Watanzania Wanachangia Milioni 300 za harusi lakini hawawezi kuchangia Milioni 20 za kujenga darasa

MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.

Harusi ya milioni 300 ndo ikoje hiyo mkuu? Hebu tupe mfano wake.

Milioni 300 unapata bus Golden gradon single diff used mbili.
 
Afadhali yako wewe umewaza kwenye kuwekeza .... wanafanya hivyo hao wenye nazo. Sisi tunaowaza kutafuta ndo tunaona nyingi.
 
Kodi zinafanya nini? Niache kuandaa harusi yangu ya milion 5 nikachangie madarasa kutafuta nini? Niache starehe nichangie halafu hayo madarsa yawe mali ya serikali na siku ya uzinduzi waje ccm wazindue? Usifanye una uchungu sana na hii nchi wakati serikali yenyewe haina uchungu na wananchi wake. Mwenyekiti wako wa ccm amefuta ajira za walimu na madaktari ambazo hizi ajira zilikuwa zinakimbiliwa sana wanatanzania wenye kipato cha chini. (SIYO LAZIMA KUAJIRIWA NA SERIKALI KWAHIYO SIYO LAZIMA KUCHANGIA MADARASA).TUSIPANGIANE CHA KUFANYA
Nikiwa sina hela, chakula au ninaumwa hiyo serikali yako mbona siioni kuja kunisaidia?Natoa pesa zangu mfukoni kujigharamia halafu niache starehe nichangie madarasa? Tuyaache hayo shule za private zipo na kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. Watoto wa viongozi wanasoma shule za private halafu mm nichangie pesa kwa ajli ya shule ya kata ni bora pesa zichangwe zifungue shule ya private.
Miaka ya 1990 - hapo kwenye bold ilifanyika hiyo lakini siku hizi hakuna.
 
Bilion 12 zinatumika kwenye chaguzi uchwara za kumfurahisha JIWE.

Milion 900 wanalipiwa tiketi ya ndege watu wa NEC kwenda kupora chaguzi uchwara.

Pesa nyingine zinakaa kwenye fuko la JIWE na BASHITE kuhonga watu mpaka MISIKITI.

Halafu muda huo eti wananchi ndio baada ya kulipa KODI ZA KUJENGA hivyo vitu, wachange tena WAJIJENGEE !
Labda hoja yangu haijaeleweka vizuri. Ila naamini wapo wachache walionielewa!
 
Kuna kipindi nilienda ghana, kuna mtaa wanakaa mamilionea lakini barabara ya huo mtaa ni ya vumbi na mashimo kibao...sasa nikajiuliza hta hawa mamilionea wanasubiri serikali iwajengee hii barabara?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo tulijifunza kutoka serikali zetu za kiafrika angalia maisha ya viongozi wa afrika pamoja na sherehe na dhifa za kiserikali tunatumia mamilioni lakini madarasa na hospitali hamna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana. Tafakari tena.
Kabla ya kutafakali fuatilia mwenendo huu ...
ELIMU RASMI ....
Chekechea akimaliza anataka kuingia Elimu ya Msingi ... ili iweje????
Akimaliza elimu ya msingi ... anataka aendelee na elimu ya Upili (Secondary) ... ili iweje?
Akihitimu Secondary anataka aingie elimu ya juu ..... ili iweje?
Akitoka elimu ya Juu anataka aingie chuo ... ili iweje?
Akitoka chuo anataka ajira .... ajira iko wapi? HAKUNA. ..

ELIMU ISIYO RASMI
Mchukue kijana wa STD VII au Form IV
* Mfundishe mbinu za kujifunza ... alafu
*Mfundishe mbinu za kutafuta fursa ... alafu
*Mpatie maarifa ya kazi kulingana na uelewa wake ...

Huyu anakuwa tayari ametoka .. hahitaji kuangaika tena na makaratasi kuzunguka eti anatafuta ajira. Huyu anatafutwa kwa ujuzi alio nao ili afanye kazi.
 
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
Huso sio ukweli madarasa tunachangia kupitia kodi zetu za harakati za kila siku mfano.Income Tax,VAT,makodi yasioeleweka.SO MTUACHE WANANCHI TUPUMUE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tunalipa kodi hatulalamiki,
Tunachanga kujenga madarasa na kununua madawati hatulalamiki,
Anayepokea kodi yetu anaitumia kununua watu!!!
Huo moyo wa kujenga madarasa tutaendelea nao kwa style hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
Waulize serikali yako,kwanini wanajenga uwanja wa kimataifa chato badala ya kujenga madarasa?
-kwanini wananunua magari ya washawasha na silaha kila chaguzi zinapokaribia badala ya kujenga madarasa?Mwaka 2015,yallingizwa magari 777 ya polisi kwa ambapo kila moja ilikuwa mil 120!
-Hujasikia kivuko kibovu kikinunuliwa kwa mabilioni na baadae kukabidhiwa jeshi ili tusihoji?
-Kwanini bil 12 zinatumika kugharamia uchaguzi wa marudio wa majimbo matatu kisa tu kumfurahisha bwana mkubwa kuwa anaungwa mkono????

Baada ya hayo,unakuja kuniambia nichangie madarasa,bora nichangie harusu na vigodoro tu,labda mtumie nguvu!
 
Mchukue kijana wa STD VII au Form IV
Ni baada ya kujua 'Kusoma na Kuandika kwa ufahamu' ambavyo amevipata kutoka mfumo rasmi wa elimu! Maarifa na elimu vinapowekwa pamoja ni bora zaidi kuliko kimoja wapo hata kama kitazidishwa mara mbili au zaidi.
Mfano mtu kafundishwa kufuga ng'ombe (maarifa) na mzazi wake afu akanyimwa fursa ya elimu rasmi ataendelea kupangiwa pa kulishia mifugo yake na baadaye kufurushwa tena....
 
Mkuu mimi siko na hao wakoloni weusi - hapo kwenye bold usiniunganishe.
 
Ni baada ya kujua 'Kusoma na Kuandika kwa ufahamu' ambavyo amevipata kutoka mfumo rasmi wa elimu! Maarifa na elimu vinapowekwa pamoja ni bora zaidi kuliko kimoja wapo hata kama kitazidishwa mara mbili au zaidi.
Mfano mtu kafundishwa kufuga ng'ombe (maarifa) na mzazi wake afu akanyimwa fursa ya elimu rasmi ataendelea kupangiwa pa kulishia mifugo yake na baadaye kufurushwa tena....
Uko sawa - ila elimu rasmi ndo imezalisha vijana wengi tegemezi .. au hulijui hilo? Nenda migodini uone vijana wenye elimu isiyo rasmi wanavyopiga kazi.
 
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
kujenga madarasa au miundombinu ya umma ni kazi na wajibu wa serikali,kwani yenyewe ndio inayokusanya kodi zetu ili ijendeshe katika kutimiza wajibu wake wa kutuletea maendeleo ,kwa kuibua miradi na kutumia kozi zetu vizuri.sio jukum la kisheria kuchangishana pesa za madarasa wakati kodi zetu zinatumika vibaya kwa kununua wanasiasa wa upinzani ili wajunge upande wa utawala ili kuonekana wanapendwa .Tilion 2 na usheee hazijulikani zilipo zingejenga madarasa mamgapi?hela za marudio ya uchaguzi kwa majimbo ambayo wabunge kwa "hiari" yao wamejiuzuru kisha kwenda upande wa pil zisingetosha kujenga madarasa kadhaa??
 
ila elimu rasmi ndo imezalisha vijana wengi tegemezi
Kusoma vitabu na kuhudhuria warsha ni mchepuko tu wa elimu rasmi. Mwezeshaji wa warsha anatumia ubao na chaki (projector - kileo) na mwanafunzi 'kalamu na karatasi' sawa na elimu rasmi!.... ELIMU RASMI NA ISIYO RASMI vinafanya vizuri zaidi vinapokuwa pamoja... kumbuka uliandika pahala haya 'ili kufanikiwa ... maarifa, hekima na busara' Maarifa nadhani ulimaanisha Taaluma.
Hata hivyo wa-Tanzania tunapaswa kuwaza kuwekeza zaidi leo (sasa), kesho na hata milele kwenye elimu (maarifa) zaidi kuliko vitu vya muda mfupi kama harusi n.k.
 
MARADHI MABAYA SANA KWA WATANZANIA …

“Hawataki kusoma vitabu na hawako tayari kuchangia elimu”

Wamarekani wana kiu ya kusoma vitabu tofauti na Watanzania na huu utamaduni wa kutosoma vitabu sijui tumerithishwa na nani. Lakini hiyo ndiyo dalili ya awali ya utamaduni wa Mtanzania kutothamini elimu.

Mfano angalia sherehe za harusi za watoto wa wakubwa ama familia za matajiri utaona siku moja tu harusi inagharimu mamilioni ya shilingi lakini wakubwa hao hao hawawezi kuchangia mamilioni kujenga darasa wala choo cha wanafunzi wako radhi kuandika "writeup" na kuiwasilisha USAID, DANIDA JICA UNDP wakiomba milioni chache kama msaada wa kujenga choo!

Mtu unashangaa harusi ya milioni 300 Watanzania wanazo wanachangia lakini choo au darasa linalogharimu milioni 20 wanataka mfadhili ajitolee haya ni maradhi mabaya tuombe Mungu atusaidie.

Inaandaliwa semina kwa ajili ya kutoa elimu kombozi ... watu hawataki kuhudhuria. Ukiwaambia wachangie kidogo hapo huoni mtu ... ukiwatangazia kuwa ni bure ... wanauliza kama kuna chakula na posho!

Kama wewe ni mmoja wa watu wa namna hii ujue wazi kuwa una matatizo makubwa sana kwenye mfumo wako wa kufikiri.
Siku hizi elimu na afya ni biashara, ndiyo maana utakuta hospitali na shule nyingi za watu binafsi zimeenea nchini na wamiliki wengi ni watu waliyokuwa aidha wanafanya kazi serikalini au kuna watu wenye ubia na watu wa serikalini. Hivyo usitegemee watu wachangishane kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, na kusoma vitabu ni "hobby" kwa baadhi ya watu, wengi wetu hatuna hiyo "hobby".
 
Back
Top Bottom