Watanzania 25 watimuliwa Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania 25 watimuliwa Kenya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 8, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA 25 wamefukuzwa nchini Kenya tangu kuanza kwa mwaka huu baada ya kumaliza kutumikia vifungo kutokana na makosa mbalimbali ya kiuhamiaji yakiwemo ya kuishi nchini humo bila kuwa na vibali.

  Hayo yalisemwa jana na Ofisa Uhamiaji Mfawidhi, Frederick Kiondo wa kituo cha uhamiaji cha Holili-Himo mkoani Kilimanjaro wakati akimweleza Mkuu wa Mkoa huo taarifa fupi ya namna kituo hicho kinavyofanya kazi.

  Kiondo alisema licha ya Watanzania hao kufukuzwa nchini humo pia kuna wageni kutoka nje ya nchi waliokataliwa kuingia nchini Tanzania kwa kipindi hicho hicho cha mwaka 2011 kwa sababu mbalimbali.

  Alisema kati yao, wapo Wakenya wanane wenye asili ya Somalia ambao walizuiliwa kuingia nchini kutokana na kutokujua lugha ya Kiswahili wala Kiingereza.

  Aliongeza kuwa, walizuiliwa Waethiopia watano kutokana na kutokuwa na viza rejea, Wabangladeshi wanane pia kutokuwa na viza rejea na Mwingereza mmoja aliyeshindwa kulipa viza.

  Aidha, Kiondo aliongeza kuwa kwa mwaka huu tayari kituo hicho kimetoa viza 327 zenye jumla ya dola za Marekani 17,610 (Sh milioni 28) na matarajio ya kituo hicho kufikia Desemba ni kulipisha viza 198 za dola 9,900 (Sh milioni 15.8) hivyo kufanya viza zitakazokuwa zimetolewa kwa mwaka huu kufikia 525 zenye thamani ya dola za Marekani 27,510 (Sh milioni 44).

  “Viza moja ya kawaida ina thamani ya dola za Marekani 50 (Sh 80,000), tumeboresha huduma zetu kwa wateja ili kutoa ushawishi na mvuto kwa wageni wengi wapitie hapa kuingia nchini na kulipa viza ili pato la taifa liongezeke,” alisema Kiondo.

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama aliwapongeza wafanyakazi wa kituo hicho na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa kwani wao ni taswira ya taifa kwa wageni wangiao nchini.

  “Nyie ndiyo mnaotuwakilisha maana mko hapa mpakani kwa hivyo mgeni akifika hapa akiona ukarimu wenu atapata picha ya Watanzania wote, fanyeni kazi kwa moyo wa uzalendo, wakirimuni wageni, epukeni kabisa vitendo vya rushwa kwani ni adui wa haki.”
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nilivyoona hiyo 25 nikadhani unanizungumzia mimi!
   
 3. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Na wewe unahishi kenya?
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mbona wakenya wengi wanaishi tanzania bila vibali?
   
 5. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  usinivunje mbavu mwita2. Du watu wengine kwa masihara na dhihaka!!!!!!
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi ili uishi Kenya unatakiwa kibali? Kumbe mie sielewi chochote kuhusu East Africa Comunity....... Mambo ya CCM, bana...... :)
   
 7. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  watimueni na wao basi. unasema Wakenya tu, kuna Warundi, Wanyarwanda, wacongo, waganda na...... kibao tena siku hizi wengine wanachukua hata pasi za kusafiria. tanzania yetu Kichwa cha Mwendawazimu
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  bado mambo ya kipande system yanawasumbua hii kasumba haitaisha, africa ni moja waachwe bwana
   
Loading...