchangiane harusi zetu na hata misiba tutakavyo.
 
Wachangie NN wakati watu wanalipa kodi ? Tra inakwambia lipa Kodi Kwa maendeleo ya Taifa , sasa mtu achangie then alipe Kodi si itakuwa double payments at a single source of income
 
Hakuna mwenyewe wivu na vihela vyako Bali binafsi nashangaa akili za wabongo zilivyo za hovyo. Hivi unataka hata semina / warsha za kunoa bongo zilipiwe na serikali?
Kutokujitambua kwako hakukupa haki ya kushangaa na kubeza uwezo wa watu wengine!

Unaweza ukawa vipi Tutor ukashindwa kuona falsafa ya andishi langu?...kwa nini ujibu juu juu kwa jazba?

Kama umeshindwa kuhoji, kupigania na kuisimamia serikali itimize majukumu yake kwako kupitia kodi unayolipa, unawezaje kuona uhovyo wa akili za wengine wakati za kwako tu hazikusaiidii hata kudai kile kilichostahili kwako?

Kama unashindwa jambo dogo namna hii, hilo kubwa la kuisimamia serikali kutumia vizuri kodi yako na hata kukuletea miundombinu muhimu ili ujiendeleze utaweza?

Sioni u Tutor ndani yako!
 
Watanzania tunafikiri kufanyiwa maendeleo na Serikali ni hisadi au msaada. Utasikia mtu mzima kabisa anahojiwa anasema tunaiomba Serikali itujengee barabarani tunateseka kwenda wilayani. Hopeless kabisa! Semeni tunaitaka serikali itujengee barabarani maana kodi si wnachukua?! Mbona wao wakija kudai kodi ukiwambia huna wanakufungia biashara hawabembelezi?!
 
Serikali haina aibu kabisa inakusanya tril 1.3 kwa mwezi halafu inataka tuchangie elimu? Kwa nn? Hizo hela wanazipeleka wapi na wakati wenyewe wanasema eameziba mianya yote ya wizi na sasa wanamudu kutoa elimu bure?

Serikali iache ubabaishaji iendelee kutoa elimu bure kikamilifu kama ilivyoahidi. Hela wanazokusanya kwa mwezi zinatosha sana kutoa elimu bure. Sisi watuache tuchangiane harusi zetu na hata misiba tutakavyo.
Hapo kwenye bold; kama imeshindwa nini kifanyike?
Tendelee kuona uozo kwenye elimu kwa kuwa seikali haioni aibu?
Tuiondoe madarakani? kwa vipi wakati wao ni mabingwa wa kuchakachua matokeo ya chaguzi karibia zote?
Naendelea kukusikiliza mkuu!
 
Watanzania tunafikiri kufanyiwa maendeleo na Serikali ni hisadi au msaada. Utasikia mtu mzima kabisa anahojiwa anasema tunaiomba Serikali itujengee barabarani tunateseka kwenda wilayani. Hopeless kabisa! Semeni tunaitaka serikali itujengee barabarani maana kodi si wnachukua?! Mbona wao wakija kudai kodi ukiwambia huna wanakufungia biashara hawabembelezi?!

Hilo polite language ndo inatuangusha; inabidi tujue wazi kuwa HAKI HUWA HAIOMBWI - -HAKI INADAIWA.
 
Back
Top Bottom