Ni ukweli usiopingika kuwa CCM ni chama kongwe na hawakurupuki ktk maamuzi. We angalia mchakao wa kusuluhisha hili suala la madakitari, ni suala ambalo limefanywa kwa umakini na linaendelea kutatuliwa kwa umakini. Sasa hao kenya tangu waweke upinzani;
- Mwaikibaki na Raila waligombana
- Raila alijilimbikizia mali kwa kuchukua mikataba ya mafuta toka Arabuni,
- Mwaka 2007 wakenya wakachinjana kwa sababu ya uchu wa madaraka wa hao wapinzani
- Na sasa hawataki kuwasikiliza wanachi wanyonge waliowapatia kura na wameamua kuwafukuza kazi!
Je kumfukuza mtu au kumfuta mtu kazi ni suluhisho? si ni ujinga? Kwani serikali ya CCM wasingeweza kuwafukuza ma Dr? Mbona wameamua kutumia njia ya mahakama wakati huo wanaendelea na mazungumuzo! Msiniite kiduku, naomba mtafakari!!
Napata hofu na uwezo wako wa kuelewa na namna ambavyo unatumia mifano. Jaribu kufikiria nchi nyingine ya Afrika ambayo imeweka upinzani na kukatokea machafuko kama ya Kenya. Mimi sitaki kuangalia Kenya walifanya nini hadi wakafika hapo walipo kwa sababu hakuna ambacho tunawazidi Wkenya zaidi ya Ardhi.
1. Elimu wanatuzidi sana, tena siyo kidogo, ni wakenya wangapi wanafundisha shule na vyuo Tz?
2. Ni watz wangapi wanafundisha Kenya?
3. Tz tunabenk ambazo wawekezaji wake ni Wkenya, ngapi Kenya zimewekezwa na Wtz?
4. Uchumi wa Kenya hauwezi kulingalisha na kwetu, tupo mbali sana.
5. Elimu ya uraia Kenya ni kubwa kuliko kwetu, ndio maana bado tunauza viparata vya kura kwa buku.
Inawezekana kweli CCM ni chama kizuri, sina uhakika sana, labda kikipakwa rangi kinaweza kuonekana. Lakini Muonekano wake Tangu alipokiacha Mwl JK 1985 ni tofauti sana na vile ambavyo wengi tulidhani kuwa kingelikuwa. Kifupi serikali na CCM imeshindwa na ili tutoke hapa tulipo tunahitaji chama Mbadala ambacho kitakuwa na maono na mtazamo mpya utakaoendana na hali ya maisha ya sasa. Hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo zinaonesha kuwa serikali ya JK imeshindwa...
1. Angalia hali ya uchumi wa nchi ilivyo mbaya. Rejea malalamiko ya wafanyakazi kucheleweshewa mishahara, angalia ukosefu wa fedha za kigeni na kuporomoka kwa shilingi dhidi ya dola
2.Angalia upatikanaji wa UMEME ulivyo wa kusua sua. Hakuna nchi ambayo imeendelea ikiwa na nishati ya umeme ya kipuuzi kama Tz
3. Angalia Rais wa serikali na CCM yake anavyouza sura kwenye TV akisisitiza watu kuomba risiti punde wanaponunua bidhaa.Hii inaonesha ni kiasi gani serikali ya JK inavyotegemea mapato yake ya ndani kutoka kwenye kodi za walalahoi huku wamiliki wa migodi, viwanda, vitalu vya hifadhi, makampuni ya cm na wawekezaji wengine wasivyolipa kodi na wakiongezewa muda wa majaribio bila kulipa kodi.
4. Hakuna serikali ambayo iliwahi kuwaendeleza wananchi wake kwa kutegemea kodi za kununua na kuuza bidhaa, maendeleo huletwa kwa kutegemea raslimali za nchi. Sisi dhahabu, almasi, tanzanite, gas, misitu, wanayama, samaki na vingine vingi tumeuza kwa wazungu bila kupata lolote.
5. Rais ameshindwa mara nyingi kuwawajibisha aliowateua kumuwakilisha kwenye wizara mbalimbali. Rejea mabomu mbagala, mauaji ya Arusha, mauaji ya Tarime (Nyamongo), kukosekana kwa Umeme na mengine mengi.
6. Kikwete na kabineti yake wameshindwa kukaa na kuelewana ni kipi cha kuongea na wakati gani. rais amegeuka kuwa machinga wa kutembea kila anakosikia kuna kusanyiko la viongozi bila kushughulikia matatizo ya nchi. rejea safari za KIkwete za hivi Karibuni nje ya nchi huku Wtz wakifa kwa mgomo wa mdk.
7.......................................
8.......................................
8.......................................
Siku tukiwa na akili za kuona kuwa tatizo ni CCM na vilaza wake, ndipo tutafahamu ni namna gani ya kujitoa hapa tulipo. vinginevyo, hakuna ambacho kitafanyika kama CCM itaendelea kutawala nchi hii.