Watanzania KWAHERINI YA KUONANA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania KWAHERINI YA KUONANA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MsandoAlberto, Mar 18, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu Zangu,

  Ni matumaini yangu kwamba mu-wazima kwa kujiangalia. Natambua kutokana na sababu nitakazotoa baadae si rahisi kujua kama wewe ni mzima au la. Hata waliotoka Loliondo wanasema 'wamepata nafuu'.

  Mimi namshukuru Mungu nimeweza kuwasha simu na kufungua jamvi letu siku ya leo. Namshukuru Mungu kwa sababu ina maana simu yangu ina charge na nina salio. Pia kwa sababu simu yangu inafaa kwa matumizi ya internet.

  Wengine watahoji, sasa Albert, wakumshukuru si Raisi wako wa nchi na serikali? Inakuwaje tena unamshukuru Mungu? Sababu zitajulikana.

  Ila, kuwaka kwa simu yangu kila siku kunanikumbusha aidha kimoja kati ya hivi au vyote, UMEME na MAFUTA. Haiwezi kuwaka bila kuwa na charge. Siwezi kucharge bila UMEME au MAFUTA ya generator. Hasira kumbe zinaanzia mara tu ninapowasha simu.

  Ndugu zangu, hali hii ni ya kila siku. Kila siku iendayo kwa Mungu. Sasa nitawezaje kumshukuru Raisi wangu? Namshukuru Mungu kwa sababu HASIRA zangu zinabaki kuwa hasira, UVUMILIVU unachukua nafasi kubwa zaidi.

  Kama HASIRA zinasababishwa na Raisi wangu UVUMILIVU napewa na Mungu siamini kama nakosea kumshukuru.

  Yeye aliyetuumba alituagiza tuheshimu na kutii mamlaka za nchi. Ndio maana anatupa UVUMILIVU.

  Lakini, HASIRA zikizidi kutokana na hali kuwa ile ile kila siku UVUMILIVU si unapotea?

  Mhhh! Nimekumbuka. Mtu mwenye NJAA ni mtu mwenye HASIRA. Ukimwangalia anaweza akakubwatukia 'unamwangalia nani'? Amesahau unamwangalia yeye. NJAA.

  Nadhani imetosha kusema kwanini namshukuru Mungu na sio Raisi wa nchi kwa simu yangu kuwaka leo asubuhi.

  Madhumuni ya ujumbe wangu wa leo ndugu zangu ni kuwaaga. Kwa herini ya kuonana.

  Ndugu zangu, UVUMILIVU umefika mwisho. HASIRA zimezidi. NJAA imepitiliza. Usalama wangu mwenyewe na wale wanaonizunguka uko mashakani.
  Wao wana hali kama yangu hakuna wa kumfariji mwenzake.

  WanaJF, mtakubaliana nami kwamba tulikuwa na wenzetu, wengi tu humu jamvini ambao tulifanana. Lakini UVUMILIVU wao ulipofika mwisho na HASIRA zao zilipozidi na NJAA zao zilipopitiliza wametuacha.

  Sasa hivi wanatubeza. Wengine wanatuonya. AMANI na UTULIVU. Wengine wanasema sisi WACHAWI wa upinzani. Wengine wanasema hatuipendi nchi yetu kisa hatukatiwi umeme na hatujui kero hiyo.

  Ni wengi mno jamani. Wao wameondoka bila kuaga. Naamini kama wangeaga wangeshauriwa. Wangefarijiwa na kutiwa moyo wawe na SUBIRA hata kama UVUMILIVU umefika mwisho na HASIRA zimezidi.

  Wakatudanganya. Ooh, nipo 'around' 'nachekicheki mazingira hapa nje'. Tumeendelea kuamini kwamba bado wapo. Kumbe walishaondoka siku nyingi wametuachia kichungi cha sigara juu ya meza kutuaminisha kwamba bado wapo.

  He! Namshukuru Mungu tena. Kumbe kichungi cha sigara huwa kinazimika. Kimezimika sasa tunajua hawapo tena. Walishaondoka. Ule moshi ulikuwa geresha tu. Mungu mkubwa.

  Sasa hivi tunawasikia majukwaani. Kwenye vyombo vya habari. Wanatoa matamko. Wanawasemea wenye HASIRA, NJAA na waliokosa UVUMILIVU. Wanachosema sio kile cha hao wanaowasemea.

  Sasa, nani anatishia AMANI na UTULIVU? Kila mwenye akili timamu atapatia jibu la swali hilo.

  Basi jamani, nisiwachoshe. Mimi naaga. Imetosha naenda zangu. Niko kwenye hatua za mwisho kuuza kilicho changu niende zangu kusikojulikana. Ninachosubiri ni vitu vifuatavyo kabla sijaondoka;

  1. Kitambulisho cha Taifa

  2. Cheti cha Umilikaji Ardhi kijijini kwangu - MKUKUTA, MKURABITA nk.

  3. Matokeo ya vijana wangu baada ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari - MEM n.k

  4. Kipimo na ripoti ya daktari kutoka kituo cha afya cha Kata. Tunasubiri maabara ikamilike, mpimaji amalize kusoma na vifaa vinunuliwe.

  Katiba na malipo ya Dowans sitasubiri. Mimi si mrushi, najua kama mwananchi hata kama sikufaidika sana na umeme waliozalisha Dowans mchango wangu si zaidi ya elfu 5 kwani tupo Mil. 38+. So nitamkabidhi Mtendaji Kata sh. 5,000 kabla sijaondoka.

  Vinginevyo kwaherini ya kuonana. Mkumbusheni Raisi kuhusu maneno yenye herufi kubwa asijidanganye na maneo yaliyo kwenye mabano;

  NJAA (eti mwana malegeza) .

  HASIRA (eti hasara).

  UVUMILIVU (eti huleta mbivu).

  SUBIRA (eti ya vuta heri).

  Pia, sio wote wataamua kuondoka kama mimi. Wengi watabaki. PATATOSHA kweli?

  Wasalaam,

  AGM.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  SHUJAA hakimbii vita!
  Komaa humuhumu kiongozi!...Mbona unakimbia wakati kazi ndio inaishia?...
  UKIRUDI utajisikiaje utakapokuta wanaume tulishawagaragaza mabeberu?
  Waza na kuwazua kiongozi!
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kaka kwa hayo unayosubiri nadhani hadi kieleweke ndio uondoke si leo wala kesho!!! TUPO PAMOJA
   
 4. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 20,391
  Trophy Points: 280
  Umekata tamaa mkuu!? Kitambulisho ndo kwanza tumetangaza nafasi za ajira, hospitali ya kata jengo la maabara lipo ila vifaa/samani za maabara ndo tumeitisha tenda, subiri. Tena wala usiuze kila unachokimiliki hata kama una hakika ya kuondoka, hapa ndo kwenu na kmbio zako kuondoka haziwezi kurekebisha hayo uliyokumbushia. Cha muhimu, tulia angalia namna gani tutakabiliana na changamoto hizi, hatupaswi kuishi kinafiki hata kama tunajiona ni waoga wa kukabiliana na ufisadi na unyanyasaji w kitabaka.

  Umeandika vizuri Guru, nimekugongea
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nilianza kulia, lakini nimesoma mara mbili, angalao nimeridhika nimefurahi kuwa utakuwepo mpaka Vitambulisho vya Utaifa vitoke, umenifurahisha kuwa tutakuwa wote hadi waanze kutoa vyeti vya Kumiliki ardhi kijiji kwako, Nimefarijika zaidi kuona kuwa tutakuwa wote hadi wanao wamalize elimu ya Msingi na Sekondari, nimefurahi mno, kuwa utashiriki kuona kata yako inapata Maabara na kituo cha afya.

  Kilicho nifariji hapo ni kitu kimoja tu! "Tutakuwa wote kwa muda mrefu" basi hakuna kingine.

  Changamoto iliopo ni kukutumia vizuri kabla hujaondoka maana umeaga. Nakuomba tafadhali sana muda wote utakapo kuwa nasi kabla ya kutokomea husifanye kazi kama mtu anayeondoka, husitutenge kama si wenzako tena, eti kwasababu umekwisha kuaga kutoweka.

  Natumaini baada ya kukamilika hayo mambo manne unayosubiri, Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema, unaweza kupata ufunguzi mwingine na kufikia vinginevyo, tunakuhitaji sana, tunakutegemea pia.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Unataka kutuambia silaha zote umeshindwa kuzitumia,punguza kulalama,fanya kweli kwa sababu ukingoja kama unavyodhani itakuwa rahisi ukweli utangoja mpaka kiama njia ni moja tuu chukua hatua sasa,na saa ya ukombozi ni sasa
   
 7. m

  mja JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli tupo pamoja,mpaka hayo unayosubiri yatime, utakuwa umeshondoa wazo , na utaendelea kuwa mpiganaji hapa hapa JF, welcome back before going
   
 8. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Haondoki mtu hapa, wale mliokuja kwa kampeni za 2010 ondokeni mtuachie jamvi letu, sie tutabanana humu humu mpaka kieleweke!

  Hapa ni JF Where We Dare Talk Openly, uondoke utazungumzia wapi tena? si umesikia kwenye hivyo vyama vya siasa ni FITNA tupu? kwanza hiyo 'addiction' ya JF ambao ndio ugonjwa wa wengi wetu humu dawa yake uataipata wapi?
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  fasihi sikusoma lakini nimefurahia utunzi wako!
   
 10. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Albert ndugu yangu
  Usikimbie when the going gets tough...the tough gets going!
  Shupaa kiume
   
 11. N

  Ntandalilo Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  . Kitambulisho cha Taifa

  2. Cheti cha Umilikaji Ardhi kijijini kwangu - MKUKUTA, MKURABITA nk.

  3. Matokeo ya vijana wangu baada ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari - MEM n.k

  4. Kipimo na ripoti ya daktari kutoka kituo cha afya cha Kata. Tunasubiri maabara ikamilike, mpimaji amalize kusoma na vifaa vinunuliwe.


  Umeandaa shilingi ngapi upate vyote hivi mapema?............Kaa tukomae wote mkuu! mbona tumeshapita wote kule kwa kukimbia na kutembea kwa kasi pamebaki mahali pafupi pa kutambaa tufike????.................
   
 12. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  vita hivi si vya damu na nyama.
   
 13. p

  paulk JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe wala huondoki, ni maneno tu maana anayeondoka huwa haagi
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  safari njema wasalimie huko uendako.
   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Sasa nimegundua kweli una mapungufu,huu sio wakati wa kufyata mkia na kurudi nyuma huu ni wakati wa mapambano na kusonga mbele,unajisikiaje dada zako,mama zako na wanao wanapopigania haki na wewe unakunja mkia kama wale wanyama tunaowafugaaga nyumbani ???
   
 16. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Msando ndugu yangu

  Muda wa kuondoka bado sana, hatuwezi ondoka bila kupata suruhisho na hitimisho la matatizo yetu, kuondoka mapema ni kukata tamaa na kuwaogomba, hatuna budi kupambana na mpaka mwisho wa safari, najua kuwa safari ni ndefu na ina milima na mabonde mengi, lakini hatuna budi kuendelea na safari kwani tumekwisha amua kuoga na nguo tumevua so hatuna budi kuoga.

  Kwenye safari ndefu na yeye kundi kubwa la watu, kuna kila tabia, kuna wenye tabia za mbu, mchwa, chawa, mende, kunguni na nyinginezo nyingi sana, lakini ndani ya safari ndiyo tunazidi kujuana nani ni nani?, yupo serious kweli na safari, au anabahatisha, au siyo mwezetu, n.k so hatutakiwi kukata tamaa kwa sababu eti mbele ya safari yetu tumekutana na simba mla watu, wala eti kwa sababu kwenye mto tunavuka kuna mamba wengi wala watu la hasha, ndiyo muda wa kujipa moyo na kuongeza juhudi ili tufike, hakika safari ina vikwazo vingi lakini lazima tufike.

  Naamini kuwa siyo wote watafika mwisho wa safari, kuna wengine lazima wataishia njiani kwa sababu mbalimbali na visigizio vingi sana, kuna wale ambao watukuwa wasalati na kununuliwa na adui, kuna ambao wataogopa nguvu za adui, kuna ambao adui atafanikiwa kuwateka na kuwaagambiza etc, lakini uamuzi ni wako kusuka ama kunyoa, kuwa msaliti au kufa kifo chenye heshima mbele ya safari, hakika safari ni ndefu na ina mambo mengi.

  Mimi nitaendelea na safari mpaka mwisho, simuogopi adui hata kama ana nguvu kiasi gani, na kuomba na wawe pia uwepo katika safari hii ili tumalize na kusheherekea pamoja, adui yupo mikononi mwetu na anaendelea kutapatatapa, huku akiwatumia wezetu ambao tulizani wapo imara kuliko sisi, kumbe ni waoga kama panya na wajinga kama kuku, ipo siku lazima adui akisha maliza kuwatumia atawagamiza na kuwajichilia mbali.
   
 17. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Son of Peasant,

  Ndio maana nikasema wapo waliondoka bila kuaga wakakosa nafasi ya kushauriwa. Sasa hivi wanaungana kuandamana kupongeza hotuba na maneno Amani yetu tunaipenda! Wengine wanakurupuka eti CDM wachawi wa upinzani. Afadhali nimeaga ndugu zangu mmenishauri wengine mmenionya, wengine mmenikumbusha, wengine mmenitia nguvu! Wao walikosa nafasi hii. Nabaki.
   
 18. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Walisema " East or West, home is the best"

  Tuliondoka (bila kuaga), tumerudi, JF is home.

  Mtu hafukuzwi "kwao"

  Huondoka kwa "muda tuu"

  Mapambano yanaendele

  Saa ya ukombozi "imewadia"

  Haikwepeki hata kwa "kikombe cha babu"

  Mjenga nchi ni mwananchi

  Tumejipanga kuchukua nchi yetu!
   
 19. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  MSANDO, hapo kwenye red, jibu lake liko straight sanaa, PATAKUWA PADOGO SANA!
   
 20. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  kwa vitu unavyosubir ni matumain yang utazeeka na kufia hapa hapa kwetu. unless uwe mstari wa mbele kudai haki onyesha nia ila kwa kunhea bila vitendo haaaaaaaaaaaaa tutakufa tutaviacha kama babu zetu na hela E.A
   
Loading...