Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,533
- 4,317
Kwa umoja wetu, Tukiamini sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, Na kamwe watawala hawajawahi kuishinda nguvu ya umoja wa umma ambao ndiyo sisi watanzania, Tuungane kukemea, Kupinga na kuchukua hatua ikibidi kuwalazimisha kung'atuka au kutokurudia makosa kuwarudisha katika viti vyao wakati wa uchaguzi ili kama taifa tuweze kusonga mbele.
1. Viongozi wanaosisitiza na kutamka hadharani kwamba kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake. Hii ni hatari na inapelekea viongozi kujihalalishia vitendo vya wizi wa mali ya umma
2. Viongozi wanaoendekeza ziara zisizokuwa na tija wala zisizobeba vipaumbele vya watanzania ambao wengi wanahitaji huduma za msingi za afya, maji, elimu, miundombinu n.k na sio maswala mengine yasiyo vipaumbele kwao. Ziara hizo pamoja na delegation zake zinaigharimu nchi kiwango kikubwa cha fedha zinazotokana na kodi zao.
3.Viongozi wasiojishusha na kufika chini kabisa kujua uhalisia wa maisha ya watanzania walio wengi na ikibidi kushiriki katika kutatua kero zao.
4.Viongozi wasio na uchungu wa mali na rasilimali za watanzania.Viongozi walio tayari kufukuza wamaasai katika makazi yao ya asili kwa ushawishi wa mwekezaji. Kiongozi ambaye yupo tayari kutoa bandari zetu ambazo tumeshagharamikia kwa kiasi kikubwa kwa masharti ambayo si rafiki, Ni Kiongozi wa kupingwa kwa nguvu zote.
5.Kukosa maono, kushindwa kuanzisha wala kusimamia miradi mikubwa na ya kimkakati.
Hayo ni machache, Nadhani Kiongozi wa aina hii hatufai hata kidogo!