Watanzania tuna utamaduni gani,mpaka hatuna uwezo wa kujitetea?

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Naandika nikiwa na hasira sana juu ya jinsi mimi na watanzania wenzangu tunavyoishi katika mazingira yetu ya kila siku.
Unakuta mtu naporwa simu, au naonewa lakini watu pembeni wamekaa tu hawashughuliki kumsaidia. Raia wote wanaacha jukumu la kujilinda liwe la polisi tu kana kwamba wao hawahitajiki kufanya juhudi zozote.
Kwenye kura zitaibiwa, patafanywa figisu za wazi lakini watu wametulia tu. Kila mtu anasubiri mwenzake ndio aanze kudai haki na akianza wanamwangalia tu kuwa anajifanya mjuaji watamuunga mkono tu kama kuna dalili za yeye kwenda kufanikiwa.
Kuna ishu kama hii ya panya road, inakuwaje watu mia moja mtaa unafungwa na watu 10? Polisi hata watuahidi vipi hawawezi kuwa kila eneo kwa wakati husika. Nchi zilizoendelea pamoja na kuwa na mifumo mizuri ya ulinzi lakini bado raia wanaruhusiwa kumiliki silaha ili kujitetea. Cha ajabu utakuta mtanzania hana hata panga ndani la kujilinda siku pakitokea uvamizi, ukimuuliza atakuambia kazi ya polisi ni nini?
Hawa panya road kwa record huwa wanatumia silaha za jadi ambazo kila mtanzania anaweza kuwa nazo ndani, kwanini tusiamua kujitetea kwa kuwa na silaha na unapotokea uvamizi twende wote kwa kishindo tuwape "show" ya maana?
Panya road sio smart kuliko sisi, hawana idadi kubwa kuliko sisi kwanini watutese?
Nawaomba watanzania japo hairuhusiwi kujichukulia sheria mkononi lakini tutoe funzo kidogo patapotokea uvamizi hebu tutoke na marungu na mapanga kwa moyo mmoja tushushe kipigo, tuhakikishe polisi wakifika kazi imemalizika.
Hili jiji watu tumewekeza kwa jasho na damu kwenye mali zetu na biashara zetu, inakuwaje tukubali wahuni wachache watufanye tuishi kwa tabu?
Tuache huu utamaduni wa kipumbavu tutoke tujitetee, polisi wakija sawa wasipokuja watabeba mizoga ya wahuni.
 
Ni muda sasa kamati za ulinzi binafsi zianze vikao. Wazazi wasiojua kuwanyoosha watoto wao adabu wajiandae kufunga maturubai kufanya misiba ambayo hatutahudhuria kuzika takataka.

Kamati hapa mtaani kwetu tumeshafanya kikao cha siri na tumeshakubaliana kuweka malengo na mikakati ya kuanza shughuli ya kupambana na hawa watoto wasio na maadili.

Polisi kutokufanya kazi yao kwa ukamilifu haituzuii sisi kama wananchi kusimama na kulinda mali zetu kwa nguvu zetu wenyewe.

Ambacho hatutaki ni kulaumiwa na hawa wazazi wenye watoto mabazazi wasio na adabu.
 
Ndo kilichobaki asiyefunzwa na mamaye sisi tutamfunza
 
Naandika nikiwa na hasira sana juu ya jinsi mimi na watanzania wenzangu tunavyoishi katika mazingira yetu ya kila siku.
Unakuta mtu naporwa simu, au naonewa lakini watu pembeni wamekaa tu hawashughuliki kumsaidia. Raia wote wanaacha jukumu la kujilinda liwe la polisi tu kana kwamba wao hawahitajiki kufanya juhudi zozote.
Kwenye kura zitaibiwa, patafanywa figisu za wazi lakini watu wametulia tu. Kila mtu anasubiri mwenzake ndio aanze kudai haki na akianza wanamwangalia tu kuwa anajifanya mjuaji watamuunga mkono tu kama kuna dalili za yeye kwenda kufanikiwa.
Kuna ishu kama hii ya panya road, inakuwaje watu mia moja mtaa unafungwa na watu 10? Polisi hata watuahidi vipi hawawezi kuwa kila eneo kwa wakati husika. Nchi zilizoendelea pamoja na kuwa na mifumo mizuri ya ulinzi lakini bado raia wanaruhusiwa kumiliki silaha ili kujitetea. Cha ajabu utakuta mtanzania hana hata panga ndani la kujilinda siku pakitokea uvamizi, ukimuuliza atakuambia kazi ya polisi ni nini?
Hawa panya road kwa record huwa wanatumia silaha za jadi ambazo kila mtanzania anaweza kuwa nazo ndani, kwanini tusiamua kujitetea kwa kuwa na silaha na unapotokea uvamizi twende wote kwa kishindo tuwape "show" ya maana?
Panya road sio smart kuliko sisi, hawana idadi kubwa kuliko sisi kwanini watutese?
Nawaomba watanzania japo hairuhusiwi kujichukulia sheria mkononi lakini tutoe funzo kidogo patapotokea uvamizi hebu tutoke na marungu na mapanga kwa moyo mmoja tushushe kipigo, tuhakikishe polisi wakifika kazi imemalizika.
Hili jiji watu tumewekeza kwa jasho na damu kwenye mali zetu na biashara zetu, inakuwaje tukubali wahuni wachache watufanye tuishi kwa tabu?
Tuache huu utamaduni wa kipumbavu tutoke tujitetee, polisi wakija sawa wasipokuja watabeba mizoga ya wahuni.
Mi nafikiri tungeanza na hawa majambazi na mafisadi wa kalamu, hawa ndio sababu kubwa tabaka la chini wanajiingiza kwenye vitendo vya kihalifu.

Vijana hawana future, unategemea kuna nini?
 
Unafiki ndio umetufanya tuwe hivi tulivyo, tukiacha unafiki automatically uoga nao utatoweka. Unafiki ni mbaya sana ila sisi wabongo tunauchukulia poa tu, hii nidhamu ya uongo ndio imetufikisha hapa tulipo. Hawa viongozi ndio maana wanatuchukulia poa tu
 
Leo nilikua nakatiza mitaa ya Taifa,ghafla bodaboda akakwapua Simu,Mtu anaita MWIZI mwizii bhasi ikawa imeisha hivyo
 
Mi nafikiri tungeanza na hawa majambazi na mafisadi wa kalamu, hawa ndio sababu kubwa tabaka la chini wanajiingiza kwenye vitendo vya kihalifu.

Vijana hawana future, unategemea kuna nini?

Uhalifu ni uhalifu tu. Wakalamu ni katiba bora lakini panya road ni za kichwa
 
Back
Top Bottom