Watanzania walioishabikia kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa Kaizer Chief wamekosa uzalendo

Nikiwa Mtanzania Mzalendo nimeumia sana kuona baadhi ya wenzetu waliomua kwa makusudi kutusaliti kwa kuwapa support wageni

Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya Watanzania kuamua kuishabikia timu ya Kaizer Chief FC ya Afrika Kusini na kuibeza timu yetu ya Simba kufuatia kipigo cha goli 4

Ni kitendo kibaya cha kusikitisha, kutia huzuni na cha aibu kubwa kwa Watanzania hao walioamua kuisaliti nchi yao kwa kushabikia wageni huku wakitambua Simba inasimama kwa niaba yetu sote

Kushindwa kwa Simba ni kushindwa kwa Tanzania

Mafanikio ya Simba ndiyo mafanikio ya Tanzania

Ni msiba wetu sote kama Taifa hivyo tufarijiane na kutiana nguvu wakati huu wa huzuni huku tukijaribu kurekebisha mapungufu yetu madogo

Niombe Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litoe kauli ya kuwafariji WanaSimba na Watanzania kwa ujumla

Neno uzalendo lishaharibiwa
 
Simba Nguvu Moja 🤣
images (56).jpeg
 
Hakuna uzalendo katika suala hili, Mimi nishabiki wa Simba lakini ni ujinga eti kuwataka Yanga watushabikie wala mimi siwezi kuwaombea mazuri Yanga hakuna kitu hicho kila mtu apambane na hali yake. Mimi huwa nachukia mtu analeta hoja ya uzalendo au mchezaji au kocha anahojiwa kwanini mmefungwa kusema "tunashukuru Mungu tu hakupenda ila mechi ijayo tuombeeni" acheni kusingizia Mungu mambo ya kijinga sema tu tumezidiwa tutajipanga next game team haishindi kwa maombi.
 
Mm ni mzalendo sana ndio maana nilikuwa naomba simba lifungwa goli 7 kwani kwa mchezo ule wangeweza kufunga hata 10 - 0
 
Mashabiki wa Utopolo wamekosa uzalendo hawa,sijui wamekula maharage ya wapi hawaa!
 
Mkishida mnataka mshangile wenyewe mkifungwa mnataka tushangilie wote...!
===
Kweli jana uzalendo uliniingia hasa bao la nne lilipofungwa huku kaburu kocha wa Kaiza Chief akitucheka....! Sorry akiwacheka Simba. Nirikasirika!
 
Na mwaka huu mnalo Uzalendo huo vipi na wakati kila mtu ana uhuru wa kushangilia apendacho
 
Nyie mlituzomea wakati wa mechi na Namungo.mkasema ile ni mechi ya kina mama na kua tusubiri mechi ya wanaume saa moja.....sie tukasubiri game iliyofuata ya wanaume na jwa bahati nzuri matojeo yakawa yale na watu wakazimia mara mbili

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wahi hospital haraka sana nahisi unanyemelewa na mental illness aisee. Mafanikio ya Tanzania kivipi? Nyie si mnajua kutoa burudani kwa pira biriani au?
 
Yaani nishabikie hawa hawa wapinga Uhuru hawa




Waoshwe Tu mafuta tutawapaka na maseji wakizimia
 
Back
Top Bottom