zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
- Thread starter
- #41
hayo maswali nalolijua ni Kuwa Vasco Da Gama alikuwa mzungu wa kwanza kupita Pwani ya Africa Mashariki akienda bara Hindi.. Sasa na wewe unaendelea Kuwa mmbaguzi wa Ujinga badala ya kutupa Elmu kuhusu hayo maswala mengine na ufafanuzi unaturingishia Kama unatoa darasa toa sio ujivuni wa kujua kitu halafu husemi, wengine sisi ni walimu na nyuzi za historia Kama hizi zinztufundisha mengi na tunapata challenges mpya za kuwapelekea wanafunzi wetu Sasa ka wewe hutoi majibu wala maelezo afu unatunanga utakuwa hujatusaidia sisi wala wanafunzi wetu. Siku zote najua Dar Es Salaam ni bandari ya salama ka sio hivyo sema ni nini? Na tupe maana ya majina ya Mikoa ili tuelimike sisi na wanafunzi wetu, ni Kama unajua kitu afu unataka ubembeleeezweee! Kufafanua huo pia ni ubaguzi wa ujinga
Kwanza, punguza ghadhab. Pili, umenifurahisha sana kuwa hasira na hamasa yako ni katika kutaka kusoma na kusomesha. Nakupa mkono wa heko kwa hilo.
Tatu twende taratibu, elimu haipatikani kiharaka na kiurahisi ndio maana leo tunaongelea Ubaguzi wa Ujinga. Laiti tungekuwa tunaipata elimu kiurahisi na sahali kama upendavyo basi tusingekuwa na Ubaguzi wa Ujinga. Nachelea kukupeleka haraka usije nibagua kwa ujinga tu. Tuanze na Dar Es Salaam:
Si Kiarabu tu, ni jina linalopatikana ndani ya Qur'an 10:25:
وَاللّهُ يَدْعُو إِلَى دَارِ السَّلاَمِ وَيَهْدِي مَن يَشَاء إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
WaAllahu yadAAoo ila dari alssalami wayahdee man yashao ila siratin mustaqeemin
But Allah doth call to the Home of Peace: He doth guide whom He pleaseth to a way that is straight.
Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea Nyumba ya Amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Utaona kwa tafsiri hizo, jina Dar Es Salaam halihusiani kabisa na neno "bandari". Isitoshe, kuna miji mingine duniani ina jina hilo, hata mji maarufu sana Kihistoria na Kisiasa, uitwao Jerusalem, nao pia ni Dar Es Salaam, nako hakuna bahari kwayo Dar Es Salaam si "bandari" Salama, maana halisi ni hiyo hapo juu.
Pia kuna nchi inaitwa Brunei Darusalaam (Dar Es Salaam) nako mji wao ni wa bandari na unaitwa Bandar Seri Begawan. Ulidhani ingekuwa Dar Es Salaam.
Ukiridhika ni hili tutahamia lingine.