Watanzania ni wanafiki hasa kuhusu Sakata la BSS

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Watanzania wengi wanatatizo lakuwa wanafiki na wasio na shukrani hata kidogo, nimeona wengi wakiiponda BSS na wengine kwenda mbali zaidi kuitukana na kutoa lugha chafu juu yao Cha ajabu mpaka washiriki wenyewe walioshiriki bss nao wameingia kwenye Huu mkumbo.

Pamoja na BSS kutuumiwa kula hela ya washiriki lakini pia tusisahau bss wanamchango mkubwa Sana kwa Hawa washiriki wasio na shukrani hata kidogo hiv leo hii bila bss Nani angemfahamu kayumba au hamisi,Nimeangalia interview ya hamisi imenisikitisha Sana ametumia lugha chafu kuisema BSS.

Washiriki wengi walikuwa wanafanyiwa audition wakiwa hata kupaka make up walikuwa hawajui na wengine walikuja ikiwemo hamisi na mavazi ya ajabu ajabu wakafundishwa kuvaa wakawa wanatrainiwa vocal pamoja na kuimba na bendi ili watu hawaoni na washiriki wenyewe hawaoni zaidi ya kutoa lugha chafu.

walikuwa pia wanakaa kwenye hotel za nyota 5 Kama kambi na Zina gharama kubwa Sana kweli tunashindwa hata kuliona hili kweli?

Hao washiriki wanaoisema vibaya BSS mbona hatuoni juhudi zao katika mziki? Kazi yao Ni kutupia zigo lote kwa BSS bila hata wao wenyewe kujiangalia.kuna wasanii wengi hawajapata hata bahati ya kupata platform kubwa ya kuonekana ya BSS lakini wametoboa kwenye mziki wao wameshindwa vipi kutoboa?

NB: Ni kweli BSS wanakula hela lakini hiyo haimaanishi tusione uzuri wao waliofanya kwenye hii tansia ya mziki.
 
Nchi hii ukitenda mema kimbia kabla hawajakugeuka.
Wakati ukitenda mema utapewa majina yote mazuri, ukikosea utaogeshwa uchafu wa kila namna.
Ninaongea kwa uzoefu.
Hii nchi imelogwa na watu wake pia.
Hamisi alikjua kama chokoraa, Rita kamtetea sana ssna na kumtia moyi kuwa anaweza.
Hii ni zaidi ya zawadi ya million 300.

Watu wanapenda kupewa samaki na sio ndoano ya kuvulia samaki wala elimu juu ya uvuvi.
Naruadia;
Zawadi ilikuwa chachu ya mashindano lakini lengo kuu ni kutambua vipaji na kuwatambulisha wenye vipaji ili jamii iwapokee na waendeleza vipaji wawaone.
Kazi hii ilifanyika kwa weledi, walifaulu mara zote...JAPO WAMEFELI UPANDE WA ZAWADI...hili silitetei hata kidogo ni doa kubwa.
Namshauri Madam Rita arekebishe hili na mashindano yasikome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ' Upuuzi ' wako wote huu uliouandika hapa ndiyo ' unahalalisha ' huo ' Uhuni ' wa Bongo Star Search ya Madam Rita na Washirika wake kwa huyo Kijana wa Watu ambaye anazunguka kila Mwezi kutokea Mkoani kuja Jijini Dar es Salaam tena hadi Wazazi wake wakiwa Wanakopa Pesa kwa Watu ili Kupigania Haki ya Mtoto ( Kijana ) Wao?

Kuna Watu uwezo wenu wa Kujenga Hoja unakera hadi Kutusikitisha. Siku zingine kama mnajijua ni ' Watupu ' Vichwani mwenu msiwe mnatupotezea muda kwa Kuja na ' Hoja ' za hovyo hovyo kama hizi. Hiyo Kampuni imefanya si tu ' Uhuni ' bali ni ' Ukatili ' kabisa kwa Mshindi huyo Kijana wa Watu. Hebu Wewe vaa Viatu vyake ungejisikiaje?

Tena nitashukuru kama Wizara husika itaipa Adhabu Kali hiyo Kampuni na ikiwezekana hata Kuifungia kama si Kuifuta kabisa ili iwe Fundisho kwa ' Wahuni ' wengine nchini.
 
Peak ya matumbozzz
Alikuwep kwenye Peak kakaa tena alikua ana imba Mpak na kina kidumu wa Burundi
If am not mistaken, Sahivi kaoa sijui yuk wap
Tanzania kuna vipaji vingi havipewi nafasi mfano amin,ben paul, barnaba hawa ni wanamuziki wazuri sana lakini tazama hatua waliyopo ni ya kawaida sana,hawa walitakiwa wapewe support kubwa
 
Kwahiyo ' Upuuzi ' wako wote huu uliouandika hapa ndiyo ' unahalalisha ' huo ' Uhuni ' wa Bongo Star Search ya Madam Rita na Washirika wake kwa huyo Kijana wa Watu ambaye anazunguka kila Mwezi kutokea Mkoani kuja Jijini Dar es Salaam tena hadi Wazazi wake wakiwa Wanakopa Pesa kwa Watu ili Kupigania Haki ya Mtoto ( Kijana ) Wao? Kuna Watu uwezo wenu wa Kujenga Hoja unakera hadi Kutusikitisha. Siku zingine kama mnajijua ni ' Watupu ' Vichwani mwenu msiwe mnatupotezea muda kwa Kuja na ' Hoja ' za hovyo hovyo kama hizi. Hiyo Kampuni imefanya si tu ' Uhuni ' bali ni ' Ukatili ' kabisa kwa Mshindi huyo Kijana wa Watu. Hebu Wewe vaa Viatu vyake ungejisikiaje? Tena nitashukuru kama Wizara husika itaipa Adhabu Kali hiyo Kampuni na ikiwezekana hata Kuifungia kama si Kuifuta kabisa ili iwe Fundisho kwa ' Wahuni ' wengine nchini.
Ungesoma main point ya mada yangu usingeandika gazeti lote Hilo.
 
Back
Top Bottom