Watanzania vs waganda & wakenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania vs waganda & wakenya

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by MwanaFalsafa1, Jun 2, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na Mwandishi Wetu, Iringa

  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, amewataka wasomi nchini kujiamini na kujiandaa kufanya kazi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

  Dk. Kamala alitoa kauli hiyo juzi katika Chuo Kikuu cha Tumaini mjini Iringa, wakati akizindua maonyesho ya Siku ya Waajiri Kukutana na Wahitimu Tarajiwa (Careers Day).

  Alisema, mwakani milango ya soko la pamoja katika EAC itafunguliwa, hivyo Watanzania wanapaswa kujiandaa kwa ushindani.

  Alisema, Watanzania wanayo maarifa ya kutosha, hivyo hawapaswi kuwa na wasiwasi juu ya kinachodaiwa kuwa Wakenya wanafahamu Kiingereza vyema kuliko Watanzania.

  "Nawahakikishia kuwa Wakenya wanazungumza Kiingereza cha kienyeji, lakini sisi Watanzania tunazungumza Kiingereza cha Oxford (Uingereza)," alisema Dk. Kamala na kushangiliwa.

  Alisisitiza kuwa, Watanzania wanapaswa kujifunza somo la Maendeleo ya Jamii (Development Studies), Mawasiliano ya Umma (Communication Skills), Maadili (Ethics) na Technolojia ya Mawasiliano ya Umma (ICT) kwa nia ya kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kiushindani.

  Alionya kuwa, wakati umefika kwa Watanzania kuanza kujifunza Kifaransa, kwani soko likifunguliwa nchi za Rwanda na Burundi zinazungumza Kifaransa, lakini zinajifunza Kiingereza kwa kasi kubwa, hivyo kama Watanzania watakuwa hawajui Kifaransa, itawawia vigumu kufanya kazi katika nchi hizo.

  Waziri huyo alisema, faida za kuingia katika soko la Afrika Mashariki ni nyingi, kwani ukubwa wa soko utapanuka na gharama za uzalisjaji zinazidi kupungua.

  Alitoa mfano wa mauzo ya Tanzania kwenda Kenya kuwa, tangu ushuru wa pamoja uanze kutekelezwa 2007, Tanzania imeongeza mauzo nchini humo kutoka wastani wa Sh bilioni 94.5 kufikia Sh bilioni 275.5.

  Dk. Kamala alizitaka nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuruhusu wananchi wa nchi hizo kufanya kazi katika nchi zao, kwa maelezo kuwa Tanzania imeshaonyesha njia.

  "Leo hii Tanzania inaajiri wana-Afrika Mashariki wengi kuliko nchi nyingine yoyote, wapo kwenye hoteli na kila mahala," alisema.

  Aliongeza kuwa serikali ya Tanzania imejenga misingi mizuri ya uchumi, na hadi sasa imedhibti mfumko wa bei kuliko nchi zote wanachama wa EAC.

  "Mfumko wa beki kwa Kenya ni asilimia 26, Rwanda ni asilimi 19, Burundi ni asilimia 19, Uganda ni asilimia 13.4 na Tanzania ni asilimia 13.

  Hii inamaanisha kwamba kama kuna mtu anataka kuwekeza dola zake, atanona ni hasara kuwekeza katika hizi nchi nyingine, hivyo atakimbilia Tanzania na ndivyo inavyokuwa," alisema na kushangiliwa.

  Chuo Kikuu cha Tumaini kimekuwa cha kwanza kukutanisha waajiri na wahitimu tarajiwa, suala ambalo ni kawaida kwa nchi za Ulaya.  I agree with some of the things this guy has said. Tanzanians shouldn't be scared to compete and have more confidence with themselves. Some parts I don't agree with is e.g Tanzanians(I'm assuming he meant the majority) speak English from Oxford. Smatta my Kenyan bro, I am more curious to hear your opinions on this. I'm sure this is one piece both me and you will agree upon.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Na Political Science
   
 3. Offish

  Offish Senior Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakaubaliana naye kuhusu Kiingereza kama Wakenya wanavyokubaliana kuwa ati Watanzania ni wavivu! Ukimkuta Mtanzania anaongea Kiingereza huwa kimenyooka kuliko jirani zetu ambao wengi wanaijua lugha hiyo laikin wameelemewa na lafudhi za lugha zao. 'Generalisation' hata hivyo sio kigezo kizuri kufanyia maamuzi.

  Masomo yote aliyoyataja ni muhimu kuliko Watanzania wengi wanavyodanganyika kuwa ati Kiingereza kikiendelea kuwa lugha ya kufundishia mashuleni na vyuoni kitawasaidia sana Watanzania katika anga za kimataifa. Ujuzi ndio utakaotufikisha hapo na ikumbukwe kuwa ujuzi hauna lugha, angalia Wajapani, Wajerumani na Wachina walipofikia ingawa wengi wao hawazungumzi Kiingereza...
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nakubaliana na maoni yakoo..

  ni kweli ujuzi hauna lugha ila muhimu ni kuelewa kuelezea kile unachokifahamu regardless ya lughaa unayotumiaa..KUELEWEKA NI MUHIMU.

  Waziri kanigusa kwa aina ya masomo alivyotaja hasa DS kwani maana hapo ni pana zaidi kuielewa jamii na mambo yake. hapa ndo current affairs, socio economic iisues, geo and local politics, ICT na mengineyoo ni muhimu sanaa..

  naomba sasa mtaala wetu uboreshwe ila hayo masomo yawe more visible na sio add on subjects au topics...
  Tutaaanza na wakufunzi au tuingie tuuu kimkandamkandaaa????

  nawasilishaa.
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nakubaliana na maoni yakoo..

  ni kweli ujuzi hauna lugha ila muhimu ni kuelewa kuelezea kile unachokifahamu regardless ya lughaa unayotumiaa..KUELEWEKA NI MUHIMU.

  Waziri kanigusa kwa aina ya masomo alivyotaja hasa DS kwani maana hapo ni pana zaidi kuielewa jamii na mambo yake. hapa ndo current affairs, socio economic iisues, geo and local politics, ICT na mengineyoo ni muhimu sanaa..

  naomba sasa mtaala wetu uboreshwe ila hayo masomo yawe more visible na sio add on subjects au topics...
  Tutaaanza na wakufunzi au tuingie tuuu kimkandamkandaaa????

  nawasilishaa.
   
 6. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  English, not being the first language to most of us, to some extent, can bring certain issues to the speaker. Kenyans speak English, and most of them especially outside the office setting prefer speaking slang(mixing English with swahili), but officially we speak the queens language eloquently depending with the importance of the matter of discussion. I have heard Tanzanians speak gooood English, and some bad.. the same case applies here at home, where some speak good English while others kill the queens language.

  I think that the honourable Minister was right when he said that there is no need to be afraid of Kenyans, however he messed when he said that we speak bad English, just liike any African country you cant find majority of the population speaking impecable English, lazima kuna adhari ya lugha ya mama kidogo. We should love competition, it can spring us to heights we never thought we could reach .

  ps
  We should all try to promote our Kiswahili and indeginous languages. The Chinese, Arabs e.t.c dont emphasise on English, they speak there own language and that has seen them curtupult to places we only dream of.
   
 7. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  wajapani, wachina, wajerumani, wafaransa nk ambao wanatumia lugha zao
  wanajitosheleza kwa kiasi kikubwa kwa utaalamu (yaani wale ambao tayari wamepata huo utaalamu wanaandika yale waliyofuzu kwa lugha zao).

  tatizo tulilokuwa nalo hapa kwetu wataalamu wetu hawayaweki yale waliyokwishafuzu katika maandishi ya kiswahili. hivyo siku zote kwa kiasi kikubwa tunajikuta ni muhimu ufahamu lugha ya wageni ili uwe mtaalamu.

  wasomi wetu hibu tuwekeeni utaalamu wenu katika kiswahili ili lugha hii iweze
  kujitosheleza katika kupata wataalamu
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kwani Watz wanawaogopa Wakenya??
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Hayo masomo aliyosema tanasaidia lakini angesisitiza zaidi sayansi na teknologia. Masomo ya hisabati, fizikia, biologia, kemia, ni muhimi

  by the way ameshamaliza PhD yake ya Pili?
   
 10. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  ...waahhh!!!...No comment.
   
 11. s

  susu Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nikiwa kama mtanzania niliyesoma kenya kabla ya kuhamia hapa uingereza napenda kuchangia hoja hii kama ifuatavyo.Elimu ya kenya iko juu ikilinganishwa na ya kwetu.Na uzoefu wao wa kingereza unawapa wao uwezo wa kujieleza kwa ujasiri na kuijamini .Huyu waziri alifaa awaeleze wanainchi waliandaa vipi Taifa kabla ya huwo muungano Afrika mashariki.Watanzania sio wanaogopa bali wanashuhudia kazi zao zinavyochukuilwa .hata kazi za waosha vyombo mahotelini zisizo hitaji kingereza zinachukuliwa na wakenya na waganda.Huyu waziri aituzingue kwa kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Watanzania wengi tu ni wasomi hawana kazi na hata wakienda huko kenya na Uganda hawapewi kazi,Kwa sababu wanalinda masilahi yao.serikali inatakiwa iiangalie swala hili.i pitishwe sheria kazi kwa watanzaia kwanza.wageni wapewe endapo tu hakuna mtanzania anayeweza kufanya kazi hiyo.
  Asanteni,
  Susu,
  London-UK
   
 12. K

  Kimwe Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Suala hapa si kuwaogopa kwamba wanatisha kielimu na kiujuzi la, jamaaa wamechoka tu.Tunawaogopa kiukabila maana unapofungua milango ya ushindani maanake nasi twende kwao kusaka kazi kitu ambacho kitakua ni njozi hawa jamaa kukupa ajira.

  Kuna kipindi serikali ya Botswana ilitangaza ajira za ualimu na walihitaji walimu wa sayansi toka Tanzania na kosa likawa kuipa kampuni ya Kenya kufanya recruitment.Watanzania wengi tena wenye elimu nzuri tu hata hawakujibiwa nini kupata hata interview.

  Hivyo kufungua milango na watu ambao hawako fair ni kujidanganya!
   
 13. K

  Koba JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...blah blah blah blah blah blah...baa ba aaba ababababaaa!
   
 14. H

  Hondo Member

  #14
  Jun 3, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa anayeitwa Kamala nimemuelewa kidogo pale aliposema watanzania wanatakiwa kujiamini hiyo nampa 100% ni kweli hilo ndilo tatizo kubwa la watanzania. Tumeshindwa kujiamini katika kila kitu kwasababu msingi mibovu tuliyo nayo .Pia wengi wetu tumendekeza ubishoo, ulimbwete na Usanii hatakama tumepata elimu nzuri .Hatuko serious na mambo yetu .Wakenya wako serious na ni wachapa kazi kwahiyo kwenye soko lolote bado wanaweza kutuzidi kwani ukiwaambia kudeliver wanaweza bila matatizo ndio maana bado wanapendwa na waajiri.
  Ili tuweze kuingia kwenye soko lazima tuache ubabaishaji.
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaye waogopa wakenya au challenge kwa jumla, tatizo letu ni kuwa na viongozi wabovu ambao wana kutupa sehemu huna nyenzo wakati mwenzako anakianzio, hivyo huwezi kushindana nae, mfano elimu unaweza kuwa nayo lakini hakuna mikopo kama kianzio cha maisha au vitu vya msingi katika maisha, hata mishahara wanayo lipwa watanzania wengi ni midogo kulinganisha na mkenya , kwa nafasi hiyo hiyo, sasa mtu wanamna hiyo anaweza kuwa na confidence zaidi na utulivu wa kiakili katika kutekeleza majukumu yake, lakini mtanzania anayelipwa kiduchu anafikiria namna gani atapata mlo wake au atamsaidia namna gani wazazi wake au ndugu etc etc. tukiacha utekelezaji mbovu wa sera zetu , hakuna kipingamizi, mfano aina ya walimu wengi hapa kwetu ni chini ya kiwango , hivyo hata wanafunzi matokeo ni mabaya, mtu akitaka kujenga nyumba hakuna mikopo hivyo mpaka ukaibe, uchumi wetu ume duma hivyo hata hizo nafasi za kazi ni chache, ukipata hiyo kazi hakuna professionalism katika mashirika yetu, mtu moja anahodhi karibu kila kitu unabaki kama robot ya majamaa, matokeo yake kila kitu kinaduma, mfano mwingine hapa miaka ya karibuni ntulibinafsisha mashirika ya umma, badala ya kuwauzia watu wenye uwezo tukawauzia wasio na uwezo matokeo yake ni kuduma kwa uchumi. in short misingi yetu ya kiuchumi haiwasaidi wananchi kwa hiyo integration. labda ya kuwa manamba au wasindikizaji
   
 16. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Sie hatujachoka ustadh........
  This one had me laughing, At a time in my life, I worked at KEMRi (Kenya Medical Research Inst.) in Kilifi, Coast province. We had about four young Tanzanian doctors, and a nutritional officer, a very hard working and intelligent research team.. what am trying to insinuate is that, just as some Kenyans are employed in Bongo because of their qualification, the same applies to Kenya, if you are qualified you can get the job (but priority will be given to the Kenyan national if the job is in Kenya, and I know the same case applies to Tanzania).
   
 17. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kwanini Wakenya na Waganda wanawaoutshine watanzania katika nafasi nzuri za kazi hasa katika mashirika ya kimataifa hata ndani ya Tanzania.

  Nafahamu Kugha ya Kiingereza ni moja ya sababu, naomba tujadili sababu nyingine zaidi, na nini watanzania wafanye ili kuwa bora zaidi.

  Karibuni
   
 18. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  wewe ni mkenya au mganda,....
   
 19. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mganda au Mkenya akisha kaa kwenye ofisi moja, ikitokea nafasi huwa anawambia watu wa kwao kwanza kabla tangazo halijatoka. Hivyo applicants wengi wanakuwa waganda au wakenya. Mmbongo akikaa sehemu nzuri hataki kuwaita wabongo wenzake kwasababu watafaidika halafu atashindwa kuwatambia baadaye.
   
 20. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wanabahati nzuri
   
Loading...