100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 10,205
- 36,443
Kipindi Nchimbi anazungumzia suala la wananchi kupambania katiba mpya wadau wengi humu walidai ni tamthilia chama tawala kinafanya na EN ni muigizaji tu...
Wakasema wakitaka waamini kama kweli ana maanisha asemacho ajiuzulu...
Kama vile EN aliwasikia, kajiuzulu, wadau wamerudi tena povu likiwatoka kwanini amejiuzulu, kwanini asingekomaa hadi kieleweke... Kwanini ajiuzulu kiwepesi wepesi..
Wakati huo huo angeendelea kupambana akiwa kiongozi hao hao wangesema anafanya maigizo na lao ni moja na boss wake... kwa kweli kuwaelewa Watanzania ni kazi ngumu sana...
Ndio yale ya Polepole , anayeikosoa serikali akiwa nje ya nchi unasikia wakisema kwanini asije nchini kama ni mzalendo kweli... walipogundua ametekwa akiwa nchini hao hao wakasema kwanini aikosoe serikali akiwa nchini? Kwanini asingejificha nje ya nchi?
Sasa sijui tushike wapi?