Watanzania tuelimike, kuchana pesa kwa kisingizio cha "chuma ulete" kumepitwa na wakati

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,332
Leo hii kumekuwa na ongezeko kubwa la noti kuukuu, zilizochakaa na kuchanwa kwenye ncha au kutobolewa kwa makusudi kabisa kisa wafanyabiashara wanaamini katika ushirikina.

Watanzania wenzetu mnahiaribia nchi yenu wenyewe uchumi wake, haiwezekani pesa umeipokea ni nzima tena mpya inanukia wewe unakunja kunja kama toilet pepa then unaitunza mahali unapojua wewe ukija kuitoa huko kumpa mwenzio utazani imetafunwa na ng'ombe kwa namna hii kwa nini pesa yetu isidharaulike, kwanini mkipewa dollar mnaitunza kwa heshima kuliko mnavyojali vitambulisho vyenu vya NIDA.

Sasa kuna huu mtindo ulioibuka wa sasa sijuhi nani katukaririsha ujinga huu kwa jina CHUMA ULETE kama serikali isipochukua hatua kutokomeza kirusi hiki kipya dhidi ya NOTI zetu hasara ni kubwa.

Haiwezekani katika noti kumi ulizonazo mfukoni lazima ukutane na iliyochanwa au kunyofolewa kipande, katika hizo nawe unakimbilia kuichambua kwenye waleti chap ile yenye tatizo umshikishe mwenzio usibakie na msala huo peke yako matokeo yake mpaka ATM zetu nazo zimeanza kuzitapika noti hizo hizo cha ajabu hata public awareness haifanywi na wadau au serikali pengine wameridhika na hali au ndo tuseme bado wanamudu uharibifu huu.

Kama pesa zetu tumezidharau wenyewe nakuzishusha thamani kiasi cha kuziita pesa za madafu bado hata kuziona zikiwa nzima pia tunaona donge, tafadhali tuachane na dhana hizi potofu za imani zisizo na maana yeyote ndugu Watanzania wenzangu.

Ikiwa kila noti inayopitia kwako utaichana kuepuka chuma ulete, jirani yako naye afanye hivyo keshokutwa tutakuwa na watu milioni 10 kwenye nchi wachanaji pesa. Je, kesho ya pesa zetu itakuwaje?
Eti machinga nae apokei pesa mkononi anakwambia umtupie chini au mahali pachafu eti ndo aokote sijuhi utamuibia nyota mara sijuhi nini itakuwa nini.

Hizi ni imani za kitoto kama kipindi hicho tukiwa watoto tuliaminishwa mara baada ya kukojoa hakikisha unatemea mate hili wachawi wasikuroge au ukinyoa fukia nywele usirogwe mbona siku hizi saluni tunakwenda sana na hizo nywele tunawaachia huko huko na atudhuriki na hao wanga? Haya mambo yamepitwa na wakati huu ni muda wa kufanya mambo yenye kuleta manufaa nakuachana na vitu vya dhahania.

Tafadhali tuache ujinga tufikirie vya maana kama hao wanaozitengeneza huko kwao wanazitunza na kuziheshimu wakijua nje ya kuzitumia kama medium of exchange pia pesa utambulisha taifa na utumika wakati mwingine kama kipimo cha uchumi wa nchi kwanini tusiipe matunzo stahiki?

Yangu ni hayo tu Watanzania wenzangu TUBADILIKE kuendelea kuamini imani potofu nikujidumaza na kulitia taifa lako umasikini usiyo na ulazima.
 
Wachaga hao
Kuna mchaga alikuwa akinisimulia jinsi alivyokuwa akichana pesa kisa kujikinga na chuma ulete.
Nilimwona primitive sana
Ni kweli mkuu haya mambo yanakasirisha sana, kitendo cha kumpa mtu hela nzima anakupa pesa ilochanwa kimakusudi inaudhi mno kisa watu wanaabudu ushirikina.
 
Dar es Salaam yapo maeneo yanaongoza kwa uchanaji, kwa kisingizio iko cha chuma ulete.
Unatoa hela bank/ama kwenye ATM unakuta notes kadhaa zimechanwa kwenye kona zotee
 
Mie na wale wanaozifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Wananikera basi tu!
Na haohao wanakua kimbelembele kukataa hela kuukuu.
Ila yote haya JK, noti za kabla ya awamu yake zilikua imara sana. Sijui kwanini huyu mswahili wa Msoga aliamua kubadili na kutuletea noti zisizo na ubora, hali akijua taifa hili bado lina nakisi kubwa ya watu sio civilised.
 
Kwa hiyo huyu chuma ulete anashindwa kuchukua pesa kwa kuwa tu imechanwa pembeni? Huyu atakuwa siyo chuma ulete tunayemfahamu.Ndugu zangu tuache imani za ajabu.
 
Tuanzishe kampeni ya kutopokea pesa yoyote iliyochanika. Nadhani kila mmoja akili zitamkaa sawa. Kwa kipindi cha mwaka mmoja hii tabia itakwisha
 
Je umetoa suluhu mbadala?
Sipendi hii tabia, ila kama hujawahi 'pigwa' kisawasawaa, huezi elewa kwa nini tunachana
 
Hauhljafanya utafiti wa kutosha kama kweli chuma ilete huiba hela na kuchana ndio kinga yao.
Ukikua utaacha kulaumu.
Kila mtu alinde pesa take anavyojua tusipanguane.
Hakuna mwenye pesa hivuo usiumie sana utapata presha.
Pesa mpya zinapendwa sana na chuma ulete na dawa yao ni kukata kona ya hio noti.
Mi binafsi sita acha kuchana pesa hasa mpya nilioipokea benki, pesa kuukuu kwangu hazina shida.
 
Back
Top Bottom