NairobiWalker
JF-Expert Member
- Oct 31, 2012
- 11,861
- 11,887
Tofauti na Wakenya wasioogopa kuongelea ukosefu wao mitandaoni na popote pale, Wabongo wana tabia ya kuficha ukosefu wao na hata kutia mbaroni wanaouweka wazi. Ndiyo maana watu kama joto la jiwe wamo humu wanadhani Tanzania ni mahali pazuri sana pasipo na shida. Haya, ona haya, mwanafunzi atiwa mbaroni kwa kusema ukweli.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Tungu Mgaya, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma tangu jana kwa kutuhuma za kupiga na kusambaza picha inayoonesha shida ya maji chuoni hapo.
MWANAFUNZI MUYAGA TUNGU ANAYEDHANIWA KUPIGA PICHA ZA KUONYESHA TATIZO LA MAJI UDOM MIKONONI MWA POLISI DODOMA
Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesoma Sayansi ya Asili (Natural Science ) chuo kikuu cha UDOM , Mugaya Tungu alikamatwa Jan 21 mwaka 2020 akiwa chumbani kwake ndani ya bweni la wanafunzi UDOM.
Mwanafunzi huyo alikamatwa na polisi bila kuambiwa kosa lake ni lipi na kwanini alikamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa kituo cha polisi chimwaga Dodoma.
Lakini pia rafiki yake wa karibu (jina lake limehifadhiwa) naye alifuatwa kukamatwa usiku lakini alishtukia mapema na hakuweza kulala chumbani kwake hivyo polisi walimtafuta na hawakumpata.
THRDC tumefuatilia kwa ukaribu kukamatwa kwa mwanafunzi huyo na kupata taarifa kwamba mwanafunzi huyo anadhaniwa kupiga picha zinazoonyesha uhaba wa maji katika chuo kikuu cha Dodoma. Wanafunzi wanapata changamoto sana kuhusu maji hali inayowasababishia kupanga foleni muda mrefu na pengine kuchelewa masomo darasani, hivyo mwanafunzi Tungu anadaiwa kupiga picha za wanafunzi wenzake wakiwa wamepanga foleni muda mrefu na kwa wingi na hatimae kukamatwa kwake.
Wanafunzi wenzake walienda leo jan 22, 2020 mnamo sa saba mchana kwenye kituo cha polisi alipowekwa mwanafunzi Tungu lakini hawakufanikiwa kumuona. Wanafunzi wenzake baada ya kufika kituo cha polisi waliambiwa kuwa Tungu amepewa dhamana ya polisi lakini walipohoji endapo kuna mtu amemdhamini waliambiwa hayo hayawahusu.
Hata hivyo wanafunzi wenzake wamejaribu kupiga simu zake hazipatikani na mwanafunzi huyo hajaonekana bwenini mpaka sasa hivyo bado haijulikani alipo.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu kukamatwa kwa mwanafunzi Mugaya Tungu, na tutawapa taarifa kadri tutakavyobaini.
Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC)
Jan 22, 2020