Wizara ya Nje: Hakuna Mtanzania aliyeshambuliwa Afrika Kusini katika ghasia dhidi ya Wageni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,073
Reaction score
15,350
TAARIFA KWA UMMA (2).jpg
HAKUNA RAIA WA TANZANIA ALIYESHAMBULIWA NCHINI AFRIKA KUSINI

Wizara inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hakuna raia wa Tanzania anayeishi Afrika Kusini aliyeshambuliwa kutokana na ghasia dhidi ya wageni nchini humo (xenophobia).

Aidha, Wizara inauhakikishia umma wa Watanzania kuwa picha mjengeo (Video clips) zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha raia wa Tanzania akishambuliwa nchini Afrika Kusini ni upotoshaji unaofanywa na watu wenye nia ovu.

Picha hizo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii ni za mwaka 2023 na zimehaririwa upya na watu wenye nia ovu na kuzihusanisha na matukio ya sasa yanayoendelea nchini humo.

Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umefanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya za Watanzania katika majimbo Tisa na kuhakikishiwa kuwa hakuna Mtanzania yeyote aliyeshambuliwa nchini humo kutokana na uraia wake wa kigeni.

Wizara inatoa rai kwa waandaa maudhui mitandaoni kuhakikisha kuwa wanakuwa na taarifa sahihi kabla ya kusambaza katika mitandao ili kuepuka kuzusha taharuki zisizo za lazima kwa jamii.

Ubalozi wa Tanzania unaendelea kushirikiana na mamlaka husika nchini Afrika Kusini kuhakikisha kuwa Watanzania nchini humo wanaendelea kulindwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za kimataifa.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
 
Kwahiyo wao wapo special kukanusha kila kitu ...
Yule jamaa tulieona akiambiwa akimbie ni mnyarwanda?
Haya vipi kuhusu watanzania wanaopata madhira uarabuni!? Wizara imewahi kuchukua hatua gani?
 
HAKUNA RAIA WA TANZANIA ALIYESHAMBULIWA NCHINI AFRIKA KUSINI

Wizara inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hakuna raia wa Tanzania anayeishi Afrika Kusini aliyeshambuliwa kutokana na ghasia dhidi ya wageni nchini humo (xenophobia).

Aidha, Wizara inauhakikishia umma wa Watanzania kuwa picha mjengeo (Video clips) zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha raia wa Tanzania akishambuliwa nchini Afrika Kusini ni upotoshaji unaofanywa na watu wenye nia ovu.

Picha hizo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii ni za mwaka 2023 na zimehaririwa upya na watu wenye nia ovu na kuzihusanisha na matukio ya sasa yanayoendelea nchini humo.

Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umefanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya za Watanzania katika majimbo Tisa na kuhakikishiwa kuwa hakuna Mtanzania yeyote aliyeshambuliwa nchini humo kutokana na uraia wake wa kigeni.

Wizara inatoa rai kwa waandaa maudhui mitandaoni kuhakikisha kuwa wanakuwa na taarifa sahihi kabla ya kusambaza katika mitandao ili kuepuka kuzusha taharuki zisizo za lazima kwa jamii.

Ubalozi wa Tanzania unaendelea kushirikiana na mamlaka husika nchini Afrika Kusini kuhakikisha kuwa Watanzania nchini humo wanaendelea kulindwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za kimataifa.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Template ya kukanusha inakuwepo hapo ni kupachika tarehe tu
 
Back
Top Bottom