Watanzania Na umarekani


Afadhali umezungumza ndugu yangu; nimewahi kusoma mialiko ya July 4 bash inayofanyika Dar nikachoka. Tanzania siku hizi tuna hata Haloween day, Labor Day weekend na Veterans' Day Weekenda ambazo haziendani kabisa na zetu tunazojua bali ni zile za Marekani.
 
Kwani wanasheherekea nini, na kunausahihi wowote kwamba hamna nchi nyingine wanaoitambua hiyo sherehe?

Tofautisha kuitambua na kusherehekea, kenya wanaweza kuitambua 9DEC lkn wasisherehekee.
 

.....Happy Thanksgiving arifu!...
 
duuh ila kweli asee tushakua maphotocopy machines wa style za maisha za watu
 

Umemzodoaje???? Ataoga Maji ya bahari
 
Hata nywele tunataka za kizungu, ingawa za maiti lakini tunazinunua kwa bei mbaya sana, ingawa zinatunyonyoa nywele zetu za asili na kutufanya vipara lakini tuko tayari kujiharibu na kuzishonea vichwani mwetu ili tuwe kama wazungu. Tupo tayari tuunguwe vichwa vyetu kwa kemikali lakini tuonekane kama wazungu aka wa-maana.

Rangi tunataka za kizungu, tuko tayari kula makemikali ya kutudhuru na kututia makansa ili tuwe weupe, tuko tayari kunuka miili yetu kwa kujichubuwa kwa makemikali ili tuwe weupe.

Tuko tayari hata kumkosoa Mwenyeezi Mungu kwa kuabudu picha ya mzungu na kumfanya Mungu ili tunekane wa-maana.

Tumempa mzungu cheo cha Uungu kwa kumuita "Mzungu" (toa "z" hapo uone inakuwa nini).

Tumejidhalilisha na kuendelea kujidhalilisha kwa kujiita "Wa Afrika", neno linalotokana na "Afrit" na (aliyemuasi Mwenyeezi Mungu na baba la mashetani wote) kujinasibisha nae.

Miafrika Ndivyo Tulivyo - Nyani Ngabu
 
He! he !he! mwisho wa mwaka huu pungwa wapi undengerekoni nikatambike!tokomile wapi uzaramuni nikajimwaemwae!mwaka kogwa lini vile makunduchi? mbona watanzania za chini ya mbuyu tunazo nyingi tu sema hamtaki kuzipromoti!
 
kama kizuri unaiga tu, kwa hiyo title tu 'Thanks Giving' na hisi itakua inamaana nzuri
 
Sisi tena! Yaani 50Cent akivaa skuna kesho yake utaona heka heka za mabrazameni na masharobaro kuvaa skuna.
Tunapenda kuiga mambo ya kigeni mengine hayana msingi kwetu tunaiga tuuuuu.
 
wabongo siku hizi husheherekea mpaka haloween.mradi kuiga tu
 
Hiyo sikukuu ya thanks giving ndio inasherehekewaje?
 
Na ile ya halloween ina maana gani? Nilishawahi ona picha watu flani hapa bongo wanaishobokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…