Watanzania Waasia kwenye vyombo vya Usalama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania Waasia kwenye vyombo vya Usalama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 10, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kinachoonesha utii wa mtu kwa nchi yake kama utayari wake kufa kwa ajili ya nchi hiyo. Ni kipimo cha juu kabisa cha mapenzi ya mtu kwa nchi yake. Lakini pia kuitumikia nchi katika nafasi mbalimbali kunaonesha jinsi gani mtu anavyolipenda Taifa lake.

  Mojawapo ya vitu ambavyo havionekani sana katika Taifa letu ni Watanzania wenzetu wenye asili ya Asia (wahindi, Waarabu, n.k) kujiunga na vyombo vyetu vya usalama hasa majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama.

  Nikikumbuka vizuri baada ya uasi mwaka 1964 ni maafisa wachache wa kizungu ambao waliendelea na jeshi na ni mmoja ambaye aliendelea kuitumikia kwa muda mrefu tu. Sifahamu sasa hivi kama kuna maafisa wowote wa JWTZ ambao aidha wana asili ya Uhindi au Uarabuni.

  Kwa upande wa Polisi kumekuwepo na maafisa kadhaa wa Kihindi na wenye asili ya Uarabuni lakini nadhani sasa hivi wengi watakuwa wameshastaafu. Nafahamu wapo vijana wachache ambao waliingia huko (namkumbuka Bi. Khadija K. binti wa kiarabu aliyejiunga toka Tanga) na pia Insp. Khan ambao at the time nilikuwa nashangaa kweli kuwaona kwenye jeshi letu.

  Hata kwenye taasisi nyingine (ukiondoa za Kitaaluma) bado jamii hii ya Watanzania inakosekana sana. Sijui idadi yao kwenye TRA, Public service n.k

  Kwa upande wa Magereza ndiyo sijui kabisa kama kuna watanzania wenye asili ya nje ya bara letu ambao wanaitumikia nchi yao hivyo. Wakati ambao nakumbuka tuliweza kuwaona Wahindi na Waarabu wengi ni wakati wa JKT ule. Sijui katika JKT hiii ya kujitolea inakuwaje.

  BIla ya shaka unajiuliza "what is the point". Point yangu ni kuwa inaonekana aidha kwa makusudi au by default mchango wa Watanzania hawa unataka kuishia kwenye siasa na biashara au sekta binafsi na siyo kwenye utumishi wa umma.

  Nakabiliwa na maswali machache:

  a. Kwanini Watanzania wenye asili ya Uhindi au Uarabuni hawaingii kwenye vikosi vya usalama? Zamani nakumbuka tulikuwa tunawatania kuwa wao ni "watoto mayai" hawawezi kazi za shurba lakini nikagundua kuwa hata kule Uhindi na Uarabuni kuna majeshi na POlisi na wao wanapewa mafunzo ya kijeshi na kuhenyeka kama sisi. Hivyo suala la "umayai" halipo.

  b. Ni juhudi gani zinafanyika kurecruit Watanzania hawa hasa kutokana na ujuzi wao wa mambo ya biashara, utaalamu wa IT, n.k n.k na hivyo kuleta vipaji ambavyo vinahitajika sana kwenye vyombo vyetu hivi?

  c. NI kwa kiasi gani familia za ndugu zetu hawa zinawa encourage watoto wao kuitumikia nchi yao kwa zaidi ya siasa na biashara na kuingia kwenye utumishi wa umma. Watakuwa wanaendelea kutoa misaada tu mpaka lini.
   
 2. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  simple: Institutional racism.. (circumstancial rather than deliberate)
  Waarabu in most cases wako business oriented as well as wahindi. Family business in most cases, maduka etc. they hail from a class of traders and merchants rather than farmers.

  They, in all likelihood fail to see any merits of joining such forces because all they want is wealth and prosperity. I cant imagine that they are interested in honour, sijui defending their country etc.
  Its much easier to bribe the police when necessary, get rich and then become an MP by buying the votes... All the while, the paramount objective being to further their economic interests... very simple logic... but it works so i cant blame them.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  lakini hawa zaidi ni wazee wao; kizazi chao cha vijana hakina ile rebel spirit? Sidhani kama mtu ni mfanyabiashara basi watoto wake nao wanafuata njia hiyo hiyo. Yawezekana kuna vitu vingine mbalimbali vinavyochangia hili sidhani kama kutafuta utajiri tu inatosha kwa sababu utajiri ni mzuri na mtamu as long as you are free to enjoy it.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Nov 10, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Kwani idadi yao (Watanzania wenye asili ya Asia na Uarabuni) ki asilimia wako wangapi?
   
 5. Gosheni

  Gosheni Senior Member

  #5
  Nov 10, 2008
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 189
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 60
  Wanajua kwa hakika tokea ndani ya mioyo yao kuwa wao si watanzania, na hata kama tunajifariji na kuwaona kama watanzania wenzetu, ndani ya miyo yao wanajua kabisa sisi si watanzania, ndio mana hawana uchungu na nchi, utawakuta katika ubadhilifu mkubwa wowote wa nchi hii wao wamo. kwa ujumla wanajua hii sio nchi yao, nakumbuka kuna muhindi mmoja nilikuwa naye chuo kikuu, cha ajabu kwa huyu muhindi alikuwa hafamu kiswahili vizuri huku akiwa amezaliwa tanzania na kusomea tanzania hadi kufikia level ya chuo kikuu, ila kiswahili hafahamu vizuri inavyotakiwa lakini muulize kuhusu kihindi ambapo huko india kwenyewe anakusikai tu kwa jina, haja wahi kufika, utamkuta alivyo mfasaha katika lugha hiyo kama amekuja jana toka india, kumbe hata kufika huko india hajawahi kufika

  Kuna mambo mengi ambayo yanatambulisha utaifa wa mtu, moja wapo ni lugha. hawajamaa wanatuthibitshia jinsi wanavyo tumia lugha ya taifa letu, namna wanavyo wangalia watanzania weusi katika makampuni yao, namna wanavyo jitenga mahali pa kuishi, yote hii inaashilia wao si wenzetu.

  Kurudi kwenye mada ya swali, wata kuwaje kwenye usalama wa taifa ambapo wanahakika wwanachokwenda kulinda sio chao? kumbuka usalama wa taifa unamaanisha kujitolea maisha(uhai). inapotekea majambazi na kwenda kupambana nao, hii inamaanisha kuwa tayari kufa wakati wowote kwa ajili ya taifa lako, ukiwa jeshini, inapotokea vita n.k. Kwa kifupi hawajamaa sio watanzania, na wao hilo wanatueleza kwa matendo yao, ila inapokuja swala la maslahi ya fedha basi sisi ni watanzania, kuna mengi yanayoonyesha hawa jamaa si wenzetu
   
 6. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  as you say.. as long as you are free. Nimesoma shule ya wahindi.. fortunately maana it gave me insight into their world maana i have many friends wahindi. Their institution of the family is stronger than the Black Tanzanian institution. For one, all decisions are centralized. So what you will do is a family decision since income generation is something that affects every one. Mhindi lazima mtoto wake awe dukani at least a few times a week akiwa bado anasoma, at the same time watoto wao wanakuwa taught how the 'waswahili' as they call us, hatuko organized and how corruptable we are.

  Wazazi wao wana serious control over the family and the decisions that their children make. Lakini i've seen it time and time again hakuna rebellion kabisa, and in the odd occasion of such a thing.. mtoto atafungua duka lake mwenyewe au garage, au spare parts dealer au atakuwa transporter kama ni muarabu.. but never join the army.lol Mambo ya rebellion that is white kids syndrome ambayo wahindi na waarab hawana.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni kama asilimia moja hivi..
   
 8. kamonga

  kamonga Senior Member

  #8
  Nov 10, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kua they emerge from merchants and traders backgrounds ila kuna yale mambo ya.....kutothamini kazi community jobs.
  Ni kuona they are not part of it.... sababu they are a number of Indians and arabs who would rather squeeze four or more trying to sell in one family shop or rather playing bao or crowded in a single petrol station just so they are not employed as public workers and stuff.
  kwa kifupi ni kama hawataki kutumwa tumwa (umwinyi)
  Tathmini yangu.....
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kwanini wakurya wanaingia kwa wingi kwenye majeshi yetu?wangekwa wengi mngeanza kupiga filimbi ooh mbona IGP muhindi?!....... "mbona bosi wa usalama wa taifa muarabu tena muislamu?......!!!
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Nov 10, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Duh! kumbe wako wachache hivyo....so what is the fuss all about?
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mabadiliko ya vizazi vya sasanadhani inatarajia jinsi wanavyolelewa na kukuzwa. Hao vijana tunaotarajia wa-rebel wanakuzwa katika utamaduni wa kuthamini biashara na kutengeneza utajiri, na ninadhani ndio maana bado hawajapata mwamko wa kujiunga na majeshi.
  Ukiangalia hata katika maisha ya kawaida mitaani, malezi na makuzi (yale ya ndani) ya hawa wenye asili ya nje, ni tofauti sana na ya 'waswahili' hata kama watakuwa wanachanganyika katika mambo mengi
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Nov 10, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Heheheheee...hii thread taratibu itaanza kuchukua detour na kwenda kwenye udini na ukabila.....mwishowe tutaanza kuuliza kwa nini Wakristo wengi wako kwenye ngazi fulani za kijeshi...halafu tutauliza kwa nini Walutheri wengi wanashikilia nafasi flani....mwishowe tutagawanyika kati ya Waislamu na Wakristo.....
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  kuwa polisi sidhani kama inaonekana "dili" Tanzania, na majority ya Waasia wana much better options.
   
 14. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #14
  Nov 10, 2008
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kama kuna mhindi ambae kaajiriwa bongo, kama ni serikalini atakuwa anafanya kazi benki, kwenye private sector atakuwa anafanya kazi kiwandani tena cha mhindi mwenzake au hotelini tena hotel ya mhindi mwenzake!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lakini huko India, Pakistani, Indonesia n.k wahindi wanafanya kazi za usalama pia. Na wako tayari kufia nchi zao na kujitoa mhanga kulinda taifa lao. Yawezekana kuwa ni kweli bado hawajakubali kuwa wao ni Watanzania hasa au ni watanzania as long as things are going good for them?

  Je yawezekana ni kwa sababu hawaoni sababu ya kushiriki katika usalama wa Taifa namna hii maana naamini tunaweza kuwa na maagenti wazuri tu katika TISS, wapelelezi n.k na tukaweza kufanikiwa katika mapambano ya vita vya ufisadi?
   
 16. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu ku-imagine mhindi amevaa white suit ya traffic police ananisimamisha pale Boma ng'ombe anadai hela ya soda sijui chilli curry? Hiyo picha sijaipenda, makonda watawatesa sana lakini....
   
 17. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Simple: Money and Power (they don't care about respect..!!).

  Sasa hebu nielimishe ni vipi utaweza kufanikisha hayo kwa kuwa Polisi, askiri Magereza au Nesi pale Muhimbili??

  Kuangalia hawa wenzetu kwa nini hawako kwenye public service ni kwenda mbali mno. Mimi napendekeza tuanzi huku chini...jinsi wanavyolelewa na kuelimishwa kadri hadi wanavyokuwa watu wazima.

  Malezi: Mpaka miaka ya 1990 kwenye mashule ya Primary kama Forodhani, Bunge, Olympio, Mtendeni, Kisutu n.k ulikuwa unakuta watoto wanafunzi wenye asili ya kiarabu na asia wengi tu. Kwenye Sekondari kama Shabban Robert, Mzizima, Tambaza, Al Muntazir n.k pia ulikuwa unawakuta. Sasa tujiulize iwapo kwenye vyuo vikuu pia walikuwa wanakuwepo? Jibu ni kwamba wanakuwepo wachache sana...sijawahi kufanya utafiti wa makini lakini naamini wengi wao wanasoma elimu ya juu nje ya Tanzania. Ninaamini pia huwa wanabakia huko kwa miaka mingi. Iwapo hali ingekuwa tofauti basi leo hii tungekuwa na majirani wahindi au waarabu wengi tu kule Sinza, Kijitonyama, Mbagala, Mbezi Temboni, Tabata n.k kwa sababu zile nyumba za msajili katikati ya jiji zisingewatosha...!!
   
 18. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi siamini hoja yako hapa.. Inamaana hujui kabisa kuwa hawa watu hawajichukulii kama ni watanzania. They are only here as far as economic opportunities allow.. ndio maana wengi wanauza drugs alafu wanahamia Canada and UK.(wahindi) waarabu wanaishi hapa lakini wanandugu zao Oman, Yemen and UAE. They dont see themselves as watanzania... Mimi rafiki zangu wote nnao wajua wanasema wao ni waarab na waismailia na hindus and shia'ithnashri na sunni they never and i mean EVER refer to themselves as WATANZANIA. hilo halipo akilini.. wanaishi tanzania lakini sio watanzania (they just dont see it like that).

  I happened to date a few Arab girls a few years ago.. yani ilibidi iwe in secrecy, tena gari langu at the time ilibidi liwe tinted all windows mpaka wind screen kwachini kidogo so that no arab sees what they are duin... maana wanajuana karibia wote. They see us as a lower class.. and its true they resent kuwa employed by waswahili... tena waarabu ndio kabisa...

  Wahindi pia its a similar thing... wanamtazamo fulani kuhusu watu weusi.. wako tayari kudeal na wewe kama Govt official au kama mfanya biashara lakini sio eti umuajiri yeye au mwanae au serikali imuajiri (basically nothing that has something to do with being under the supervision of someone with more melanin then them..lol)
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Nov 10, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Pia yawezekana wanajisikia hivyo kwa vile na sisi tunawaita "wahindi" na "waarabu".....jiweke katika hali/ nafasi yao labda unaweza kuona au kuelewa ni kwa nini huwaoni kwa wingi katika hizo nyanja ulizozitaja....
   
 20. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Wako teyari kufia nchi zao ambazo zipo kwenye vita or at least in some state of chaos, think pakistan/India!
  Tanzania tuko peace, ukijiunga jeshi sana sana utaenda kukaa kambi, hakuna ile motiivational force.
  Secondly vitengo vingi vya usalama haviheshimiki TZ think about the first thing that comes to mind when you think of the traffic/Police? CORRUPTION!! Sijui kama nimewahi kusikia mtanzania amejiunga Polisi ili alinde nchi yake, maybe wapo ila slim minority.
   
Loading...