Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 47,010
- 32,443
Wanabodi,
Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).
Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.
Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.
SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012