Watanzania tujipongeze: Tz ni ya 5 duniani kwa kasi ya ukuaji uchumi.

uchumi unakuwa kwa ngazi ya taifa ... lkn kwa huku mtaani maisha au vijijini maisha ni magumu kuliko kipindi kilichopita....
 
20170617_121905.jpg

Tufanye kazi kwa ajili ya hawa watoto ili wakikua waweze kupambana na watoto wenzao wa Kizungu.
 
1. Kushangilia kasi kubwa ya kukua uchumi bila kueleza ukubwa wa uchumi, unaweza kushangilia uchumi kukua kwa asilimia mia moja kutoka shilingi mia moja kwenda shilingi mia mbili.

2. Kasi kubwa ya kukua uchumi ni dalili ya uchumi mdogo. Ni kama vile mtoto mdogo anavyokua kwa kasi sana ukimlinganisha na watu wakubwa.
 
2. Kasi kubwa ya kukua uchumi ni dalili ya uchumi mdogo. Ni kama vile mtoto mdogo anavyokua kwa kasi sana ukimlinganisha na watu wakubwa.
ni dalili nzuri, kama mtoto anakua kwa kasi ipo siku atamfikia na hata kumpita yule mkubwa.

China kabla ya kuendelea na wao walipitia kipindi kigumu kama sie tu. huwezi ukakua bila ya shida kdogo.
 
uchumi unakuwa kwa ngazi ya taifa ... lkn kwa huku mtaani maisha au vijijini maisha ni magumu kuliko kipindi kilichopita....
tatizo watu hawataki kufanya kazi, wanataka pesa iwafate wao badala ya wao kwenda kuisaka pesa.
 
salaam...

kama kichwa cha habari kinavyosomeka. Hii taarifa imetolewa na world bank (WB), uchumi wetu wa Tanzania unakua kwa kasi ya 7.2% kwa mwaka huu 2017. Hivyo kuifanya Tanzania kuwa ya 4 duniani na ya pili kwa Africa kwa kasi ya ukuaji uchumi. naomba tujipigie makofi...

View attachment 526300

Ushauri: tusiendekeze sana siasa, tuchapeni kazi jamani. ugumu wa maisha hatoumaliza Magu wala Loawasa. ni sisi wenyewe raia tukichapa kazi kwa bidii tutau tokomeza umasikini. kila mtanzania kwa nafasi yake aliyopo ajenge nchi. siasa tufanye ikifika 2020. sasa hivi tuwaache waliochagulia wafanye kazi zao, huu sio muda wa kuwa evaluate. they need time to accomplish what they have promised.
Natabiri machafuko makubwa kwenye thread hii, ama la sivyo umuombe mange atoe hizi takwimu
 
Kwa hiyo unaishi maghorofani lakini unajidai una shidaa?Hebu njoo Kikonga Tulime.
We kweli LIJINGALAO la ccm! nani kasema nna shida?

IVI ZILE NOAH MWENYEKITI WAKO ATAZITOA LINI? nasikitika mpaka leo hajatoa zile milioni 50 kwa kila kijiji!
 
Natabiri machafuko makubwa kwenye thread hii, ama la sivyo umuombe mange atoe hizi takwimu
hahaha kweli mkuu, yaani hapa nijiandee kushambuliwa na team mange. maana wao wana muda wa kutosha kuwepo online siku nzima ila bado wanalalamika maisha magumu.
 
ni dalili nzuri, kama mtoto anakua kwa kasi ipo siku atamfikia na hata kumpita yule mkubwa.

China kabla ya kuendelea na wao walipitia kipindi kigumu kama sie tu. huwezi ukakua bila ya shida kdogo.
Anaweza kufa kwa kifaduro kabla ya kufikia miaka mitano pia.

Let's put things in perspective.

Kuna watu wakisikia Tanzania ni ya tano kwa kukua uchumi duniani wanashangilia kama vile wameambiwa Tanzania ni ya tano kwa ukubwa wa uchumi duniani.

Vitu viwili hivi ni tofauti.

Unaweza kuongoza kwa kukua kwa uchumi halafu ukaongiza zaidi kwa kukua kwa population mpaka kuongiza jwako kwa kukua kwa uchumi kukakosa maana.

Nyerere alipata shida sana na tatizo hili katika mipango yake ya maendeleo ya miaka mitano mitano miaka yote ya 60 na 70.
 
Watanzania jamani kuweni na akili kila siku mnaambiwa Sekta zinazochangia kwenye pato la taifa-kama Nishati, Madini, telecommunicatio, utalii Watanzania wengi hawajaajiliwa huko na kinachopatikana kwenye hizo sekta bado kinapelekwa kwenye sekta ambazo haziwafaidishi watanzania wengi
 
Na uchumi unaweza kukua hela karibu zote wakachukua kina Acacia katika makanika..

Huku Watanzania wanashangilia kukua kwa uchumi.
 
Back
Top Bottom