Watanzania walioishabikia kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa Kaizer Chief wamekosa uzalendo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,694
Nikiwa Mtanzania Mzalendo nimeumia sana kuona baadhi ya wenzetu waliomua kwa makusudi kutusaliti kwa kuwapa support wageni

Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya Watanzania kuamua kuishabikia timu ya Kaizer Chief FC ya Afrika Kusini na kuibeza timu yetu ya Simba kufuatia kipigo cha goli 4

Ni kitendo kibaya cha kusikitisha, kutia huzuni na cha aibu kubwa kwa Watanzania hao walioamua kuisaliti nchi yao kwa kushabikia wageni huku wakitambua Simba inasimama kwa niaba yetu sote

Kushindwa kwa Simba ni kushindwa kwa Tanzania

Mafanikio ya Simba ndiyo mafanikio ya Tanzania

Ni msiba wetu sote kama Taifa hivyo tufarijiane na kutiana nguvu wakati huu wa huzuni huku tukijaribu kurekebisha mapungufu yetu madogo

Niombe Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litoe kauli ya kuwafariji WanaSimba na Watanzania kwa ujumla
 
Simba ya leo!😄😄😄
View attachment 1786303
20210515211437.jpg
 
Yaani many town leo imepoa kila sehemu, yaani isingekuwa Eid pili nadhani wake wenye waume wengi wangetoa ushuhuda kesho na Jumatatu 😁!.
 
Tatizo sio kukosa UZALENDO ,tatizo ni MANENO MACHAFU ya yule Msemaji wa Simba ,ameugeuza Utani wa Jadi kati ya Simba na Yanga kuwa Upinzani na Uadui ,hakika hasipo onywa mapema natabiri Jambo baya kutokea kwenye Soka la Tanzania hususani hizi Timu 2 ,Simba na Yanga.
 
Nikiwa Mtanzania Mzalendo nimeumia sana kuona baadhi ya wenzetu waliomua kwa makusudi kutusaliti kwa kuwapa support wageni

Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya Watanzania kuamua kuishabikia timu ya Kaizer Chief FC ya Afrika Kusini na kuibeza timu yetu ya Simba kufuatia kipigo cha goli 4

Ni kitendo kibaya cha kusikitisha, kutia huzuni na cha aibu kubwa kwa Watanzania hao walioamua kuisaliti nchi yao kwa kushabikia wageni huku wakitambua Simba inasimama kwa niaba yetu sote

Kushindwa kwa Simba ni kushindwa kwa Tanzania
Mafanikio ya Simba ndiyo mafanikio ya Tanzania

Ni msiba wetu sote kama Taifa hivyo tufarijiane na kutiana nguvu wakati huu wa huzuni huku tukijaribu kurekebisha mapungufu yetu madogo

Niombe Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litoe kauli ya kuwafariji WanaSimba na Watanzania kwa ujumla
Malipo ya dharau
 
Back
Top Bottom