Madhara ya kusoma Tanzania Mtu akishindwa kujibu hoja huanza kukasirika na kutukana
Serikali haijaanzisha hii mifuko kujaza watu pesa duniani kote, Ipo kutoa Kinga tu
Tatizo hamjasoma hiyo sheria, Pia hamfahamu maana ya Pension
Pension unapewa kwa Kanuni na mahesabu maalum
Serikali kwa Sasa imekuja na Kanuni muafaka wameondokana na Kila mfuko kujifanyia lake
Am a qualified Engineer niliyepata Elimu bora ya enzi ya Mwalimu Kambarage Nikianzia Ifunda Tech Sec.School miaka 1983. Sina shida kabisa ya maisha. Lakini haiondoki haki yangu ya kutoshabikia ujinga wa maamuzi yenu kwa haki za Watanzania.Madhara ya kusubiri serikali iwaletee maendeleo kwenye majumba yenu ndio haya mnalilia Bila kuhoji faida zake, soma hitimisho la uzi
Pole wewe. Kwanza kwa kudhani naongelea kwa akili ya darasani tu. Nimekuambia source ili ukajisomee.Pole Sana Hizo habari za mwajiri kuchangia sijui 10 per na mwajiriwa 10 per au mwajiri 15 per na muajiriwa 5per ni Kanuni za mfuko husika, Hapa hatuongelei Mada hiyo, Hapa tunaongelea uelewa wa watanzania kuhusu Pension
Story za darasani sijui percent hizo hazituhusu au story Za sijui Nssf au Psssf hizo Kanuni anzisha uzi wako
Tatizo lenu hamjasoma hiyo sheria mnasubiri vipande vipande mtafuniwe
Rudi soma sheria yote na kikokotozi cha pension yaani Formula ya Sasa ikoje
Ahsante kiongozi kwa kuuliza na kuhoji
Kwenye hizi bima hasa ya NHIF kuna mambo watu hawaambiwi pia, Hii Bima ya NHIF kuna vitu "neno la kiswahili "not covered niseme haitoi Kinga kwa baadhi ya Magonjwa lakini watu hawajaambiwa mpaka yakukute,
Tunapojadili Mtu anachangia na serikali pia inachangia NHIF walichofanya ni kupunguza gharama yaani Cost sharing tu tofauti na zamani
Sababu ya serikali kufanya hivyo imekula fedha za mifuko ya hifadhi ya jamiiTatizo uelewa wako kuhusu Pension mdogo?
Unafahamu Kwanini wamefanya hivyo?
Punguza hasira, ukiwa na jazba mambo mengi utaona unaonewa wewe tu
Pension ina mambo mengi Sana
Inajenga vitega uchumi vya majengoSamahani Biashara ipi?
Kiongozi ndio maana nimekuambia kuna aina nyingi za kuchangia, Elimu ni ndogo sana ya pension hapa kwetu, Huo mfumo wa ma DC au RC ni ishu ya Wataalamu tu kuamua, wao wanalipwa kwa Mara moja wanaita "Gratuity "
Kikubwa ni kuelimisha Raia mifumo iliyopo halafu tuchague
Kumbe hata ulichopost hukijui... Ukiajiriwa serikalini Tz unaingizwa moja kwa moja NHIF sasa hapo mtu akitaka kujiunga na bima nyingine anafanyaje? Na kwa taarifa yako hizo bima nyingine km AAR serikali imeingiza makucha yake...Tembea uone Mkuu,
Huko Africa kusini hata mambo ya Afya mwajiri hayamuhusu ni wewe mwenyewe unatafuta Insurance upendayo unachangia
Hapa Tanzania uelewa ni mdogo Sana, Watu Kila kitu wanasubiri serikali
Achana na mambo ya serikali utakufa maskini Jifunze
ukisoma makala ya mleta uzi inaonyesha kabisa kuwa kuishi miaka mingi kwa mstaafu ni kikwazo na tatizo kwao hao watu wa mifuko ya pensheni,wanapendelea wastaafu wafe mapema.Kuna uwezekano mkubwa wastaafu watakaoanza na sheria hii wakafa mapema kutokana na msongo wa mawazo.
Kwani kisaikolojia walishajiandaa kustaafu na kanuni za kikokotozi cha awali lakini hii imekuja pasipo kutarajia na tayari mda wa kujipanga kimaisha uko ukingoni kama hakujipanga akitegemea pensheni.
Ukitaka kujua hali ikoje, jaribu kuvaa viatu vya wahusika.
Nadhani lengo la serikali ni kutaka hela hii ibaki kwenye mikono yao ili waendelee kuiwekeza kwenye shughuli za maendeleo. Nia ni nzuri lakini sasa inawaumiza wazee hawa. Siilaumu sana serikali lakini nawahurumia sana hawa walioguswa moja kwa moja katika hili pengine kadiri mda utakavyoenda watumishi watajipanga kisaikolojia kuikubali hali hii maana saivi wengi bado wanashangaa hawaamini amini kama ndio imekuwa vile.
Watumishi pigeni moyo konde wala msihuzunike sana badala yake badilisheni mitazamo na mambo yataenda vizuri tu.