nyamujulemukama
Senior Member
- Jul 13, 2013
- 147
- 64
Na upuuzi mwingi unaoandikwa na magazeti ya udaku nayo yachukuliwe hatua
TCRA isiishie Radio kuna magazeti ya udaku yanaweka picha chafu tena front page waingie mtaani watayaona.
Na upuuzi mwingi unaoandikwa na magazeti ya udaku nayo yachukuliwe hatua
Wamekisimamisha au watakisimamisha?
Times ni majanga, kuanzia Dida hadi kina misana. Mi mwenyewe kipindi cha pillow talk nasikia kukereka nikikisikiliza. Dida nae anatukana mchana kweupe. ana hasira sana na watu fulani yaelekea
Times hawana ubavu wa kumletea kibesi Dida, Kipindi chake ndo kinachosikilizwa na watu wengi zaidi na kina matangazo mengi ya biashara...nani hataki pesa?
Ila yule kapinda...
Kituo cha Redio cha Times FM kimetozwa faini ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni moja na kupewa onyo kali kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya TCRA, Margareth Munyagi, alisema ‘Times FM' imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua Tatu' kinachosikika saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani', kilichosikika mchana wa Agosti 29, 2014, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono, na kukiuka maadili ya utangazaji..
Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri lakini kinyume na chake, zilitangazwa muda ambao vipindi hivyo vingewezwa kusikilizwa pia na watoto.
Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao. Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri. Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.
Wavuti
Wamekisimamisha.
Walisema watakisimamisha
Kisiposimama sijui itakuwaje
radio free africa,mthe sound of africa, kati ya radio zangu bora kabisa, angalia vipindi vyao.
si hao wengine saa12-4, PB, 4-7, leo tena, 7-10, xxl, 10-1 jahazi, 1-3 amplifer, kila siku hivyo hivyo tu bire kabisa.
Clouds Fm the people station number 7 the best radio in Africa
TCRA isiishie Radio kuna magazeti ya udaku yanaweka picha chafu tena front page waingie mtaani watayaona.
Times hawana ubavu wa kumletea kibesi Dida, Kipindi chake ndo kinachosikilizwa na watu wengi zaidi na kina matangazo mengi ya biashara...nani hataki pesa?
Ila yule kapinda...
radio free africa,mthe sound of africa, kati ya radio zangu bora kabisa, angalia vipindi vyao.
si hao wengine saa12-4, PB, 4-7, leo tena, 7-10, xxl, 10-1 jahazi, 1-3 amplifer, kila siku hivyo hivyo tu bire kabisa.
dida ndo kila kitu anawashika mbaya wamama wa mjin
saa sita ngiiiiiii
kitu kimeanza DAR NZIMA
MI dida namkubali mwanamke kujiamini
Clouds Fm the people station number 7 the best radio in Africa
Clouds Fm the people station number 7 the best radio in Africa
Mbona kama unazunguzia kitu kingine badala ya kipindi? Au mimi ndio sielewi?!Kisiposimama sijui itakuwaje