Watano wauawa huko Nyantorotoro - Geita

Kwanza uwe na adabu!
Mods huwa hawapotoshi,wako hapa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa humu jukwaani!

Wanaweza ku-verify mahali husika na kuweka sawa kama jambo halieleweki vizuri na mleta mada kama hili lako!

Lakini pia sisi wanachama wa jf tunaruhusiwa kufuatilia jambo na kuwaeleza mods kama unaweza kufanya hivyo kama kuna utata!

Sasa ngoja tukusaidie hili jambo vizuri,

Kwanza hakuna gaidi aliyeua,wala aliyeuawa!

Pili Watu waliouawa ni watano na ni vibaka ambao jana wallikwenda kuvamia msibani na kukwapua sahani iliyokuwa na fedha za rambirambi shilingi 67,000 na wakaondoka nazo!

Tatu baada ya kuondoka uongozi wa Sungusungu wa katika kijiji hicho walianza msako na kubahatika kumpata mmoja wao ambaye baada ya kumhoji alikiri na kuwataja wenzake wanne!

Baada ya kuwataja wakakamatwa na sungusungu,wakati wanaendelea kuhojiwa wananchi wakapata taarifa wakawafuata wakaanza kuwasahambulia kwa mawe na silaha zingine za jadi!

Mmoja alivunjwa miguu yote wawili,waliotambuliwa majina ni wawili,mmoja ametambuliwa kwa jina moja na wengine bado hawajatambuliwa jina hata moja!

Hao ni vibaka,wawili waliotambuliwa majina nimMarwa Chacha,Shija Mlingwa,Ezekiel,wakazi wa nyantorotoro wawili hawajafahamika.

Polisi wanawashikilia watu watatu akiwemo wa kiongozi mmoja wa sungusungu,wanaume wote wamekimbia familia zao kwa hofu ya kukamatwa.

Haya ni maelezo kamili niliyoyapata kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Leonard Paul katika mahojiano kati yangu na yeye kwa njia ya simu!

mtoa mada alitaka tu kupamba habari ili ipate sapoti ya wana JF!

Kwa hiyo mods mnaweza kubadili kichwa cha habari vyovyote vile kulingana na hayo maelezo niliyowapa hapo juu,tusipende kuwapa watu presha huu ni mwisho wa mwaka.

Mimi naongelea waliouwa wewe unaongelewa waliouawa. Waliouwa ni magaidi kuna sheria gani ya kuuwa watu watano eti kwa kuwa ni vibaka? huo walifanyiwa kama si ugaidi ni nini?

Ingekuwa mod hajakosea asingeondoa neno "Majambazi" aliloliweka badala ya magaidi.

Mimi nasema tena kwa kinywa kipana waliouwa ni magaidi. Kutoa roho za watu watano kwa kisingizio kuwa wameiba elfu sitini huo ni ugaidi tena wa hali ya juu.

Kwanini mnakataa hao waliouwa wasiitwe magaidi?
 
Mimi naongelea waliouwa wewe unaongelewa waliouawa. Waliouwa ni magaidi kuna sheria gani ya kuuwa watu watano eti kwa kuwa ni vibaka? huo walifanyiwa kama si ugaidi ni nini?

Ingekuwa mod hajakosea asingeondoa neno "Majambazi" aliloliweka badala ya magaidi

Mimi nasema tena kwa kinywa kipana waliouwa ni magaidi. Kutoa roho za watu watano kwa kisingizio kuwa wameiba elfu sitini huo ni ugaidi tena wa hali ya juu.

Kwanini mnakataa hao waliouwa wasiitwe magaidi?

Inaonekana wewe ni gaidi na wafuasi wako hao ndio maana umeng'ang'ania hilo neno huku ukihusisha na uislamu!

Jambazi kabisa ww!!
 
Inaonekana wewe ni gaidi na wafuasi wako hao ndio maana umeng'ang'ania hilo neno huku ukihusisha na uislamu!

Jambazi kabisa ww!!

Uzuri ni kwamba waliuouwa wote hakuna Muislaam na wanaoshikiliwa na Polisi hakuna Muislaam. Hapo sasa, huo Uislaam labda uuhusishe wewe.

Waliouwa watu watano ni magaidi.
 
Back
Top Bottom