Watangazaji waiponza Times FM

djesco

Senior Member
Jun 26, 2013
166
52
Kituo cha Redio cha Times FM kimetozwa faini ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni moja na kupewa onyo kali kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya TCRA, Margareth Munyagi, alisema ‘Times FM' imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua Tatu' kinachosikika saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani', kilichosikika mchana wa Agosti 29, 2014, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono, na kukiuka maadili ya utangazaji..

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri lakini kinyume na chake, zilitangazwa muda ambao vipindi hivyo vingewezwa kusikilizwa pia na watoto.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao. Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri. Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.

Wavuti
 
Times ni majanga, kuanzia Dida hadi kina misana. Mi mwenyewe kipindi cha pillow talk nasikia kukereka nikikisikiliza. Dida nae anatukana mchana kweupe. ana hasira sana na watu fulani yaelekea
 
ndugu we acha tu!!!!!!! kwa jinsi dida anavotukana mpaka mtu unaona aibu,mie nungekuwa mkurugenzi wa hii redio hiyo milioni wangelipa wao kwa kuwakata kwenye mishahara yao,pia kuna haja ya kuangalia mitaala inayotumika kufundishia hawa watangazaji uchwara maana yawezekana wanafundishwa matusi huko vyuoni
 
TCRA haina tofauti na TBS ukitaka kufungua station dar unaambiwa freequency zimejaa ukiingiza mkono mfukoni unapata masafa. Ni wababaishaji tu kama matapeli wa mtaa wa kongo na wauza mche wa sabuni kuwa ni simu huko aggrey kariakoo.
 
Katika Radio Niliyoona Kaka Yangu FREDWAA Amepotea Basi Ni Times Fm Sijui Akuona Radio Zingine?.
Kapoteza Mashabiki Wote.
 
Katika Radio Niliyoona Kaka Yangu FREDWAA Amepotea Basi Ni Times Fm Sijui Akuona Radio Zingine?.
Kapoteza Mashabiki Wote.
Duh.!!!!
Huyu jamaa yupo huko nilikua sijui aisee.
Hiyo Radio sijui inasikika mikoa gani.
 
Kituo cha Redio cha Times FM kimetozwa faini ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni moja na kupewa onyo kali kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya TCRA, Margareth Munyagi, alisema ‘Times FM’ imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua Tatu’ kinachosikika saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani’, kilichosikika mchana wa Agosti 29, 2014, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono, na kukiuka maadili ya utangazaji..

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri lakini kinyume na chake, zilitangazwa muda ambao vipindi hivyo vingewezwa kusikilizwa pia na watoto.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao. Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri. Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.

Wavuti
 
TCRA haina tofauti na TBS ukitaka kufungua station dar unaambiwa freequency zimejaa ukiingiza mkono mfukoni unapata masafa. Ni wababaishaji tu kama matapeli wa mtaa wa kongo na wauza mche wa sabuni kuwa ni simu huko aggrey kariakoo.
amna cha maana hawa baada ya kuwafungia vodacom wezi wao wanadili na matusi kwani wamewatukana nyie? Maadili tanzania ya sasa amna cha maadili
 
Back
Top Bottom