Watanzania huu msemo wa 'Sisi Waafrika' unatudumaza, achaneni nao

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Tumesikia au tunawasikia sana viongozi wetu wakijinasibu kwa Uafrika, aidha utawasikia wakisema sisi Waafrika, yaani wanaona shida kubwa sana kusema sisi Watanzania au kwa Utanzania wetu bora hata Wa upande wa pili utawasikia wakisema sisi WaZanzibari au Uzanzibari wetu.

Viongozi hivi mnatafuta huruma maana msemo huu wa Sisi waAfrika hutumiaka hapa Tanzania tu, nikimaanisha kwenye mikutano yetu iwe ya kichama au ya kiTaifa.

Nimekuwepo nchi za magharibi na kaskazini ya Afrika, sijawasikia kutumia msemo huu wa sisi wa Afrika, wanatumia kiwao kwa mujibu wa jina la nchi, hawajiunganishi kama sisi hapa, yaani hata kwenye mikutano ya mitaani utawasikia sisi wanavijiji wa Afrika, sisi watu weusi hivi waafrika wote ni weusi?

Kasumba hii ni mbaya sana na inatudumaza na ndio ukaona hatuendelei tumebaki paleplae sisi ni waafrika kutawaliwa ndio asili yetu, ndio utamaduni tuliokulia nao hatuoni mbali tupo paleplae sisi ni Waafrika.

Embu viongozi badilikeni msitudumaze na kutuwekea miguu ya shingo mpaka tunashindwa kupumua ,sasa sisi si waafrika tena sisi ni Watanzania, huwasikii waPakistani wakisema sisi waAsia au wa bara hindi ni sisi wapakistani yaani nchi za mabara yote huzisikii wakijinasibu kwa bara lao kusema sisi wa ulaya au sisi wa marekani kusini nakadhalika.

Na humu Afrika ni sisi waTz tu tulio na hashuo la kujiita au kujinadi sisi waafrika, hivi ni aibu kusema sisi waTanzania? Jamani kila mtu anabeba mzigo wake, hatuwezi kuibeba Africa tutazidi kudumaa kuna waTunis, Wamisri wa Moroco wa Aljeria huwasikii kusema sisi waafrika viereje sisi tu tumekwama palepale sisi wafrika? Huu ni ushamba!
 
Na katika wimbo wetu wa Taifa tusianze na; "Mungu ibariki Afrika--", bali tuanze na; Mungu ibariki Tz---"

Wasemaje??🤔
 
Sisi ni waafrika tunaoishi Tanzania. Tanzania ni sehemu ya bara la Afrika. Kama hutaki, pole.
Sisi ni waTanzania tunaoishi Tanzania ,kilugha kinakupiga chenga Kila Mtanzania sio Muafrika lakini pia sio kila Muafrika ni Mtanzania.

Itakuwa wewe ni wa kutokea milima ya Congo.

Utasemaje sisi waafrika katika mikutano ya ndani iwe bungeni au kwenye uwanja wa wazi,mkutano wa chama au kiserikali,hapaaaaanaa tujinasibu kwa kusema sisi waTanzania na sio sisi wa Afrika, kwani si kila Mtanzania ni Muafrika kuna wazungu waarabu wahindi wapemba.
 
Usipakatae kwenu!

Jitambulishe watu wakujue! Jioneshe! Jitangaze!

Hata watu wa mabara mengine pia hujitambulisha kulingana na mabara yao.

Ni kawaida tu, wala usiogope!
 
kwa kupitia fiikra kama hizo ndio mana tumekua maskini wakutupwa kutokana na ujinga uliotujaa.
 
Waafrika tunafanana mambo mengi sana tofauti na wazungu
 
Waafrika tunafanana mambo mengi sana tofauti na wazungu
Itakuwa mmedumazwa na mawazo mgando,katika hii Afrika kuna nchi ukienda ukiitaja Tanzania watakuuliza iko bara la Asia, yaani mtu anakuuliza wewe unatokea nchi gani unamwambia Tanzania ,jambo la kwanza anashangaa.
Sisi wa Afrika itumike kwenye OAU na sio UN ,kasumba ya kuona watu waafrika wote ni weusi. Pale Arusha kuna sehemu wananchi wake ni weupe pepepe utaona ni waarabu tu lakini wapi ni WaTanzania na hata kule kondoa kuna wale wa Rangi nao unawaonaje ?

Na jitu ukilisikia linapenda kujisema au kujilabu kwa kinogesho cha Sisi wa Afrika basi usifikiri anamaindi sana uafrika ,hapaaana kwenye akili yake kuna superglues clue kuwa Waafrika ni watu weusi , Mbona India kuna wahindi weusi kushinda lami na hawana asili hata chembe ya kutokea bara la Afrika.

Unaona shida gani kusema sisi WaTanzania au unaona aibu ? Kuonekana wewe ni Mtanzania,nimepita nchi nyingi za Afrika na kuhudhuria au kuangalia mikutano yao hawatumii..sisi wafrika.. hata hapo Kenya hawatuumi ulaghai huo,ukisikia jitu linasema sisi Waafrika na kutoa mijicho kama yuwanya kutu ngumu, mjue huyo ni laghai.

1627531063196.png
1627531643933.png

1627531672494.png
 
Wewe kilaza Warangi na Wambulu ni watu weusi.

View attachment 1872382View attachment 1872385
View attachment 1872386
 
Back
Top Bottom