Watanzania wana uelewa mdogo kuhusu Pension Fund, 25% ni maamuzi sahihi

yaani...ni shida ....super brand siku hizi ni shida....woga kama wote...bila sababu za msingi...
mada kama hii ya mafao...inayogusa masilai ya watu wengi...na haina chembe ya uchonganishi au siasa inatakiwa ipande hewani super brand
Hua wananikera sana, alafu vipima joto vyao vina majibu ya waziwazi ata mtoto wa primary anajibu
 
Sijajua ulikuwa baa gani wakati unaandika upupu huu wakati unakariri hiyo topic moja ya economics. Yaani waambie waliokutuma kwamba hatubadiliki hata wakitoa elimu kwa kutufunua vichwa na kujaza notice kama hizi zako. Tumechoka na tumeshachoka kweli kufanywa wapumbavu huku viongozi wa serikali ambao wengine tulisoma nao wakiwa vilaza Leo wanajiona wana akili kuliko watanzania wote kwa vile tu wana nafasi ya maamuzi ya kisiasa juu yetu. Hiyo hoja ya kitoto kwamba mstaafu akipewa fedha yake yote atatitumia vibaya kawaelezeni na wabunge ambao walipewa pensheni ya zaidi ya 200m Leo wanatembea "rightblue leftyellow" halafu sheria hii kandamizi haiwagusi. Yaani mnaanza kupangia watu matumizi ya fedha zao binafsi nyie Nani anawapangia za kwenu. Mbona mshahara mnawalipa kila mwezi lakini wapo wanaotumia vibaya na wapo wanaotumia vizuri. Kuna mtumishi Leo anapokea take home 450,000 lakini anaishi maisha ya kuridhisha kuliko Afisa wake anayepokea 1.35m yaani x3 yake sababu ya mpangilio mzuri wa matumizi yake! Mmemnyonya mtumishi kwa miaka 30+ halafu mnataka kumzika kabisa anapostaafu? Ukatili gani huu!! Halafu wewe uliyeshiba kwa kutumia fedha za wastaafu maana kwa maneno yako ni wazi uko kwenye mfuko mmojawapo wa pensheni unakuja kukejeli watumishi eti wakilipwa zote watatapanya pensheni!!? Waambie waliokutuma umeshimdwa !! Loby type person wewe!!
Hii sio economics ni uelewa tu wa mambo, soma vizuri hitimisho na maelezo yangu

Principal ya Pension ni wewe ufe mapema, ukiishi Sana kwao shida

Mkuu Wewe wanaangalia mortality Table tu
 
Kiongozi ndio maana nimekuambia kuna aina nyingi za kuchangia, Elimu ni ndogo sana ya pension hapa kwetu, Huo mfumo wa ma DC au RC ni ishu ya Wataalamu tu kuamua, wao wanalipwa kwa Mara moja wanaita "Gratuity "

Kikubwa ni kuelimisha Raia mifumo iliyopo halafu tuchague
Huu mfumo ni mzuri kwe makaratasi.ukirudi kwenye uhalisia si rafiki kama ulivyoupamba na studying materials. Watz wengi mishahara yao haiwawezeshi kufanya savings' ukizingatia na extended families tulizo nazo sababu ya Ujamaa, Mtumishi mpaka anastahafu anashindwa hata kuwa na nyumba ya kuishi' anategemea mafao anunue kanyumba aweke hata na wapangaji apate hela ya kula na kuendelea na maisha. Pili huu mfumo kwa kijana mwenye ndoto ya kujiajiri si rafiki' mtu analipwa laki saba anategemea akae kazini miaka 15 huku akijiandaa kuanzisha mradi wake aachane na ajira ili atengeneze ajira tayari keshafeli, ataajiriwa mpaka 60 huyo. Mwisho huu mfumo unatengeneza nidhamu ya uwoga kwa vijana, hawawezi kuwa jasiri kazini, wahindi watawatumikisha kweli sababu wanajua kazi zilivyo za shida na ukiacha kuna changamoto ya mtaji. Angalau mfumo ungesema kiasi unachokatwa kwenye mshahara wako(si mwajiri) kinaweza tumika kama dhamana ya mkopo wa ujenzi wa nyumba au biashara. Utaniambia mifuko ya Jamii haikuanzishwa ili kukuza mtaji' sawa, Ila ukumbuke pia maandalizi ya Uzee ni wakati mtu ni kijana' akiweza kujenga akiwa kijana uzeeni hatapata shida' akiwa na biashara mapema' uzeeni atawarithisha wajukuu na watoto yeye akiwa msimamizi na mshauri. Mifuko ingejikita kwenye kuhakikisha kwamba mawekezo yanayofanywa na wenye mafao kwa udhamini wa hayo mafao ni ya mafanikio, si kushikilia kuwa pesa haikuwekwa kwa ajili ya mtaji bali kukuhudumia uzeeni. swali la kujiuliza ni kwa mazingira yetu hapa Tz kiuhalisia Wazee wastaafu wanaishi kama mifuko inavyojinadi? Wazee wanahitaji kupatiwa ela nyingi kidogo kidogo halafu akalipe kodi ya nyumba au anahitaji kuwa na nyumba halafu alipwe kidogo ya kumwezesha kula? Wazee wengi kiuhalisia wanategemea watoto/wajukuu wao ambao na wao vimshahara ndo hivyo. Mfumo mzuri ni ule unaomwezesha mzee kuwa na mahali pa kuishi na kidogo apate ela yake ya kula. Na si lazima hili lifanyike akiwa mzee, linaweza kufanyika akiwa kijana na ana nguvu ili Uzee umkute tayari anajiweza kiuchumi
 
Kwaio wastaafu wa bungeni tuu ndo wana akili ndo maana wanapewa 100%? Ficha ujinga wako
Asante kwa kuniita mjinga maana napenda kujifunza sana habari mpya.
Kwa sasa wafanyakazi mahiri kama Maprofesa wa afya wameongiozewa muda wa kustaafu.
Badala ya kustaafu miaka 60 wameongezewa miaka mitano zaidi, hivyo wanastaafu baada ya miaka 65.
Unajua ni kwanini nao wamekubali ?
Kwakuwa wewe ni mwelevu tafuta jibu.
Nilichosahihisha ni kwamba, hiyo asilimua 75 inayoachwa inaisha baada ya miezi 80 yaani wastani wa miaka sita tu, jambo ambalo wastaafu wengi wanafikisha hiyo miaka la sivyo hawa Maprofesa wangefia kazini siku zote.
Mpango huu unalengo la kumwajiri mtumishi maisha yake yote.
Hizi nchi za tatu hazina vituo vya kulelea wazee.
Hivyo wazee wastaafu wanaishia kufa kwa umaskini.
Hivyo vimilioni 100 au 150 havifiki popote.
Miaka yote ya nyuma wastaafu walikuwa wanachukua lump sum yote na tumewashuhudia wakiishia kuishi maisha magumu sana.
Hadi serikali ikaamua kuwaonea aibu Maprofesa na kuwaongezea miaka mitano.
Walimu wengi wa vyuo au sekondari tuwashuhudi wakisha staafu na kupewa mafao yao yote baada ya muda kidogo tu wanaanza kutafuta shule au vyuo ili wafundishe part time.
Sasa watumishi kama makarani, makatibu muhtasi, nk.watapata wapi part time za kufanya kazi popote ?
Wengi mnachangia kwa hisia badala ya kufanya kwanza utafiti wa kina.
Serikaloi ipo sahihi kabisa kwa uamuzi huu.
Serikai imechoka kuwaona watumishi wake miaka michache baada ya kustaafu wanaishia kuwa ombaomba.
Wengine wanafika hadi kwenye ofisi walizofanyia kazi na kuhitaji msaada wa fedha.
Acheni hizo.
 
Rudia kusoma mswada hauandaliwi na bunge bali wataalam wa sekta husika. Mashaka yoyote wanaulizwa watoe ufafanuzi. Na kwa demokrasia ya sasa WADAU wanashirikishwa
Wataalam hao hao wanaoteuliwa na jamaa au...nahic jamaa ana kazi ya kuwapigia tu simu "mwezi huu kuna bei gani?" Akishaambiwa anakaa kwenye majukwaa na kuanza kujitapa "tuna hera nyingi"

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wewe huna ulijualo.
Ivi ukipewa milioni 100 ndo unajua umefika.
Waulize Maprofesa kwanini wamekubali kuingeozewa miaka ya kustaafu.
Miaka yote ya nyuma hao wafanyakazi wastaafu walikuwa wanachukua pesa yao yote, je umewafuatilia maisha yao japo miaka mitatu tu baada ya kustaafu ?
Mimi nina uhakika nitaishi miaka mingi baada ya kustaafu.
Kama wewe unaugonjwa usiokuwa na tiba shauri yako.
 
F****ng retard. Unashindwa hata kuwa na huruma kwa ndugu zako wa ukoo unatetea wanasiasa!!!?. F**ck u man!!
Wana JF, Mambo ya 25 percent ya Pension yameongelewa sana humu ndani na kundi Fulani likilaumu serikali. Je watu wanauelewa na elimu ya Mafao (Pension)?

Je watu wanafahamu misingi ya uendeshaji mifuko ya pension jinsi inavyopata faida na hasara?

Kuna aina ngapi za pension? na ni vihatarishi gani hii mifuko inakumbana nayo ili iendelee kulipa wastaafu?

Majibu ya hayo maswali yataondoa utata na watu hawatailaumu serikali bali wataipongeza sana sana

Mosi, Serikali imepitisha sheria kuwa Mtu atalipwa 25 percent kwa mkupuo yaani ( lump sum). Halafu baadae Mtu ataanza kulipwa kidogo kidogo yaani periodical payment kwa 75 percent tunaita (Annuities)

Mode of Operations
Katika Pension funds kulipa annuities au periodical payments yaani kulipa kidogo kidogo hiyo 75 percent ni hasara kubwa sana endapo hao wastaafu wataishi miaka mingi zaidi ya makadirio, Mara nyingi mtu akistaafu hukadiriwa ataishi chini ya miaka 15 na atafariki. Commitment ya mifuko hii wamekadiria hivyo

"Longevity situation "Hii ni hali ya mabadiliko ya kimaisha ambayo imeonyesha maisha ya wanadamu yanazidi kuboreka zaidi hasa Katika kupambana na Magonjwa, Hivyo watu wengi wataishi maisha marefu sana kwa utafiti uliofanyika ( long life). Mifuko hii hapa tayari imejiiingiza kwenye hasara mpya itokanayo na longevity risk, kitendo cha kukubali kulipa 75 percent kwa kidogo kidogo wanaweza mlipa Mtu kwa Muda mrefu zaidi hivyo hasara

Moral harzad situation, Tafiti nyingi hapa Tanzania zimeonyesha watu wanatumia vibaya uwepo wa hizi faida zitokanazo na Pension fund, Wanaishi maisha hatarishi ya kuvuta sigara, kutofanya mazoezi na kutumia pesa hovyo wakitegemea Pension watapata kwa mkupuo ,Moral hazard situation ni hali ya Mtu kuishi visivyo au hovyo akitegemea pension ipo, kungekuwa hakuna pension asingeishi maisha ya hatari.

Kudhibiti hali hii ya Moral hazard ni bora ukampa mpatia Mtu 25 percent ili ajidhibiti mapema Kama mkupuo, Kumpa 75 percent kwa mkupuo kuna weza mtokea puani akidhani maisha ameyapatia kumbe ndio kifo chake mapema

MUUNDO WA UWEKEZAJI

Mifuko ya Pension uwekezaji wao mkubwa ni kwenye amana za serikali yaani "long term treasury bond na short term treasury bills, Inategemea ipate faida toka uwekezaji huu wa serikali ambayo wengi mnafahamu riba yake ni ndogo sana sana

mifuko hii kuna muda inaamua kuwekeza kwenye riba za mabenki za biashara hapa namaanisha fixed deposit, Lakini uwekezaji kwenye mabenki bado wanatakiwa kulipa kodi (withholding tax) kwenye riba wanayopata hivyo kipato kinapungua tofauti na makadirio

UELEWA MDOGO KWA WATANZANIA
Africa ya kusini Mtu anachagua mwenyewe fedha yake ya pension iwekezwe Sehemu gani, Africa ya kusini Mtu anaweza tumia pesa yake ya pension Kuweka dhamana ya mkopo au kununua nyumba dhamana ikiwa ni michango yake ya pension

Hapa Tanzania elimu ya Pension fund ni ndogo sana sana, Serikali inachofanya siyo kibaya tatizo hawajatoa elimu kwa watu

Aina za kuchangia zipo nyingi sana, Serikali yetu inaamua kutumia mfumo wa pamoja unaoitwa "Defined Benefit Plan "Huu mfumo ni mzuri kuwa watu tunachangia kwenye pool moja Mfano Nssf au Psssf, halafu toka kwenye Pool ndio maamuzi yanafanywa hii huleta usawa kidogo kwani kunakuwa na mfumo mmoja wa kupiga hesabu wa pension

Hasara za mfumo wa "Defined Benefit plan "hujui michango yako inawekezwa wapi na faida gani imepatikana, Hapa ndipo serikali ilibidi itoe elimu kwa Raia

Mfumo wa pili ambao Afrika ya kusini wamewapa Raia wao unaitwa "Defined contribution Plan "Huu mfumo unachangia kwenye pool moja lakini Kila Mtu anakuwa na akaunti yake inafunguliwa, na Raia Kila wakati anajua kiasi gani kimewekezwa na faida yake kiasi gani, Raia anaweza toa maelezo kwa mfuko pesa yake itumike vipi?

Mwisho, Kuna mabadiliko makubwa Sana Duniani kuanzia kwenye udhibiti wa Pesa mpaka mifuko ya Pension, Wataalamu wetu lazima wajifunze na kukubali mabadiliko, kuna mambo ya virtue currency BItcoins n. k, Wataalamu wajifunze wasikae kuzuia tu

Naipongeza Serikali kwa maamuzi haya ya 25 percent na 75 percent tatizo hawajatoa elimu ya kutosha

Je? Kipi muhimu wazee wetu kulipwa pesa kwa mkupuo nyingi kwa Mara moja au Walipwe kidogo kwa mkupuo halafu Kila mwezi Walipwe pension nyingi

Lengo la sheria kwa Sasa ni kuwafanya wastaafu waishi Kama wapo kazini Kila mwezi wapokee pension kubwa kuliko wanavyoishi Sasa wengi walipata kwa mkupuo halafu Kila mwezi wanaumia

JE WATOA SERA NA WATUNGA SERA WETU WANA UELEWA MPANA KUHUSU MAMBO YA PENSION?

JE UTAFITI WA KUWA WATANZANIA WANAISHI MUDA MREFU BAADA YA KUSTAAFU NI SAHIHI ?


Tutazidi kuelimishana zaidi na zaidi kwenye ishu ya Pension na Bima zote lengo ni kutoa Cover au Kinga kwa wachangiaji,Pia Serikali itoe elimu zaidi kwa wachangiaji
 
Jamaa wanachekesha kweli yaani hela nidundulize mie matumizi uniamulie jaman sio hata kukaa na wafanyakazi kuwaambia tufanyeje mnaamua TU you just wake up and decide wht to with someone's cash

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kiongozi ndio maana nimekuambia kuna aina nyingi za kuchangia, Elimu ni ndogo sana ya pension hapa kwetu, Huo mfumo wa ma DC au RC ni ishu ya Wataalamu tu kuamua, wao wanalipwa kwa Mara moja wanaita "Gratuity "

Kikubwa ni kuelimisha Raia mifumo iliyopo halafu tuchague
Watu wanaelewa haya mambo
Usitake kuwafanya watanzania wajinga!!

Huwezi implement hiyo sheria ili hali Life expectancy ya nchi yako ni miaka 45 hadi 50. Hiyo 60 ni ya kupika tu. Haya tu assume ni 60! Mtu ana staafu na 55 au 60. Una mlipa 25% na 75% ana dhulumiwa akifa na 62 yrs.

Kabla hujapongeza huu mfumo angalia na life expectancy ktk nchi husika.

Nchi kama Germany, Japan, UK mtu kuishi 89 yrs ni kawaida sn. Hivyo hii sheria kwao ni sawa. Kwa Tz uki ishi 70 tu una pongezwa kana kamwamba kwa sasa 70 ni maajabu tofauti na mababu zetu wa zamani.

Sheria iendane na LIFE EXPECTANCY ya nchi husika.

Mm napendekeza mtu apewe 60% afu 40% ndio alipwe kidogo kidogo hata kwa miaka 10.

Wazungu wanalipa hivyo kwasababu ya High Life Expectancy yao. Tusipende ku copy na ku paste kila kitu ulaya (sheria) bila ya kuangalia mazingira yako.
 
Kwa hiyo mbunge, DC, rc wanajua kutunza pesa kuliko mfanyakazi ndiyo maana wanapewa zao zote.

Sema serikali imekula pesa za mifuko iko hoi hiyo ni njia ya kujikoa na aibu.

"Gratuity" sio "pension"
 
Mzee huwezi kuniletea mambo ya elimu kwenye pesa zangu tena watch yo mouth,nimemaliza kazi yako nipe changu nikafie mbele kwanini nianze tena kiguu na njia kwenda kudai pension yangu hali yakuwa mimi siyo muajiriwa wako tena?

Mnawaza kwa kutumia viungo gani vya miili yenu ninyi???Hizo sheria wenzetu wenye akili timamu wameweza kuzi-maintain kutokana na unakuta mtu akipewa mf hiyo 25% yake anaweza kwenda kuanzisha hata mradi sasa bongo unakuta hela yenyewe 17.2mill akipewa 25% akilipa tu nauli ya daladala hata genge hatokaa afungue.
Unaongea kwa hisia! Hii inaonyesha huu mfumo umelenga kututawala. Mtu nimestaafu, siyo mtumishi tena halafu nimfatefate aliyekuwa mwajili wangu nimlilie anipe Ela ambayo yangu kaishikilia kama yake ilhali mimi siyo mfanyakazi wake!

Ujinga huu tusiutetee kwa kutumia "usomi."
 
Kiongozi ndio maana nimekuambia kuna aina nyingi za kuchangia, Elimu ni ndogo sana ya pension hapa kwetu, Huo mfumo wa ma DC au RC ni ishu ya Wataalamu tu kuamua, wao wanalipwa kwa Mara moja wanaita "Gratuity "

Kikubwa ni kuelimisha Raia mifumo iliyopo halafu tuchague
Yaani huyo mshikaji Mimi sijamuelewa kabisa au anataka cheo nini , ya nini mmpangie MTU pesa yake, naisi waliopitisha sheria hii hawana nia nzuri na Rais JWT tutachukua nchi
 
Wewe na waliokutuma ndio hamjui maana ya pensheni.

Hivi kama kigezo chenu cha pensheni ni gharama za maisha ya mstaafu mbona hamtumii vigezo hivyo kwa kima cha chini cha mshahara? Yaani mnamthamini mtu akisha staafu!

Nani kawaambieni lifespan ya wabongoland imeongezeka?

Iliongezeka vipi wakati mishahara haiongezeki, gharama za maisha zinapanda?

Halafu mmesema tusihoji takwimu!
Utamfundishaje mstaafu jinsi ya kutumia mafao yake kama wewe mwenyewe hujayaonja machungu yake?
Hawa "wachambuzi" ni WAJINGA wakubwa! Hawajui wafanyacho! Waswahili tulishasema kitambo kuwa: JAMBO USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA GIZA, ila hawa watoto wenye mchanganyiko wa shahawa za wazungu wanajifanya wana akili za kujua hatari za pension bila hata kuwa nazo! Wanaboa sana
 
Kusema mtu ataishi miaka mingi hivyo atalipwa muda mrefu zaidi ni ujuha uliopitiliza.Kanuni zinasema ni kwa miaka kumi na mbili tuu,je akiishi zaidi ya hapo?
 
Ndiyo maana mkienda kugombea ubunge vijijini wananchi hawawaelewi wanawapiga chini, mnazani wananchi wajinga kumbe nyinyi ndiyo wasomi wajinga wa Tz. Huwa mnafikiri kutoa definition ya terms ndiyo kuelewa. Natumai neno ujinga sio dhambi especially ukimwita mjinga mjinga.

Nani wakuwafanya wananchi/wafanyakazi waijue hiyo sheria mpya kama sio serikali? Hivi sasa hakuna mijadala, hakuna makongamano, media zote zinazuwiwa kufanya mijadala hata bunge lenye halionyeshwi mubashara kwa sababu ya neno uchochezi, unategemea mwananchi aote?. Ok anaweza ona kwenye tovuti za sirikali je, kusoma ndiyo kuelewa? Hata sehemu ya kazi/ofisini ukionekana unauliza au fafanua hii sheria mpya ya mafao unaonekana mchochezi!

Hivi unaweza kumlaumu mfanyakazi anaelipwa mshahara wa laki 4 kwa mwezi ameshindwa kujiandalia maisha ya uzeeni kwa sababu ya kuvuta sigara na matumizi mabaya ya pesa!!! Unahisi mbunge au waziri mwenye magari, majumba na maisha ma zuri ndiyo mwenye akili na matumizi mazuri kuliko mwalim?

Wako watanzania wengi sana hawafanyi kazi ya kuajiriwa na wanaishi na serikali haiwapi pension ya uzeeni, wanaishije wanakufa mapema au la hakuna anaejua, hivyo hata huyu mfanyakazi anaweza kulipwa mafao yake yote akafe kesho ni juu yake.

Swali la msingi kwanini sasa, mbona kulipokuwa na mifuko mingi wastaafu walikuwa wanalipwa kiinua mgongo kwa wakati, wastaafu walilipwa pension, baadhi ya mifuko ilikuwa inawakopesha wanachama wake kwa riba nafuu , kwanini sasa hii mifuko inashindwa kulipa?. Sisi wananchi tusiosoma na tusiojua hii sheria mpya tunahisi hii 8 T iliyokopwa na serikali kutoka kwa mifuko ya hifadhi ndiyo chanzo cha hayo yote.
 
Back
Top Bottom