Watanzania na Ubaguzi Wa Ujinga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania na Ubaguzi Wa Ujinga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zomba, Oct 28, 2012.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naamini na nnadiriki kuandika kuwa Watanzania ni wabaguzi, ubaguzi wao si wa kidini au wa kijinsia au wa kikabila au wa rangi. Hizo ndio njia kuu zijulikanazo za ubaguzi duniani.

  Watanzania, wengi wao, hawana kabisa ubaguzi huo. Ubaguzi wa Watanzania ni wakijinga au wa ujinga. Naamini kabisa kuwa ubaguzi wa Watanzania ni wa ujinga zaidi ya wakijinga. Ujinga hawana ila wana ubaguzi wa ujinga.

  Ikiwa Watanzania hawana ujinga, huu ubaguzi wa ujinga wameutowa wapi? nna uhakika kuwa huu ubaguzi wamepachikwa na Waalimu wao na Waalimu wao walipachikwa na Waalimu wao na hao Waalimu wao walipachikwa huu ujinga walipojengewa mashule na kusomeshwa na kufundishwa cha kuja kuwafundisha hao waliotarajiwa kuwa ndio watakuja kufundisha, matokeo wamewajaza Watanzania ubaguzi wa ujinga.

  Mara kadhaa humu JF nimekuwa nikitumia sentensi "uneducated fool from an uneducated school", nna uhakika wanaonisoma humu JF wameshaisoma sentensi hiyo, si mara moja wala mbili, wako walioielewa wakakaa kimya na wako walioielewa wakashindwa kuielewa na wakaanza kung'aka kuwa hilo si neno la kueleweka. Sina haja ya kulielewesha kwani, muelewa huelewa haeleweshwi. Asiyeelewa hutaka kuelewa na huuliza ili aelewe wala hataharuki na kujifanya anajuwa asichokijuwa, moja ya ubaguzi wa ujinga.

  Ubaguzi mwengine wa ujinga tuliokuwa nao na uliojazwa vichwani mwa wengi ni kuwa Vasco Da Gama ndio kaivumbuwa hii Tanzania au Tanganyika wakati ukweli ni kuwa wakati wa Vasco Da Gama jina Tanzania halikuwepo wala Tanganyika halikuwepo. Kuna anaelipinga hili? Anza.

  Isitoshe, Vasco Da Gama hajawahi kuikanyaga ardhi ya nchi hii, ambayo leo inaitwa Tanzania (jina aliloipa Muhindi wa Tanga). Vasco Da Gama aliishia baharini alipotia nanga manuwari zake, hajashuka wala kuigusa hii ardhi ambayo wengi wanajazwa ujinga wa kusema kuwa Vasco Da Gama ndio mvumbuzi. Swali la kujiuliza, Jee, Vasco Da Gama alivumbuwa kipi? alimkuta nani hapo Kilwa? (Naomba wajuzi wanipe maana ya neno "Kilwa") labda hilo ni neno la Kireno? kwa kuwa umeaminishwa kuwa Vasco Da Gama kapavumbuwa? au maana ya jina (au neno) Sofala, zilipotuwa kwanza manowari zake, ambako alipewa nahodha kipofu akamuongoza hadi Kilwa. Ndio kipofu. Ni ajabu lakini kweli.

  Jee, hayo mmeyasoma huko mnakojazwa ujinga? Ni wangapi leo hii wanaojuwa kuwa hapa katika Ardhi hii kulikuwa kuna mji, kama si nchi, inayoitwa Raptha? Hii Raptha iko wapi? ilianza lini na nani walikuwa Watawala? na imeshia wapi? Maweee!

  Nani leo hii anaejuwa kuwa Majimaji ilikuwa ni vita isiyokubalika na wengi leo hii?

  Nani anaejuwa kuwa Mkwawa alikuwa anaandika Kiarabu, japo kuandikiwa?

  Nani leo hii anaekiri kuwa nchi hii ina mbegu na si shina au tawi tu la Uarabu, la hasha, si nchi hii, Kontinenti hili? Nakuhakikishia hakuna. Kwanini hakuna? ni Ubaguzi wa ujinga.

  "Afrika" ni lugha gani, au neno? tuseme jina hilo? vyovyote, iwavyo na iwe, limetokana na lugha gani uijuwayo wewe? zaidi ya neno au jina "Afrit"? kama huna zaidi ya hapo basi ujuwe umejazwa ujinga.

  Dar Es Salaam. ni lugha ipi na neno hilo linatoka wapi? anaekuambia ni "Bandari Salama" basi huyo kakujaza ujinga kwani si maana yake ya ukweli.

  Arusha, unajuwa maana yake? na neno hilo limetoka wapi? hali kadhalika Tanga? Tabora? Morogoro? Ruaha? Mbeya? Shinyanga? Zanzibar?

  Kama huyajui yote hayo basi ujuwe umejazwa ujinga wa ubaguzi wa ujinga. Hakuna zaidi.

  Tujadiliane.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  What do you want to say zomba? Unarudi kule kule...unataka kusema aliyetuletea mema ni mwarabu na sio mzungu wakati wote ni wale wale. Na huo ndio naona ujinga tulionao.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Moja ya ujinga ni pale Mtanzania anapojiona kuwa anajuwa kila kitu akakitolea maana isiyokuwepo. Huo ndio ubaguzi wa ujinga uliojazwa nao. Funguka!
   
 4. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Uzi wako hauna vingezo vya kunishawishi kuchangia, maana wewe mwenyewe hujaweza kufikisha maudhui uliyotaka kufikisha
   
 5. H

  Han'some JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe ndiyo mjinga bz hujui una andika nini zaidi ya kujikanyaga2.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Na huu ubaguzi wa kijinga naona wengi wanaufagilia...teh teh teh! Mimi si mbaguzi wala sina mpango wa kuufuatilia ubaguzi. Utaninyima maisha na kula kwangu mjini bila sababu ya msingi
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Siyo saizi yako, kaa pembeni.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Paainishe nilipo-jikanyaga. Nakuhakikishia huwezi.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  "Ubaguzi wa Ujinga". Soma vizuri.
   
 10. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,661
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  Umefulia bro.

  Uzi wako hauna mshiko hata chembe, na unazidi kujiumbua kwa ufinyu wako wa weledi na jinsi upeo wako wa fikra ulivyo mdogo.

  Do yourself a favour: wee unafaa kuchangia tuu kwa staili ya mipasho kutetea hoja zozote zinazohusu Uislamu na Waislamu dhidi ya Ukristo au Wakristo. Hamna zaidi ya hapo.
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanangu Zomba rudi kwenu Kamachumu ufundishwe kufikiri. Hakuna ujinga na upuuzi kama kutaka kujionyesha umesoma kuliko wengine. Hakuna ujuha kama kudhani kuwa kwa kuwatukana watu unawaelimisha. Nimegundua makosa yafuatayo kwenye mada hii
  Mosi mleta mada anajiona kasoma sana kwa vile amesoma mistari miwili ya historia,
  Pili, mleta mada licha ya kuhitaji kuelimishawa anaonyesha udhaifu mkubwa kwa ujumlisho wake wa kuwafanya watanzania wote waonekane wajinga. Ndiyo kila mtu ni mjinga katika jambo au mambo fulani.
  Tatu, mleta uzi hana chembe ya adabu na aibu. Allichofanya ni kuonyesha upogo na ujuha wake zaidi ya elimu,
  Nne, mada yenyewe aliyoleta haielewi vizuri,
  Tano, Mada yenyewe haieleweki zaidi ya kurejea jambo moja ujinga ambao hata hivyo hajauthibitisha kwa ngazi ya taifa zaidi ya ujinga wake binafsi,
  Sita mleta hoja ameleta hoja isiyo na utafiti,
  Sita, mada yenyewe imeandikwa hovyo haina mtiririko kimantiki,
  Saba,Mleta mada anatumia maneno mazito kama vile watanzania ni wajinga, jambo ambalo kiutafiti ni hatari. You don't just make such vague and bold statements without supporting them with evidence with empirical realities.
  Nane, licha ya kukose premises mleta mada ameshindwa hata kutoa hoja yenye mashiko ambayo angeweza kuitetea kwa ushawishi wa kiakili.
  Tisa, mleta mada ametumia hasira badala ya busara na akili.
  Na mwisho mleta mada ndiye mjinga hata zaidi ya wale anaowashutumu.
  Makosa yake ni mengi yanweza kufika hata mia kama ningekuwa na muda wa kuichambua mada yenyewe.
   
 12. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,661
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  Basically, hoja yake unaweza kui-summarize kwa maneno manne tuu:

  Wamanga and Uislamu rule!!
   
 13. H

  Han'some JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Well said aisee. Mwishowe, mleta mada ndiyo mjinga.
   
 14. Grand Master Dulla

  Grand Master Dulla JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 378
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35


  nimeshindwa kuelewa unataka kulenga kitu gani ila kwa juu tu unamaanisha unausifia utamaduni wa kiarabu!!kuhusu Mkwawa hiyo ni kweli alikuwa ni muislam na alikuwa anaitwa Chief Abdalllah Mkwawa,na kisa hasa cha kugombana na wajerumani ni kwa sababu wajerumani waliwafukuza wafanyabiashara wa kiarabu ambao alikuwa akiwauzia watumwa na yeye anapewa bunduki ndio kisa kilianzia hapo akawawekea bifu,si yeye tu hata Bushiri aliwekeana bifu na wajerumani baada ya kupiga marufuku biashara ya utumwa.ila wote wa shenzi tu mwafrika peke yake ndio kama malaika.
   
 15. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  kwangu mimi kila mtu ni mjinga ila kwa viwango tofauti.Na ndio maana elimu haina mwisho. ujinga hufutwa kwa kupata elimu.elimu kwa mapana yake hakuna mtu awezaye kuwa nayo yote,ila katika eneo dogo sana una weza kubobea.
  nirudi kwako ZOMBA , you are not organized, hujui unacho taka kuwapa wasomaji wa jf.una mkusanyiko wa masikitiko kutaka kutusadkisha kuwa unacho jua wewe ndio sahihi na anacho jua mtu mwingine hususan aliye soma elimu isiyo na asili ya kiarabu ni mjinga. kiarabu ni lugha kama kikinga, kihaya kihehe, kimakonde,n.k.sasa kama Mkwawa aliandika au kuandikiwa kwa kiarabu does it matter?ni sawa na kuandika kwa kihehe tu.
  USHAURI WANGU
  Jipange unataka kutuambia nini?
   
 16. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Inawezekana Bw. Zomba amesikia hadidhi hii ikitolewa somewhere na yeye akaichukua bila kujiandaa kwa lengo la kuonyesha naye yumo kwenye JF. Mada hii ilivyowekwa ina -reflect mazingira ya wazee waliokuwa wamekaa kupoteza muda bila kujua la kufanya na mmoja kati yao akaona wanataka kuondoka ndiyo akaingiza mada kama hiyo ili wazee wenzake waendelee kuwepo hapo. Vinginevyo hapakuwa na umuhimu wa kuwa na mada kama hii hapa.
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umeshindwa kujibu hata moja, nakuhakikishia siyo saizi yako, viatu havikuingii usilazimishe.

  Sikushangai, unazidi kuainisha Ubaguzi wa Ujinga.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unaendeleza Ubaguzi wa Ujinga huna zaidi.

  Nakuhakikishia hata majina tu ya miji niliyoiandika hapo juu, ingawa unayasikia kila siku, leo unajishangaa kuwa huwezi hata mji mmoja kuutolea maana yake. Unanikumbusha mtu anaejiainisha kuwa yeye ni m-"Bantu", uyapimuuliza hilo neno limetokea wapi? hajui.

  Jee, wewe unajuwa?

  Kama hujui, nakuhakikishia nawe pia ni mdau wa Ubaguzi wa Ujinga.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Katika yote niliyoyaandika hujakutana hata na moja ulijuwalo? basi hata Arusha? Nakuhakikishia wewe ni mdau wa Ubaguzi wa Ujinga. Patamu hapo!
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sikitegemei zaidi ya hicho ulichoandika kutoka kwako, kwani nawe ni zao hilohilo la Ubaguzi wa Ujinga, bora ungekuwa na ubaguzi wa kijinga ningekuona u mueledi. Ni walewale!
   
Loading...