Watanzania KWAHERINI YA KUONANA.

powa bwana Msando kila la heri bwana na ninakupromise kabla hujaondoka huu utawala dhalimu wa RA na EL wakiwa wamemuweka kijana mmoja mtanashati awafungulie milango ili waliibie taifa tutakuwa tushautoa madarakani, Mungu ni yule yule aliyemtokea Musa, kwenye kijiti cha moto na ni yule yule aliyewapa moyo wa ukakamavu vijana wa misri mpaka tapeli Mbaraka akakimbia, ni huyo huyo aliyetupa moyo mpaka tukalinda kura za wenje Mwanza
Naamini ni huyo huyo atatupa nguvu ya kuutoa utawala wa remote controlled nchini Mwetu, PEOPLE'S ........., power..........
 
Haondoki mtu hapa, wale mliokuja kwa kampeni za 2010 ondokeni mtuachie jamvi letu, sie tutabanana humu humu mpaka kieleweke!

Hapa ni JF Where We Dare Talk Openly, uondoke utazungumzia wapi tena? si umesikia kwenye hivyo vyama vya siasa ni FITNA tupu? kwanza hiyo 'addiction' ya JF ambao ndio ugonjwa wa wengi wetu humu dawa yake uataipata wapi?

Kazi kweli kweli! I like that haondoki mtu hapa mpaka kieleweke!
 
Unaaga kwa maana ya kuondoa uanachama wako wa JF ama una maana kwamba hautachungulia humu?Wtu ambao wanaaga humu JF huwa nawashangaa sana kwasababu huwa sielewi wanauaga umemberships ama utumiaji wa foruma hii,kama unaweza kunijibu sawa,kama huwezi,basi bye bye,shughuli njema huko uendako ie membership wise or visitation wise.
 
Kwahiyo umekubali kushindwa kirahisi hivyo?
Roho ya mpiganaji siku zote haitakiwi kukata tamaa.
 
Mkuu MsandoAlbert.
Nchi mbili zinahitaji watu kwa haraka.
Libya na Sudan ya Kusini.

Lakini mwanaharakati kama wewe kwa nini unakimbia vita? Lengo ni kutumikia wanyonge au kutunisha mfuko wako?
Well, kwa kawaida walalahoi hupigania uhuru,haki,huandamana,huumizwa na kuuawa lakini wanaongia katika uongozi ni wale wanaosubiri viyoyozi maofisini mwao na wenye kutumia ndimi zao kupanga maneno matamu.

Iwavyo vyovyote..unapoaga unatoa ujumbe gani kwa wale waliokuchukulia wewe kama tegemeo lao.Mtu uliowapa moyo kuwa "there is light at the end of the tunnel!". Unawakatisha tamaa.

Hata kama hujakusudia kuondoka au kuwakatisha tamaa wananchi wanyonge, unaelewa kuwa ufahamu wa watu unatofautiana sana na si wachambuzi wanaozama ndani na kuona kuwa machungu unayoyasikia hasa unapoitazama nchi yenye utajiri wa asili lakini imo ndani ya shimo la umasikini ,unayohaki ya kuielezea hali hiyo katika lugha unayoichagua mwenyewe.

Wengi wa wasomaji watafahamu kuwa mwanaharakati tunayemtegemea anatupa manyanga na kujiondokea. Andika katika lugha nyepesi inayofahamika kwa kila mwananchi wa kawaida ili wasije kuufahamu"MUAGO" wako, kuaga kwako kuwa mambo yamekushinda ,kinyume ya makusudio yako. Utawakatisha tamaa.
 
SHUJAA hakimbii vita!
Komaa humuhumu kiongozi!...Mbona unakimbia wakati kazi ndio inaishia?...
UKIRUDI utajisikiaje utakapokuta wanaume tulishawagaragaza mabeberu?
Waza na kuwazua kiongozi!

PakaJimmy,

Nashukuru. Angalau nafarijika kwamba kwa kuaga kwangu makamanda mmeonyesha wazi kwamba mnaweza kumuokoa yeyote anayetaka kurudi nyuma. Wangeaga wasingejikuta huko walipo. Siku ya mwisho watajuta kwa nini waliondoka kimya kimya! Tupo Pamoja.
 
Asante kwa ujumbe wako hakika ukiusoma vizuri utasikitika napengine ukakurupuka kujibu kumbe unacho kijibu sicho….
 
Kwahiyo umekubali kushindwa kirahisi hivyo?
Roho ya mpiganaji siku zote haitakiwi kukata tamaa.

Sijakata tamaa kamanda, kama kuondoka kwangu mpaka watoto wamalize elimu ya MEM si tutakuwa tumemaliza vita? Hawa jamaa ni watu wa kumaliza MKUKUTA n MKURABITA leo? Tuko Pamoja.
 
SHUJAA hakimbii vita!
Komaa humuhumu kiongozi!...Mbona unakimbia wakati kazi ndio inaishia?...
UKIRUDI utajisikiaje utakapokuta wanaume tulishawagaragaza mabeberu?
Waza na kuwazua kiongozi!

PJ, hebu msome jamaa tena vizuri utaelewa maudhui yake. Sidhani alimaanisha ulivyo respond...especially anaposema anasubiri vitu fulani alivyolist! when are those things going to happen so sidhani kama anakimbia vita, ni kwamba anataka kuleta ujumbe fulani....just read it again! Unajua wana fasihi ni wengi!
 
Asante kwa ujumbe wako hakika ukiusoma vizuri utasikitika napengine ukakurupuka kujibu kumbe unacho kijibu sicho….

Crashwise,

Nimegundua huwa tunasoma heading halafu tunajibu bila kusoma thread nzima. Yale unayolalamikia sasa yanajidhihirisha. Kuna tatizo. Tuanze kusoma kila kitu (isipokuwa yale ya uzushi na yenye lengo la kutuondoa kwenye mstari) na kuelewa kabla hatujagonga 'reply'.

Naomba tulisimamie wote.
 
Unaaga kwa maana ya kuondoa uanachama wako wa JF ama una maana kwamba hautachungulia humu?Wtu ambao wanaaga humu JF huwa nawashangaa sana kwasababu huwa sielewi wanauaga umemberships ama utumiaji wa foruma hii,kama unaweza kunijibu sawa,kama huwezi,basi bye bye,shughuli njema huko uendako ie membership wise or visitation wise.

Jmushi,

Soma tena kamanda. Angalia tena kwa nini sijasema naaga nini. Nitakuwepo mpaka wayamalize waliyoahidi. Watamaliza? Tuko pamoja kamanda.
 
Son of Peasant,

Ndio maana nikasema wapo waliondoka bila kuaga wakakosa nafasi ya kushauriwa. Sasa hivi wanaungana kuandamana kupongeza hotuba na maneno Amani yetu tunaipenda! Wengine wanakurupuka eti CDM wachawi wa upinzani. Afadhali nimeaga ndugu zangu mmenishauri wengine mmenionya, wengine mmenikumbusha, wengine mmenitia nguvu! Wao walikosa nafasi hii. Nabaki.

Nilishangaaa. Unajua hurka zote za wapiganaji zinafanana!! Mpiganaji hawezi kutupa chini bunduki kirahisi na kukimbia, ingekuwa rahisi namna hiyo Gadaffi angekuwa ameishasahaulika kam Ben Al na Mubarak lakn yeye ni mpiganaji hawezi kukimbia kirahisi. Nawe ni mpiganaji sasa uende wapi, ukajisalimishe? Kwa nani?
 
Kimbunga,

Wenzetu wamejisalimisha. Wamefika huko wamepewa kazi za upishi na upagazi. Wengine ni matarishi. Wanaamini kwamba wako salama. Wanasahau kwamba vita haijaisha na tunaelekea kushinda. Wakijisalimisha kwetu sijui watakuwa nini?
 
Kwenye safari ndefu na yeye kundi kubwa la watu, kuna kila tabia, kuna wenye tabia za mbu, mchwa, chawa, mende, kunguni na nyinginezo nyingi sana...............

Kamanda, umemaliza. Maneno haya nitayakumbuka daima na kuwakumbusha wengine!! JF isonge mbele!
 
Naamini kama nimekupata.
Nafikiri wengi mwanzoni hatukuelewa ila sasa nimeelewa kwamba unakumbusha yale tupaswayo kuyasimamia na kutekelezakwa ajili ya safari zetu za kufika pale tunapo patamani.(TANZANIA BILA MIZENGWE) Asante kwa kutukumbusha yale tunayo takiwa kufanya ili tufike mapema. Na kwamba bila kushughulikia wenyewe tukaendelea kusubiri safari haitakuwepo milele.
 
Kimbunga,

Wenzetu wamejisalimisha. Wamefika huko wamepewa kazi za upishi na upagazi. Wengine ni matarishi. Wanaamini kwamba wako salama. Wanasahau kwamba vita haijaisha na tunaelekea kushinda. Wakijisalimisha kwetu sijui watakuwa nini?

Waaache wakapike, wakabebe mizigo, wakawe midomo ya mabwana wanaowatuma, wakapeleke jumbe mbalimbali kama matarishi. Kuna siku watakuja huku wanatembea kwa magoti, hatutawachinja tutawambia inukeni nendeni zenu mmepona.
 
Dah! Samehe mara saba sabini! Ila nafsi zao zitawasuta. Wengi wataenda kujirusha kondeni na matumbo yao yatapasuka. Ndege wa angani watasheherekea!
 
Mashori wanafanyaje tena? Wmo humu kumbuka, hebu niambie.

Ila hiyo Nabaki imesema nabaki wapi? Na je nilisema naondoka naenda wapi? Ni lini natakiwa kuondoka?

Kwa kheri ya kuonana mkuu si bado tunagangamala wenye mioyo miepesi wanaondoka wanarudi tena kuchungulia.

Mungu akutangulie huko uendako.
 
Son of Peasant,

Ndio maana nikasema wapo waliondoka bila kuaga wakakosa nafasi ya kushauriwa. Sasa hivi wanaungana kuandamana kupongeza hotuba na maneno Amani yetu tunaipenda! Wengine wanakurupuka eti CDM wachawi wa upinzani. Afadhali nimeaga ndugu zangu mmenishauri wengine mmenionya, wengine mmenikumbusha, wengine mmenitia nguvu! Wao walikosa nafasi hii. Nabaki.
Now your talking like a big man.
 
Back
Top Bottom