Watanzania msiipigie kura CHADEMA 2015

Watanzania msiipigie kura CHADEMA 2015

Ni ukweli usiopingika kuwa CCM ni chama kongwe na hawakurupuki ktk maamuzi. We angalia mchakao wa kusuluhisha hili suala la madakitari, ni suala ambalo limefanywa kwa umakini na linaendelea kutatuliwa kwa umakini. Sasa hao kenya tangu waweke upinzani;
  1. Mwaikibaki na Raila waligombana
  2. Raila alijilimbikizia mali kwa kuchukua mikataba ya mafuta toka Arabuni,
  3. Mwaka 2007 wakenya wakachinjana kwa sababu ya uchu wa madaraka wa hao wapinzani
  4. Na sasa hawataki kuwasikiliza wanachi wanyonge waliowapatia kura na wameamua kuwafukuza kazi!
Je kumfukuza mtu au kumfuta mtu kazi ni suluhisho? si ni ujinga? Kwani serikali ya CCM wasingeweza kuwafukuza ma Dr? Mbona wameamua kutumia njia ya mahakama wakati huo wanaendelea na mazungumuzo! Msiniite kiduku, naomba mtafakari!!

aliyako haina tofauti na ya punda
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!

acha upuuzi wako,ishawishí familía yako.hakuna atakayeuzima moto wa chadema.
 
[h=1]Ahadi za Kikwete:
1. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa.
2. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchiya Misenyi
3. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi
4. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba
5. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma
6. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda
7. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvumakuunganishwa katika gridi ya taifa
8. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu
9. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino
10. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba
11. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
12. Serikali kulisaidia vyama vya ushirika
13. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa
kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu
14. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani
15. Kulinda muungano kwa nguvu zote
16. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa
17.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa
18.Kujenga bandari Kasanga mkoani Rukwa
19.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo
20.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira
21.Kuzuia hatari za kisiwa cha Pangani kuzama
22.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini
[/h]
 
Mtoboasiri, sikiliza! Ukilinganisha upiznani wa hizo nchi ni stable, hwezi kulinganisha na upinzani wa TZ ambao wamejaa njaa (mfano David Kafulila alikuwa na haja gani ya kupiga magoti na kulia ili asamehewe?) na CHADEMA ni chama kilicho jaa migogoro ya hapa na pale, labda kikiundwa chama kingine chenye mlengo na dhamira ya dhati ya kusikiliza matatizo ya watanzania walio wengi na kisiwe na migogoro

kama issue ni migogoro ya hapa na pale kwa chadema sasa kwa ccm tusemeje? pasipo na migongano ya kifikra basi ujue hakuna maendeleo ya dhati, mbaya zaidi hao ccm migogoro yao ni mikubwa kiasi wamefikia sehemu njia yao ya kutatua migogoro ni kuuana na kuwekeana sumu, sasa nani ananafuu? si heri ya hao cdm.
 
Angekuwepo Sadam Hussein Ng`wanakidiku ningejua pa kukupeleka... Huna aibu wala uzalendo fisadi mkubwa wewe... Nenda na CCM yako nyumbani hatuitaki...

Hospitali hazina dawa
Utalii wa nchi upo kwa wageni
Madini kwa wageni
Shule ni aibu tupu
Vyuo ndiyo balaa
Viwanda vimekufa
Thamani ya shilingi inazidi kushuka
Mfumuko wa bei

Kweli haya yote bado unataka CCm???

Shame on You...
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!

Naona kama umechanganyikiwa vile,hivi unaijua Kenya unayoisema au unaisoma kwenye magazeti na tv tu.
uliloliona wewe ni moja tu la kufukuza wafanyakazi? unajua Kenya nchi ina umeme sasa zaidi ya 80%,vijiji vingi
vina maji ya uhakika.Nairobi mji umebadilishwa barabara nyingi zina fly over za magari na za miguu.linganisha
na miji yenu na nchi yenu fly over moja nchi nzima tena ya miguu-Manzese. Pia umesahau nchi nyingi za
Afrika zinaongozwa na upinzani na ziko mbali kama Ghana,Zambia,Cape Verde nk.
Watanzania si Maboga kama mnavyojidanganya,wameamka umechelewa kuleta huu udanganyifu wako.
 
Are you compaigning for ccm? Tupa mada zenye akili, think critically and argue logically.
 
Magamba wamekutuma na sijui wanakulipa bei gani!!!!!!!!!!!!! CCM imechoka na uwezo wa kufikiri umefikia kikomo, chama bado kina viongozi kama kina Wasira, what a shame. screw CHAMA CHA MAGAMBA
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!

Ni kawaida yenu magamba, waambie wale mnaonufaika na wizi wa EPA, mliogawiana nyumaba za serekali, wageni waliofanya TZ shamba la bibi, wanaonufaika ufisadi nchi hii, wale wa Rada, Meremeta, Tangold etc.... ndiyo wasiichague CDM.

Lakini waTZ wa kawaida hesabu kuwa imekula kwako.... Hata muwape pesa na misaada ya hali na mali, hata muwajengee misikiti na makanisa 2015 lazima mhame nchi hii maana wengine toka mmezaliwa hamjawahi kukosa mboga nane..
 
Angekuwepo Sadam Hussein Ng`wanakidiku ningejua pa kukupeleka... Huna aibu wala uzalendo fisadi mkubwa wewe... Nenda na CCM yako nyumbani hatuitaki...

Hospitali hazina dawa
Utalii wa nchi upo kwa wageni
Madini kwa wageni
Shule ni aibu tupu
Vyuo ndiyo balaa
Viwanda vimekufa
Thamani ya shilingi inazidi kushuka
Mfumuko wa bei

Kweli haya yote bado unataka CCm???

Shame on You...
Pamoja na hayo, lakini kumbuka kusajili T2015CCM. Hii ni changamoto kwa vyama vya upinzani wakae mkao wa kuwa watawala na siyo kugombania madaraka na uchu wa madaraka.
 
Ng'wana unautapiamlo wa mawazo sio bure! Na nina imani kuwa wewe sio mtanzania ndio maana umekurupuka kubadili mapungufu kuwa mafanikio. Lakini labda ngumbalo ndio maana unadumisha mawazo ya mwenyekiti lkn hata kingunge hana fikra hzo cku hizi naye anajitahd kuona mbali kwa upepo wa kisasa. Take care mawazo hayo yanawaharibu watoto wako!!
 
Nkhana namhala nagabhona amashi gako! Matare gandekhile T2015CCM!!!

Thetehetehetheteeeeeeee hujatulia wewe umekunywa vodka asubuhi........watolaga bhosiga namhala.......ndoho tabu olo e ccm yako yandikilwe amshi gane..........
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!

Kwa hiyo utafiti wako umefanyia kenya tu, mbona hujageuka na kuangalia Malawi, Ghana,Zambia.
 
Kwa Afrika ni nadra upinzani kuleta maendeleo. Mfano halisi angalia Kenya ambapo hao raia waliouweka upinzani madarakani uliwasbabishia matatizo makubwa na hatimaye umefikia hatua ya kuwafukuza wafanya kazi wa sekta ya afya. Hii haikubaliki, mfano tizama jinsi chama cha mapinduzi kinavyo fanya mambo kwa kufuata sheria na ni chama kivumilivu. Nasaha zangu, watanzania msibabaishwe na vyama vya upinzani. Tujenge nchi na CCM!!

Nadhani ingalikuwa vyema ungefanya tathmini ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwa mwaka huu mmoja wa uongozi (achilia mbali miaka 50 ya uhuru) na ndipo ungekuja na wazo hili. Na pia ungekuwa na nafasi nzuri sana ya kuja na wazo hili kama ungekuwa na ufahamu wa kina wa msingi wa matatizo ya siasa za nchi ya kenya. Huwezi kulinganisha kwa ulinganifu ulio sawa kwa siasa hizi. Nafikiri hizi zote ni mbinu za kukipatia chama chako popularity wakati wananchi weshafunguka na si kama zamani ambapo kila kitu waliona sawa.
 
Back
Top Bottom