Lindi: Benki Kuu yapokea Noti zinazodaiwa kuwa na ‘Chuma Ulete’

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Meneja Huduma za Kibenki wa Benki Kuu Kanda ya Kusini, Melchiades Rutayebesibwa amesema fedha zilizochakaa zimekuwa zikirudishwa ili kubadilishwa ambapo zipo zilimwagikiwa rangi, zilizoandikwa na zingine huja zikiwa zimekatwa katika pembe nne.

Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyotokana na maswali aliyoyauliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini alipotembelea katika banda la maonyesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Alihoji kwanini baadhi ya benki za biashara zinatoa fedha zilizochakaa kwa wananchi.

Amesema kuwa katika mapokezi ya fedha chafu huwa wanapokea zilizomwagikiwa na rangi, zilizochorwa au kukatwa kwenye pembe nne za noti kwa imani za kitamaduni (chuma uletee) na zingine huunganishwa kwa gundi.

"Kuna wakati zinakuja fedha kubadilishwa zingine zinakuwa zimemwagikiwa rangi, zingine zimechorwa au kukatwa kwenye kingo nne za noti zake kwa imani za kitamaduni (chuma uletee)," amesema Rutayebesibwa.

“Unajua moja ya sera ya Benki Kuu ni kuhakikisha wakati wote uwepo wa fedha safi katika mzunguko wa fedha hapa nchini na ikumbukwe Benki Kuu kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2006 inawajibu wa kutengeneza pesa za Kitanzania,” amesema Rutayebesibwa.

“Tunazisambaza fedha za Kitanzania hapa nchini kupitia mabenki ya biashara kwa kuondoa fedha zote kwenye mzunguko hapa nchini hasa zilizochakaa ama zilizoharibika au aina yoyote ya uharibufu,” amesema Rutayebesibwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amehoji kwanini BoT wanaruhusu fedha chafu zilizochakaa kutolewa ndani ya benki za biashara," amesema.

“Kuna wakati unachukua fedha katika benki za huko vijijini mpaka unajiuliza hii pesa imetoka benki kweli zipo baadhi ya benki unakuta wanapesa safi mpaka unapenda ukatoe mara kwa kwa mara huko,” amesema Sagini.

“Lakini kuna vibenki huko sijui wakileta mnawapiga faini nahisi ndiyo maana wanaogopa kuleta. Unakuta benki ipo kijijini ukitoa fedha unachanganyikiwa ilivyochafu, wakati sisi tunaamini kuwa fedha ukitoa benki lazima iwe safi,” amesema Sagini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara, Nassor Omari amesema kuwa huwa wanaweka muda maalumu ambao benki za kibiashara hukusanya na kichambua fedha zilizochakaa na kuzirudisha ambapo hupewa mpya.

“Kabla hawajaleta kwetu wanakaa na kuzichambua ili zilizosafi zinabaki na zilizochakaa zinarejeshwa Benki Kuu ili kupata mpya kama zipo zilizochakaa na wanazitoa kwa wananchi hilo ni tatizo la benki za kibiashara,” amesema Omary.

MWANANCHI
 
Chuma ulete haifanyi kazi bank katika sehemu freemason wamecheza ni kwenye mabank hakuna mchawi anaaingia.
Mchawi haibi Hela hata akiingia ndani mwako akichukua tu atoki ndani.
Pole bro.

Mentality ndo kila kitu.

Ila mantiki ya kawaida tu ikufundishe, kwamba kama benki hawawezi basi na dukani au nyumbani hawawezi pia. In fact hakuna kitu kama hicho.

Benki kila kitu kinaenda kwa mahesabu, cha kuchekesha hata vibanda vya hela watakuambia hii kauli 'Ukitaka kuwakomesha chuma ulete, we funga mahesabu hata mara tano kwa siku chuma ulete haingii' sasa benki ni kama kila baada ya muamala mahesabu yanafanyika.

So hapo huo 'uchawi' unaousema ni hesabu tu. Mchawi hesabu. Akili mtu wangu, akili tu.
 
Pole bro.

Mentality ndo kila kitu.

Ila mantiki ya kawaida tu ikufundishe, kwamba kama benki hawawezi basi na dukani au nyumbani hawawezi pia. In fact hakuna kitu kama hicho.

Benki kila kitu kinaenda kwa mahesabu, cha kuchekesha hata vibanda vya hela watakuambia hii kauli 'Ukitaka kuwakomesha chuma ulete, we funga mahesabu hata mara tano kwa siku chuma ulete haingii' sasa benki ni kama kila baada ya muamala mahesabu yanafanyika.

So hapo huo 'uchawi' unaousema ni hesabu tu. Mchawi hesabu. Akili mtu wangu, akili tu.
Jidanyanye...
 
Jidanyanye...
Watu wa Ushirikina na Iman imani tuu huwa mnakuwa na vitisho sana ila ushahidi hamna.
Mambo ya chuma ulete ni story za kuaminiwa na watu wenye Uwezo mdogo wa kufikiri.

Hivi hao lindi wangekuwa wanachuma ulete si wangekuwa mbali sana ki maendeleo ila ndo watu wanaonuka shika balaaa.


Alafu hizo story utazisikia kwa watu wa hali ya chini yaani choka mbaya haswa.


Kama kwenye kazi yako una hisi kuna chuma ulete nakusahauri kuwa mtumizi mzuri wa hela na punguza wadokozi ambao wanatumia mwanya huo huo wa chuma ulete kukuibia.
 
Miaka ya nyuma nilienda lindi nadhani ndio mkoa unaoongoza Kuwa na matumizi ya pesa zilizochakaa na chafu sana na wanazitumia bila shida..pesa hizo ukija kutumia Dar hakuna mtu anapokea kwa hali yake zilivo mbaya.
Uko sahihi,nilipata tabu sana Nachingwea,nilikuwa nazikataa
 
Sawa mkuu. Mimi siamini kabisa whatsoever
Ni kama kutoamini kuna deep state ukiamini nchi inaongozwa na katiba ukawa unaijibu serikali unavotaka haitamaanisha madhara yake hayatakukuta
 
Ni kama kutoamini kuna deep state ukiamini nchi inaongozwa na katiba ukawa unaijibu serikali unavotaka haitamaanisha madhara yake hayatakukuta

Mimi siamini mambo ya kufikirika.
 
Back
Top Bottom