Watanzania Tuchangamkie Fursa za Total. Kujenga Vituo 100 vya Mafuta vya Total Vitakavyomilikiwa na Watanzania kwa Mfumo wa DODO

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,600
Wanabodi,

Baadhi ya Watanzania wenzetu ni masikini kwa kukosa tuu uthubutu wa kuchangamkia fursa za kibishara zinazojitokeza. Watanzania akiona mtu anafanya biashara fulani, na anapata, na yeye ndio anaiga. Hakuna biashara inayolipa vizuri kama biashara ya kununua hisa, stock markets, lakini kwa vile watu hawaoni inaendeshwaje, na pesa zinaingiaje, Watanzania wengi hawana time na biashara ya hisa, hivyo Watanzania wengi wanaonunua hisa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, wengi ni wale wa Masaki, Oysterbay, Mikocheni na Mbezi Beach, lakini Watanzania, waliowengi, wanafanya biashara za kuuza bidhaa.

Baada ya biashara ya hisa kwa faida, biashara ya pili yenye faida kubwa ni biashara ya huduma za utilities, kama umeme, maji na gesi.

Biashara ya tatu kwa faida ni biashara ya kuuza bidhaa za walaji, yaani consumables, kwenye kundi la biashara ya bidhaa za walaji, japo bidhaa zinazoongozwa kwa kuuzwa ni bidhaa za chakula, bidhaa ya mafuta ya magari, ndio biashara yenye faida kubwa, kuanzia uchimbaji, usafishaji, usafirishaji, uagizaji na usambazaji. Katika maeneo matatu ya kwanza, yaani uchimbaji, usafishaji na usafirishaji, sio biashara ya kitoto, hakuna hata Mtanzania mmoja mwenye msuli wa kuingiza pua huko. Sisi uwezo wetu ni kwenye uagizaji na usambazaji, na hapa ndipo Total anapoingia.

Kampuni ya Total ni mchimbaji mafuta, ni msafishaji mafuta, ni muagizaji mafuta, msafirishaji mafuta, na msambazaji mafuta kupitia vituo vya Total. Kwa Tanzania, Total ndio kampuni inayoongoza kwa idadi ya vituo vya mafuta na mafuta yake ni bora!. Kwa sasa Total inavyo vituo vya mafuta zaidi ya 100 kwa Tanzania nzima, na inataka kuongeza vituo 100 vingine ambavyo vitamilikiwa na Watanzania kwa mfumo unaitwa DODO.

Msikilize Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Total, Marsha Msuya-Kileo, akiizungumzia fursa hii.


Haya Watanzania wenzagu, tuchangamkie fursa hii ya Total.

Paskali
 
Dodo - dealer owned dealer operated..
Lazima mpunga wa kujenga uwe nao...

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
Mkuu Serio, sio lazima uwe na mpunga wa kujengea, unachotakiwa kuwa nacho ni ardhi ya eneo la kujengea lililopimwa na lina hati ya owneship yako. Hiyo hati ndio collateral ya kupatiwa mkopo wa kujengea kutoka bank, mkataba tuu wa franchise ya Total ni collateral tosha!
P
 
Mkuu Serio, sio lazima uwe na mpunga wa kujengea, unachotakiwa kuwa nacho ni ardhi ya eneo la kujengea lililopimwa na lina hati ya owneship yako. Hiyo hati ndio collateral ya kupatiwa mkopo wa kujengea kutoka bank, mkataba tuu wa franchise ya Total ni collateral tosha!
P
Fursa nzuri
 
Back
Top Bottom